Aibu kwa Waandishi wa Habari na Udhalilishaji wa Taaluma yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aibu kwa Waandishi wa Habari na Udhalilishaji wa Taaluma yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Filipo Lubua, Mar 13, 2013.

 1. Filipo Lubua

  Filipo Lubua Verified User

  #1
  Mar 13, 2013
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wadau,

  naombeni muniwie radhi ila leo sina budi kuwadisi waandishi wa habari wa Tanzania. Nimesoma kwenye gazeti la Mwananchi kuwa eti Waandishi Wanakutana na Dola Kujadili Usalama

  Unakwenda kujadili usalama wako na mtu huyohuyo anayeuhatarisha? Dola hiyo hiyo iwapigao mabomu, iwatekao na kuwamwagia tindikali, iwapigao risasi na kusema iliwadhania ni majambazi, dola hiyohiyo iwacharangayo mapanga, iwatoboayo macho! Dola hiyohiyo?

  Tangu lini panya wakakaa kikao cha usalama na paka? Au vipi swala na simba wakakaa kikao kwa ajili ya kujadili usalama? Hilo lawezekana?

  Waandishi wa Tanzania hawajaungana! Alimwagiwa tindikali Kubenea na mwenzake Ndimara Tegambwage kucharangwa mapanga, waandishi walikaa kimya na sikuona la maana walilofanya kulaani kuteswa kwao! Likafungiwa gazeti la Mwanahalisi, sijaona la maana walilofanya kuilaani serikali! Akauawa Mwangosi kwa bomu, sijaona la maana walilolifanya kuilaani serikali! Alipigwa Risasi Mhariri wa Business Times, hakuna la maana walilolifanya! Sasa eti Kibanda, Mwenyekiti wao, ametobolewa jicho na kung'olewa meno eti wanakaa na dola kujadili amani!!! Amani ipi?

  Hawa ndio wasaliti wa Absalomu Kibanda! Ndio wasaliti wa Kubenea; Hawa ndio wasaliti wa Mwangosi; Hawa ndio wasaliti wa taaluma nzima ya uandishi wa habari.... Badala ya kuchukua hatua madhubuti, wanabaki tu kuandikaandika vimakala vya kuilaani serikali!! Makala! Pachimbeni pachimbike! Hivyo ndivyo amani yenu itakavyopatikana na wala si kukaa meza moja na dola ambayo ndo yawatendea vitendo viovu!! Nasema pachimbeni; pachimbeni pachimbike!!
   
 2. Sefet

  Sefet JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2013
  Joined: Dec 23, 2012
  Messages: 470
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nahisi hawajitambui...!!
   
 3. Kaisari

  Kaisari JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2013
  Joined: Nov 13, 2012
  Messages: 2,424
  Likes Received: 1,205
  Trophy Points: 280
  Labda wanaenda kuomba msamaha! (They go for reconciliation)
   
 4. kashesho

  kashesho JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2013
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 4,747
  Likes Received: 962
  Trophy Points: 280
  hawana umoja
   
 5. Filipo Lubua

  Filipo Lubua Verified User

  #5
  Mar 13, 2013
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kamanda, reconciliation kwani wana ugomvi na nani? Waombe msamaha wamemkosea nani?
   
 6. i

  iseesa JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sioni ubaya Mkuu. Panya kukaa na paka ni moja ya mikakati ya kumshinda paka. Kwanza utaiona taswira ya huyo paka yukoje? ana mapungufu gani? Ni mzee au kijana? ni mnafiki au ni mkweli? Kumbuka mbinu za mwanafalsafa Socrates za kumjua mtu kwa kumuuliza MASWALI-DADISI.
   
 7. p

  pilau JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2013
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  :deadhorse: :deadhorse: :deadhorse: :deadhorse:
   
 8. Filipo Lubua

  Filipo Lubua Verified User

  #8
  Mar 13, 2013
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Yawezekana, ila mbona matukio yamekuwa mengi sana? Tangu Kubenea hadi leo, si haba nduguye!
   
 9. M

  Mkempia JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2013
  Joined: Mar 5, 2013
  Messages: 1,138
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hakuna waandishi hapo, bali kuna waganga njaa! tuwe wakweli kwa hili. mfano mdogo tu umewahi kumuona Jenerali ulimwengu anahudhuria mikutano kama hii??
   
