..nilisoma kitabu cha "the making of african statesman:moi"
alielezea ratiba yake kama mtu anayeamka mapema zaidi na kulala late zaidi .....na hakuna mzaha kati kati.....
Saa 10.00 alfajiri kila siku huamka na kusali kwa dk 30.....
Saa 10.30 kamili hufanya mazoezi ya viungo [dk 30]
saa 11 kamili huoga na kuvaa [dk 30]
saa 11.30 hupata kifungua kinywa [uji na maziwa]..ets na kuelekea ofisini
saa 12 kamili bendera ya jamuhuri inapopandishwa yeye tayari huwa ofisini
na kazi ya kwanza aliyokuwa akifanya ni kuwasiliana na wakuu wa ulinzi na usalama kupata taarifa,,...
Baada ya hapo ratiba yake ya kazi za ofisini hukamilika saa 12....hurudi nyumbani na kupumzika kidogo ...saa mbili kamili hupata mlo..na kuendelea na vikao na wasaidizi wake hadi saa 4 usiku au 5..baada ya hapo hupata muda wa kusoma taarifa ya kazi zake za kesho aliyoandaliwa na msaidizi wake....
Mara nyingi inaelezwa kuwa alikuwa akilala saa 7 hadi 8 kila siku..........na wala haikuwa ajabu kuwa na miadi ya kikazi hadi saa 6 usiku.....
Nadhani ratiba kama niliyoieleza hapo juu ni kielelezo tu cha ratiba za viongozi waliodhamiria ....haitatofautiana na ya mwalimu...,na wengine kama hao.....
Tatizo na viongozi ambao ikifika usiku kama saa hizi badala ya kufanya tafakari ......huyoo anajiiba kwenda kariakoo kucheza dhumna na maswahiba ....ambao hawana la kumshauri..au kona kona!!