Aibu ya mwaka yampata Lissu!

Aibu ya mwaka yampata Lissu!

Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. Jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.

Lissu na genge lake la wahuni watafute uongo mwingine, maana huu wa upotoshaji juu ya hati ya muungano hauna tena soko. Tuipe pongezi Ikulu kwa kukata mzizi wa fitina.
Hii ni hatari ndio maana wakawaacha waongee hadi watoke mapovu alafu waitoe
 
Hivi bila mawazo ya Nyerere na Karume huwezi fanya chochote? mawazo mgando haya. Uliambiwa kuwa hao ndo Mungu? Angalia zama kijana na hiyo si misahafu kwamba lazima tuendelee kuishi kama walivoweka wao.

I don't care about Nyerere nor Karume!! Nashangaa wewe na wanasiasa uchwara mnataka hati miaka 50 baada ya muungano. Hivi kwa akili yenu muungano ungeweza kuepo bila articles of union???
 
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. Jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.

Lissu na genge lake la wahuni watafute uongo mwingine, maana huu wa upotoshaji juu ya hati ya muungano hauna tena soko. Tuipe pongezi Ikulu kwa kukata mzizi wa fitina.
CHADEMA ni chama cha waendawazimu. Wao hawajui siasa za propaganda hazina nafasi tena. Hoja ya Muungano itawaacha hoi bin taaban. Wawaulize wenzao CUF kilichowapata. Na tena CHADEMA 2015 kitafutika katika ramani.
 
naamini kuna na wengine ambao kama ulivyo wewe, hamkumwelewa tundu lissu alikuwa anasema nini. Ila kwa tuliomwelewa anachokifanya kinakubalika.

Kupatikana kwa hati ya muungano siyo kitu kigumu kiasi cha serikali bila aibu kudai iko un! Kwamba mnataka tueleweje? Ukipangishwa nyumba mkataba anakaa nao mwenye nyumba au?

Chochote ambacho kilisemwa ni baada ya kigugumizi cha serikali kuitoa hati hiyo, hata pale ambapo iliombwa na kamati za bunge maalum la katiba! Ni serikali ya ajabu na iliyojaa upuuzi inayoweza kufanyia mzaha hata swala kama hilo. Vinginevyo ni wazi kuwa nia ya serikali haikuwa njema kwa kuificha hati hiyo.

Hata sasa, pamoja na kutolewa kwa hati hiyo kila mwenye akili timamu anapaswa kujiuliza hati hiyo ilikuwa wapi? Na huko ilikokuwa ilikuwa inafanyiwa nini ndo itolewe leo? Ni kweli watanzania wanapaswa kuiamini hati hiyo? Je! Hati hiyo iliyotolewa pamoja na kufichwa kote huko ni hati halisi na halali?

Nasikitika kuna wanaofikiria kama wewe out there!

hukuelewa maelezo ya katibu mkuu kwanini wanaificha sana?
 
Pinga kwa hoja mkuu usiwe na majibu mepesi. Lissu alijenga hoja na kuonyesha mifano ule ni utafit tosha. unapopinga njoo na hoja yako usikae na kusema mwongo. think big mkuu
 
Ni aibu kwa Ikulu kutoa hati hiyo baada ya watu kuidai kwa nguvu kubwa.

Kifuatacho ni kujibu maswali haya ya Lissu

1.Je,hati hiyo ni halali

2.Kama hati hiyo ni halali,je muungano huu ni halali?

Hayo ndio maswali ya Lissu yanayosubiri majibu

mbona very simple usingekuwa halali usingedumu miaka hamsini
 
Sasa mkitaka kujua lisu name mnyika no noma ngoja waipate hiyo hati Kama itakuwa yenyewe uone watakavyo ichambua
 
Ni aibu kwa Ikulu kutoa hati hiyo baada ya watu kuidai kwa nguvu kubwa.

Kifuatacho ni kujibu maswali haya ya Lissu

1.Je,hati hiyo ni halali

2.Kama hati hiyo ni halali,je muungano huu ni halali?

Hayo ndio maswali ya Lissu yanayosubiri majibu

Kwa hiyo hiyo hati ilikuwa ikulu!!?? Je huko ndiko mahali ilipotakiwa kuwa ama ......... just being curious!!
 
Kuhoji uhalali wa Muungano na kuifanya agenda baada ya kudumu kwa miaka hamsini badala ya kujadili mambo ya maana ni upuuzi.

Ulimwengu mzima unajua Tanzania ni jamhuri ya Muungano. Pande zote mbili kwa miaka 50 wame practice Muungano kuanzia waasisi.

