Aibu kwa Waandishi wa Habari na Udhalilishaji wa Taaluma yao

:msela:mkuu taarifa yako ni nzuri san pia ina mashiko sana,siwalaumu waandishi wa habari peke yao bali hata sisi raia wengine tuna asili ya unafiki na uwoga uliokirithiri,tumejijengea utamaduni kwamba huwezi kushinadana na serikali kwa lolote,yaani watanzania wote tumekuwa mabwege wa hali ya juu kwa serikali yetu....kuna kitabu kinaitwa "I WILL MARRY WHEN I WANT " kimeandikwa na Ngugi Wa Thiong na Mirii,yalioandikwa mle ndani maudhui yake yanasadifu asilimia 100 na serikali yetu ya Tanzania inavyowatendea wananchi wake,
ngoja niishie hapo maana machozi yameanza kunitoka
 
Sioni msingi wa hoja,acha kuwafifisha waliowengi kuhusu adui halisi wa waandishi,na ustake wafuate maneno yako kwamba adui yao ni serikali hapana, kaka ukweli karibia uwe wazi,kuna marefarii wanachezesha ngoma ila kwa sasa tayari,mageuzi ya kifikira yamepatikana, waweza danganya mara moja si mara zote,tafakari utepe wa lwakatare
 
jamani mnachangia uzi huu kama vile mnatoka usingizini,waacheni waya zungumze nadhani tunacho takiwa kujadili ni matokeo baada ya mazungumzo hayo
kwakuwa ushahidi wa kimazingira unaonesha kuwa matukio haya hayakufanywa kwa bahati mbaya bali ni mkakati unaoratibiwa, na bado objectives hazijafikiwa!..ninaamini kikao hiki hakitakuwa na tija kwa waandishi wala wanajamii. wataishia kunya chai na kupewa ahadi hewa huku serikali ikijipa umaarufu wa utii bila shurti
 
Wadau,

naombeni muniwie radhi ila leo sina budi kuwadisi waandishi wa habari wa Tanzania. Nimesoma kwenye gazeti la Mwananchi kuwa eti Waandishi Wanakutana na Dola Kujadili Usalama

Unakwenda kujadili usalama wako na mtu huyohuyo anayeuhatarisha? Dola hiyo hiyo iwapigao mabomu, iwatekao na kuwamwagia tindikali, iwapigao risasi na kusema iliwadhania ni majambazi, dola hiyohiyo iwacharangayo mapanga, iwatoboayo macho! Dola hiyohiyo?

Tangu lini panya wakakaa kikao cha usalama na paka? Au vipi swala na simba wakakaa kikao kwa ajili ya kujadili usalama? Hilo lawezekana?

Waandishi wa Tanzania hawajaungana! Alimwagiwa tindikali Kubenea na mwenzake Ndimara Tegambwage kucharangwa mapanga, waandishi walikaa kimya na sikuona la maana walilofanya kulaani kuteswa kwao! Likafungiwa gazeti la Mwanahalisi, sijaona la maana walilofanya kuilaani serikali! Akauawa Mwangosi kwa bomu, sijaona la maana walilolifanya kuilaani serikali! Alipigwa Risasi Mhariri wa Business Times, hakuna la maana walilolifanya! Sasa eti Kibanda, Mwenyekiti wao, ametobolewa jicho na kung'olewa meno eti wanakaa na dola kujadili amani!!! Amani ipi?

