Aibu kwa Waandishi wa Habari na Udhalilishaji wa Taaluma yao

Kuna msemo wa kiswahili chetu sanifu unasema Mchawi mpe mwanao amlee, lakini hii haiendani kabisa na hali ya leo maana wanaweza wakakupa ulinzi na kukumalizia mbali na mlinzi waliye kupa. Suluhisho ni Kuiambia dunia kabisa maana kama haki ya mwanahabari haipo basi hamna maisha kwa mwanadamu wa kawaida bali ni kukandamizana kwa kwenda mbele
 
Badala ya kuchukua hatua madhubuti, wanabaki tu kuandikaandika vimakala vya kuilaani serikali!! Makala!
Si bora hata hivyo vimakala vingekuwa vina last kidogo, wanaandika siku mbili ya tatu wamesahau. Nani anaandika ya Mwangosi tena?

Siku MWANAHALISI lilipofungiwa siku kama tatu baadae tunasoma "JK awaalika wahariri Ikulu," I was thinking mnaitwa Ikulu kufanya nini na gazeti lenu lishafungiwa? Wakaenda kupozwa vi juice vya mapapai vya uarabuni vina seviwa na ma bar maid wa Ikulu wakajisikia raaaaha! Wakasahau ya MWANAHALISI, and I hope Kubenea hakwenda kwenye kile ki meeting. Shame on those guys, no backbone at all, press ya Tanzania ni so crummy.
 
Mkuu,

Nadhani hili haliwezi likamhusisha mwandishi mmojammoja, lakini
litahusisha tasnia nzima ya habari. Namaanisha kuwa, hata kama wapo
wanaojitambua, bado hawajachukua hatua madhubuti za kuwaunganisha
waandishi wote na kuchukua hatua kali zaidi licha ya wao kuandika makala
mbalimbali. Swala la uuaji wa waandishi, utekaji na utesaji si la
kuandikiwa makala tu, ni swala la hatua zaidi ya hiyo

ni kweli mkuu Rwakatare na wafuasi wake wachunguzwe sisi waandishi tutoe msaada unaoitajika
 
Ukishangaa ya musa utastaajabu ya....:p si ndio hao hao walimkataa nchimbi pale jangwani wanafki hawa tukisema baadi ya makanjanja wanalamika taaluma za kuunga unga nalo ni tatizo
 
Mtoa mada hiyo "Hatua madhubuti" uayotaka waandishi waichukue mbona huitaji? usiwe mnafiki kama waandishi wa habari funguka, 'pachimbike' maana yake nini? au unaogopa Polisi wataku Lwakatare na wewe? ulkiogopa hilo na wewe ni MNAFIKI
 
Tatizo la watanzania ni moja tuu, hatujui haki zetu. hamna hata mmoja aliyeradhi kujitoa mhanga kwa ajili ya ukombozi wa ndugu zake. hatuko tayari kudai haki yetu kwa gharama yoyote iwayo. Tumebakia kulalama. Waandishi wa habari hatuwezi kuwatenganisha katika uasili huu wa watanzania watawaliwa. Wengi wao ni waoga, wengi wao ni vibaraka wa kundi la watawala na wengi wao hawamjue hata adui yao ni nani, na hata haki yao ni nini,

Kundi ndogo la wanachi wenzetu ambao kwa umbumbumbu wa watanzania kutojua haki zao wanawaita majina kama vigogo na nk limechukua nafasi ya kutukandamiza, kutuuwa na kutufanyia kila lililo baya kwa nia moja tu ya kujenga woga miongoni mwetu. Kundi hili linalotawala ambalo ni waafrika wenzetu, hawana tofauti na mkoloni mweupe tuliomkataa wakati wa kudai uhuru. Mkoloni mjerumani wakati anavamia nchi yetu alikuwa na tabia ya kujenga woga kwa kuwasaka na kuwakamata machifu waliokuwa wakorofi kwa wakati huo na kuwanjonga hadharani. Kitendo hicho kilijenga woga miongoni mwa waafrika ambao hatimaye walitawaliwa kwa mabavu na wajerumao hao. Leo, hii Serikali ya CCM iliyopo madarakani inataka kututawala kidhalimu kwa njia hiyo hiyo ya wakoloni ya kutujengea wago kwa kuwafanyia vitendo viovu watu wanaojaribu kutoa sauti zao kuipinga akina Walimboka, Mwangosi, Kibanda, Kubenea n.k. Waandishi wa habari pekee hawawezi kuleta ukombozi wa nchi hii, kinachotakiwa ni wananchi wote watambue haki zai na wawe tayari kuzipigania kwa gharama yoyote ile. PEOPLEEEEES POWER.
 
Back
Top Bottom