Aibu kwa CCM...


Kila kiongozi, mwanachama, mpenzi wa cdm wanamlalamikia Nape, huyu jamaa kweli yaonekana mmeshindwa kumdhibiti

 
Ccm kwisha kabisa! Wanabeba watu kila kona na kuwahonga ili waende kwenye mkutano wa leo jangwani. Hii ni aibu kubwa sana, hata mikutano ya kawaida tu wananunua watu! Hapa mwenge stand kuna coaster tatu, wahuni wa stend wamepewa bia na viroba ili wapelekwe jangwani kushangilia na kupiga makofi! Kwa kweli nape na nyinyiem yake hawana jipya zaidi ya kutumia pesa zetu ndivyo sivyo! Watanzania tuamke hali hii inatisha!
 
Hivi sheria za usalama barabarani huwa haziwahusu hawa wenye nguo za kijani na njano?.

Hili swala la selective justice ndo limeharibu nchi.
Ajabu sana kukuta askari ndo wapo bize kuyaongoza haya mafuso.
Ikitokea ajali tutasema kazi ya Mungu.

Tatizo ni lilelile, nalo ni uchakachuaji wa asasi za serikali na kuzigeuza vijiwe vya makada wa CCM. Ama kweli CCM kweli sasa ni maji ya shingo, wanategemea nguvu ya fedha za kifisadi ku survive. Hebu ona mwenyewe hapa; hao wote ni buku mbili mbili, chupa moja moja ya maji na pilau mbele ya safari! Ama kweli wahenga walisema hakuna refu lisilo na kilele! Wananchi wanawakimbia mwisho atabaki Nape na familia yake. Maana amesema wajapohama wote CCM yeye atabaki pekee na CCM itabaki imara kabisa (Jeshi la mtu mmoja?)
 
Nape,eti ulipata kura 10?
 
Ndio mkubali kwamba MAGAMBA yako juu ya sheria. Wamevunja Sheria ya Usalama barabarani kwa kubeba watu kwenye malori na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa! Maskini Mama yangu Tanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…