 10. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2013
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,686
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  For the record ni kitu kizuri waandishi wamefanya.....

  Mwisho wa siku bado hii ni nchi yenye mifumo rasmi japo dhaifu lakini ndio nchi yetu tena na sidhani kama walikuwa na kwingine kwa kwenda.

  Ila kwa mambo uliyoyataja kweli waandishi wa habari wetu ni wanafiki sana na wachumia tumbo hadi kusalitiana!!
   
 11. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2013
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,567
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  -Waandishi hawa wa Tanzania sijui!!tatizo kila mmoja anajiona yuko salama,mpaka pale linapomkuta
  yeye ndipo wanajua kumbe hatuko salama.
  -Waandishi hawa ambao wanaandamana halafu jukwaa la wahariri wanamwalika Nchimbi ndiye aje
  kupokea maandamo ya kupinga kuuawa mwenzao na askari walio chini ya huyo Nchimbi!!
  -Waandishi wa hawa wa Tanzania ambao kwa sasa ukipiga simu kwenye chombo cha habari kuwa
  kuna tukio au mikutano ya jamii wanataka waahidiwe kila mmoja si chini ya 50,000 ndipo waje na
  watoe hiyo habari!!
  -Waandishi ambao walimwambia Kubenea alijitakia, kwa kutoa habari za uoenevu juu ya raia!!!
  -Waandishi wa Tanzania ukombozi wao baaado sana kwani hawajajitambua'

   
 12. E

  ESI JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2013
  Joined: Dec 15, 2012
  Messages: 739
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wajinga njaa zimewajaa tumboni. Hata Jerry Mulo nasikia walimlipua wenyewe kwa Wenyewe hata hii ya kibanda wako kimya.
   
 13. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2013
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,515
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Adui yako mpende!
   
 14. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2013
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,102
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Nimesoma mapaka naisi moyo unaumwa kwani vitu viumiza sanaaaaaaaaaaa ( afande mshuti )
   
 15. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2013
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 14,089
  Likes Received: 2,922
  Trophy Points: 280
  Hawajui kuwa Kesi ya Jerry Muro ilibambikwa na polisi?TIDO MHANDO jee?siku zote dola na media huwa havikai chungu kimoja,vinginevyo uwe mtumwa
   
 16. Mromboo

  Mromboo JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2013
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 775
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  yataka moyo kuwakubali wanahabari wa Bongo!!!
  napita tuu mkuu.
  :crying:
   
 17. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2013
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Kaangalieni youtube ya lwakatare ndo mjue mchawi wa waandishi wa habari ni nani
   
 18. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26,918
  Likes Received: 44,768
  Trophy Points: 280
  Watanzania kwa ujumla wetu tuna tatizo la "kiasili" ambalo ni common kwa watanzania wote!Sisi watanzania kwa ujumla wetu pamoja na hao waandishi wa habari ni watu ambao hatuna asili ya kuwa na sauti na nguvu ya pamoja kama umma wa watanzania katika kupinga na kupambana na udhalimu wa serikali yetu na kibaya zaidi matukio yanakuja na kupita na tunaona sawa tu!Huu udhaifu ndio serikali wanaoutumia kututawala kwa mtindo huu wa "kimafya".

  Tusipobadilika, hata nchi itauzwa!
   
 19. master peace

  master peace JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 1,451
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Filipo Lubua ulichokiandika ndo ukweli kabisa, nashindwa kuelewa kwa nini hawa waandishi wa habari hawajitambui, yumkini hili limetokana na shule za kuunga -unga bila kufuata mitaala inayo eleweka, hata kama ndivyo bado haitoshi kwanini wasijifunze kutokana na makosa? Kwa nini wasiangalie wenzao wa nchi zingine wanachukua hatua gani yanapotokea matatizo kama haya yanayowakuta? Kwa mfano leo nimesikiliza taarifa ya habari, waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari vya binafsi nchini Mali wamegoma kutangaza habari yoyote ile kwa sababu kiongozi wao amekamatwa na vyombo vya dola.
   
 20. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2013
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,863
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Mkuu threed yako yaumiza ina mistari michache lakini yote ni MKUKI MOYONI UMEINGIA
   
Loading...