Hawa ndio wasaliti wa Absalomu Kibanda! Ndio wasaliti wa Kubenea; Hawa ndio wasaliti wa Mwangosi; Hawa ndio wasaliti wa taaluma nzima ya uandishi wa habari.... Badala ya kuchukua hatua madhubuti, wanabaki tu kuandikaandika vimakala vya kuilaani serikali!! Makala! Pachimbeni pachimbike! Hivyo ndivyo amani yenu itakavyopatikana na wala si kukaa meza moja na dola ambayo ndo yawatendea vitendo viovu!! Nasema pachimbeni; pachimbeni pachimbike!!
wewe unaishi dunia ipi? siku hizi chama kinachopanga na kuteka watu aliwemo kibanda kinajulikana. soma kunathread inajadilia hapa tangu juzi au nenda kwenye u tube utaikuta.
 
nahisi hawajitambui...!!
Walishaambiwa wana uwezo kiduchu wa kufikiri na kuhoji, na sasa wanauthibitishia umma walivyo sasa kuna ubaya gani?
Waandishi na waalimu ndiyo "ngome" ya CCM, wakipewa hata leso za kujifutia jasho utawaona wanavyohangaika na magwanda ya kijani na kuwapamba vibaka wa CCM! miezi miwili tu baada ya chaguzi wenzao hawana habari nao na wanasahauliwa mithili ya kandambili za kwendea vagini!
CCM hoye!
 
Ndugu yangu, wana nguvu ya kufanya hivyo ila tatizo hawajaungana. Ndio maana watatundwa mmojammoja mpaka waishe. Mwishoni watabakia waandishi wa gazeti la Mzalendo, watangazaji wa Radio Uhuru, na wale vibaraka wengine kama akina Ephraim Kibonde.
Nakubaliana kabisa na maneno yako, na ndiyo maana katika tukio lililomkuta Kibanda, vyombo vya habari vilivyolilaani tukio hilo vinahesabika. Nitavitaja miongoni mwake, gazeti la Mtanzania, ambalo ni mwajiri wake, magazeti mengine ni kama vile, Nipashe, Mwananchi na Tanzania daima.

Yapo magazeti ambayo hata ukiangalia vichwa vyake vya habari na uzito walioipa coverage ya hiyo habari, unaweza kujiuliza, hivi na hawa nao wamo kwenye tasnia ya habari?! Nitayataja baadhi ya magazeti hayo kuwa ni, Uhuru, Daily news, Habari leo, Jambo leo na Majira.

Ukija kwa upande wa vituo vya radio, huwa mara nyingi najiuliza kwa mfano Clouds radio, ambayo yenyewe inajiita the people's station, wakati katika tafsiri halisi hiyo radio ilipaswa iitwe the magamba's station!! Kwa kuwa propagandainayopigwa sasa hivi radio hiyo inaizidi hata radio yenyewe ya CCM ya Uhuru!!

Kinachofanyika na watawala hivi sasa ni ile mbinu ya devide and rule, kwa kuwa wanajua miongoni ya waandishi wa habari lazima watakuwepo watu wa design ya Yuda Iskariote, ambao watapewa vipande vichache tu vya pesa, ambavyo vitawafanya hata kama watashuhdia mwandishi mwenzao ametobolewa jicho, wao mradi mkono umeingia kinywani hawatojali!!

Kwa hiyo tunalazimika kumwomba Mungu kwa bidii sana ili aturehemu na kadhia hii kubwa sana inayolikabili Taifa letu kwa hivi sasa.
 
Nakubaliana na kile ulichosema kwa asilimia mia moja. Hasa maswala ya coverage. Ni jambo la ajabu kuona hata magazeti la serikali/wananchi kama Daily News na Habari Leo hayazungumzii habari hii kwa kina, na hilo ndilo liletalo hisia kuwa huu mchezo mchafu unachezwa na vyombo vya dola
 
Mkuu Lubua,

Unamaanisha waandishi wakiwemo Pasco na Rioba? ..........

Mkuu,

Nadhani hili haliwezi likamhusisha mwandishi mmojammoja, lakini litahusisha tasnia nzima ya habari. Namaanisha kuwa, hata kama wapo wanaojitambua, bado hawajachukua hatua madhubuti za kuwaunganisha waandishi wote na kuchukua hatua kali zaidi licha ya wao kuandika makala mbalimbali. Swala la uuaji wa waandishi, utekaji na utesaji si la kuandikiwa makala tu, ni swala la hatua zaidi ya hiyo
 
wewe unaishi dunia ipi? siku hizi chama kinachopanga na kuteka watu aliwemo kibanda kinajulikana. soma kunathread inajadilia hapa tangu juzi au nenda kwenye u tube utaikuta.