By conduct huo ni Mkataba.

Kwa maneno pia hiyo sio hoja, objective approach when invoked overrides the black letters.

Tuache kupoteza muda, wajumbe wajielekeze kwenye maboresho au mabadiliko ya uahirikiano na matatizo ya watu.
 
Je muungano huu ni halali?
Hati hii ni halali?
Sahihi ya nyerere ni halisi?
Sahihi ya karume ni halisi?
Hao akina Lissu, Jussa wenzao na wale wazee wa Pemba wanaodai hati ya makubaliano ya muungano utadhani ni majuha. Nyerere na Karume walisaini makubaliano hadharani na kumbukumbu za kitendo hicho ziko kwenye still na moving pictures. Hata kama hati ya makubaliano iliyotiwa sahihi ingepotea sio sababu kusema eti muungano ni batili kwa kua tu hati ya makubaliano haijulikani ilipo. Ni majuha tu wanaoweza kushikilia bango eti muungano ni batili baada ya miaka 50 kwa kua wanaamini hati hiyo imepotea.
 
Laiti ungalikua na uelewa mdogo wa sheria ingekusaidia sana mkuu,sawa hata kama hati imeonyeshwa japo bado inaacha mashaka is it valid? If not then can be void ab initio,hence again no contract at all

Hapa unachanganya mambo ebu, pitia Parol evidence rule /Extrinsic uone inasema nini juu ya mikataba, ambayo kimsingi parties wameridhiana na baada ya hapo wakayaweka yale makubaliano katika maandishi.

Kwa kifupi Parole evidence inasema kwamba ikiwa watu wamekubaliana kwa maana ya kuwa wameingia mkataba juu ya mambo waliyokubaliana na kisha wakayaweka yale makubaliano yao katika maandishi,na kutiliana saini haiwezekani tena mtu wa tatu au mmoja wa wale walioingia mkataba ule kudai kwamba contents za makubaliano yale ni batili.
 
Hoja muhimu kuliko zote, hata kama hati ipo, je, lipo wapi azimio la baraza la mapinduzi kuidhinisha muungano? Kama halipo zanziba hawakuridhia muungano kihalali


MUUNGANO.jpg


Kutokana na mvutano huu, gazeti hili [Mwananchi] limefanya mahojiano maalumu na aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi mwaka 1964, Salum Rashid ili kupata ufafanuzi wake juu ya jambo hilo hasa baada ya Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa kueleza anayojua kuhusu suala hilo.

Swali: Ni changamoto zipi hizo ambazo tangu mwanzo, zilionekana?
Jibu: Kuna mengi, lakini kikubwa ilikuwa ni usiri wa jambo hili, kwani mimi kama Katibu wa Baraza la Mapinduzi sikujua ila hili la Zanzibar kumezwa tangu wakati huo lilionekana.

Swali: Je, kidogo una ufahamu ilipo Hati ya Muungano? Kuna ambao wanasema ipo Umoja wa Mataifa, wewe unasemaje kwani ulikuwa kiongozi wa Serikali wakati huo?
Jibu: Ninachokumbuka ni kwamba hati haikupelekwa Umoja wa Mataifa (UN), bali kilichopelekwa ni taarifa ya ya kuungana Tanganyika na Zanzibar.

Swali: Katika Bunge linaloendelea sasa kuna mijadala mingi imeibuka kuhusiana na hati ya sheria ya Zanzibar kuridhia Muungano je, una taarifa gani juu ya hati hii?
Jibu: Hati ya Sheria ya Zanzibar Presidential Decree kukubali Muungano, hiyo haipo na wala wasihangaike kuitafuta.


Swali: Kuna hati ya sheria namba 22 ya mwaka 1964, ilisainiwa kwa upande wa Tanganyika na Rais wa Tanganyika wakati huo, Hayati Julius Nyerere, Katibu wa Bunge Pius Msekwa na Spika wa Bunge hilo, Adam Sapi Mkwawa, Aprili 25 mwaka 1964. Je, kwa upande wa Zanzibar hamkupata hati hii?

Jibu: Mimi kama Katibu wa Baraza sijawahi kuiona hiyo Sheria (Presidential Decree) ambayo ilipaswa kusainiwa na Rais wa Zanzibar hayati Abeid Karume na mimi. Mimi ndiye nilikuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Baraza halikuwahi kuridhia Muungano, kilichofanyika ni kupewa taarifa tu .

Swali: Je, unadhani ni kwa nini sheria hii haijasainiwa na wewe?
Jibu: Unajua haya mambo yalikuwa siri sana na kuna mambo mengi yanapotoshwa kuhusu muungano..

Swali: Je, hujawahi kuona Hati ya Muungano na wewe ulikuwa kiongozi mkubwa wa serikali wakati huo?
Jibu: Mimi niliona ile draft (rasimu) ya kwanza ya muungano na nilipoiona nikiwa na hayati Karume nilimshauri vitu vingi na tulirekebisha na baadaye ilirudi Dar es Salaam.

Swali: Je, baada ya kukamilika uliwahi kuiona tena?
Jibu: Hapana, sijaiona nilikuwapo Zanzibar wakati huo, lakini jambo hili baadaye lilifanywa siri kubwa sana, Nyerere hakutaka mtu yeyote ajue na upande wetu Zanzibar hatukupata ushauri wa kisheria hata Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alikuwa hana taarifa, lakini Tanganyika walikuwa na ushauri wa kisheria.

Rashid: Muungano ulikuwa siri ya Nyerere na Karume - Katiba - mwananchi.co.tz
 
Ogopa sana kuingia madarakani au kupata nafasi za kisiasa kama hisani hata mkuu akijamba unampa hongera sana boss, ccm wanadhani watatawala hii nchi milele hoja zenu ni dhaifu sana mnatoa mapovu tu, akili gani unashindwa kutofautisha kama yale ni maoni ya watanzania na si ya walioba ? Muwaseme watanzania waliopendekeza serikali 3 na si kuwasakama wajumbe mnaona raha kupiga vigeregere kama mko kwenye kitcheni party !aibu kwenu na mkuu wenu asiyejitambua,
 
Baada ya upotoshaji mkubwa kufanywa bungeni na watu wasio itakia nchi yetu mema wakiwa wameongozwa na Tundu Lissu. Sasa watu hao wamepata aibu ya mwaka baada ya Ikulu kusambaratisha upotoshaji wao.

Tundu Lissu na genge lake la waongo wamekuwa wakipotosha bungeni kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar haupo kisheria kisa hakuna hati ya muungano huo. Jambo ambalo limepingwa vikali na Ikulu tena kwa kutoa uthibitisho wa uwepo wa hati hiyo ya muungano.

Lissu na genge lake la wahuni watafute uongo mwingine, maana huu wa upotoshaji juu ya hati ya muungano hauna tena soko. Tuipe pongezi Ikulu kwa kukata mzizi wa fitina.
Majanga!
 
I don't care about Nyerere nor Karume!! Nashangaa wewe na wanasiasa uchwara mnataka hati miaka 50 baada ya muungano. Hivi kwa akili yenu muungano ungeweza kuepo bila articles of union???

Man I like this point. The truth is, it's absurd to think that all that time there was no an article of union!

Yani ni jambo la ajabu kuona wapo Watanzania wanaamini maneno ya wahuni kama Lissu! Seriously!

Binafsi nilidhani tumejitahidi kupigana na adui ujinga, ila kwa huu ujinga ulioonyeshwa na Watanzania walio muamini Lissu, naona serikali inapaswa kufanya kazi ya ziada.
 
Kama ujui kusoma hilo sio tatizo langu.

Jambo la kufanya ni kuwalaumu wazazi wako ambao wameshindwa kukusomesha.

Who knows, huenda hata wazazi wako hawakwenda shule so hawakuona umuhimu wa ikukupeleka shule.
Duh wewe ndo umekwenda shule ukamaliza hadi tuishen.Sijui kama unafahamu unaweza kusoma usielimike..na hili ndo nnaloliona kwako!
 
Je muungano huu ni halali?
Hati hii ni halali?
Sahihi ya nyerere ni halisi?
Sahihi ya karume ni halisi?

Ile saini haiwezi kuwa ya Amri Abeid Karume, ila kuna mtu kasaini kwa niaba yake. Niliwahi kusoma mahali kuwa Karume 'hakusoma; lkn ile saini iloyopo kwenye hati iliyoonyeshwa na Balozi Sefue inaonekana ni ya msomi wa hali ya juu kuliko hata Nyerere wakati ule.

Ile hati itazidisha utata zaidi badala ya kuundoa kwa maswali yafuatayo(
1. Kwa nini walikuwa wanadao mara iko UN?
2. Kwa nini awali waliwapa wajumbe wa Kamati hati nyingine ambayo haifanani na hii aliyeionyesha Sefue leo? Je! Kuna hati ngapi za Muungano?

-------- huamini kila neno, lkn mwenye akili huhoji kila neno.
 
Back
Top Bottom