.
Rama Ighondu amekamatwa?
.
 
hakuna waandishi wa habari makini hapa bongo,wanalalia kwa kibanda kwa sababu ndo mwenyekiti wao,yule aliyegongwa na gari moshi akifichua biashara za magendo mpakani mbona hata story moja hatukuziona?,wanafiki wakubwa hao,wasipoungana na kukemea kila kinachompata mwandishi yoyote bila kujali sura,watakwisha
 
.
Rama Ighondu amekamatwa?
.
hebu basi nidokeze kidogo kuwa ni nani anayefuata baada ya huyu, nitaficha siri. ila nawasikitikia kuwa muda si mrefu mtakuja jua madhara ya haya myafanyayo, mungu yu pamoja na wafanyao mema,
 
Walimdhihaki Kubenea wakambeza wala hawakumpa ushirikiano alipo simami na kuufia ukweli wa alichokiamini,leo wamejionea!!basi tusemeje?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
hakuna waandishi wa habari makini hapa bongo,wanalalia kwa kibanda kwa sababu ndo mwenyekiti wao,yule aliyegongwa na gari moshi akifichua biashara za magendo mpakani mbona hata story moja hatukuziona?,wanafiki wakubwa hao,wasipoungana na kukemea kila kinachompata mwandishi yoyote bila kujali sura,watakwisha

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba hawa waandishi wa habari watakwisha kwa sababu hawana umoja,ni wanafiki sana unakuta wachache wenye misimamo kama akina Kubenea,Tegambwage,na kibanda pia marehemi Mwangosi wanaokuwa tayari kukataa kitu,lakini waliobaki wote wanaendekeza njaa kuombaomba kwa wenye fedha ndio kazi wanayojua na kupokea bahasha ili wafiche ukweli,na kununuliwa pombe kutawamaliza,simameni imara mteteane kuonyesha mshikamano wenu kwanza mngesusa hata kutoa au kuandika habari za serikali kwa wiki moka au mbili ili waone athari ya kutokuwathamini waandishi wa habari lakini NJAA jamani NJAA MBAYA mumefikia hata kusalitiana sababu ya pesa WATAWAMALIZA na hamtakuwa na sauti

Na ubovu wenu ni bahasha,pombe na kupelekwa sehemu za starehe mmekwish
 
Tatizo la hawa jamaa wametanguliza sana njaa na imewafanya wawe wanafiki kupindukia ukiwasikia kwenye radio na kusoma makala zao magazetini wakiwasifia magamba pale wanapokuwa wamevuta kabahasha unaona kichapo ni haki ya mnafiki
 
Natamani kuishi maisha ya Babu yangu ambaye hakukanyaga Darasani lakini aliishi maisha ya ufahari na kujiamini katika Taifa hili kuliko yangu na waadishi wa habari wa Tanzania.Hakika CCM wanakila sababu ya kujipongeza kwa kuua uwezo wa Watanzania kujitambua katika mambo muhimu ya haki zao za Kiraia.
 
hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho wa Tanzania ipo siku ukweli utajulikana na rais wetu msikivu Dr Jk atafikishwa the hague kujibu tuhuma zake,maana tanzania ya leo hakuna usalama wako wapi wauaji wa profesa mwakyusa.wako wapi waliomwagia Tindikali Kubenea,wako wapi waliompiga risasi mwandishi wa Tanzania DAIMA,wako wapi waliowakata mapanga wabunge wa mwanza,KIWIHA NA MACHEMLI.wako wapi walio vuruga kampeni za ubunge SHIBUDA anahutubia mpaka mtu1 akakatwa kichwa,yote yana mwisho rais msikivu mr maendeleo DR JK
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom