Aibu Kuu Uhamiaji: Uchakachuaji wa matokeo ya usaili wa nafasi za koplo na konstebo

Kurithishana ni mojawapo ya sera (zisizoandikwa) za CCM!
 
Bornagain,
Hizi taarifa haziko sahihi na mwisho wake ni watu kuchanganyikiwa.#

Uhamiaji kulikuwa na makundi matatu ya kazi ambayo ni:
1. Waliomaliza vyuo vikuu ambao waliomba nafasi za kuwa Wakaguzi wasaidizi.
2. Waliomaliza form six ambao waliomba nafasi za kuwa Konstebo wa Uhamiaji
3. Waliomaliza form four ambao waliomba nafasi za kuwa koplo wa Uhamiaji

1. Kundi namba moja ndilo hilo liliwekwa uwanja wa taifa wakiwania nafasi 70. Usaili wake uliendeshwa na wizara yenyewe ya mambo ya ndani na majina ya waliochaguliwa ni haya hapa:
http://www.immigration.go.tz/news.pdf

2. Kundi la pili la hao form six wao usaili wao uliendeshwa na idara ya uhamiaji yenyewe na nasikia walioomba hawakuwa wengi sana. Nafasi zilikuwa 100 na waliochaguliwa wako hapa:
http://www.immigration.go.tz/downloads/Tangazo-.pdf

3. Kundi la mwisho ni la form four ambao nao usaili wake uliendeshwa na Uhamiaji na nafasi zilikuwa 100. Waliochaguliwa hawa hapa:
http://www.immigration.go.tz/downloads/Tangazo-.pdf

Wakati watu waliwekeza nguvu zote kwenye nafasi zile za uwanja wa taifa, idara ya Uhamiaji ilikuwa na nafasi zingine 200 za walalahoi. Pamoja na kutangazwa, hili kundi halikuchamgamkiwa sana kama lile la wahitimu vyuo vikuu. Hili kundi la vijana 200 ndio kuna majina kama 30 ambayo inaonekana yana uhusiano wa aina moja ama nyingine na baadhi ya wafanyakazi wa idara ya Uhamiaji.

Taarifa zikiwa sahihi ni rahisi kujadili hii habari. Je vijana wetu wangapi wenye sifa waliomba hizi nafasi za watu 200 na wakakosa? Unajua siku hizi kila mtu anakimbilia vyuo vikuu na baadhi ya nafasi za form four na form six wanaojua ni wale wenye uhusiano wa aina fulani na nafasi hizo. Vijana wengine wanafikiria kwenda vyuo vikuu tu na wakimaliza huko wanakosa ajira.


Acha hizo bwana wewe, nafasi zipo 70 walioomba walikuwa elfu kumi na kitu mpaka wakakalishwa uwanja wa taifa.Sasa kati ya hao unaniambia kutoka moyoni kuwa 30 ya watahiniwa ambao wametajwa kuwa wenye ndugu Uhamiaji ndiyo walikuwa vizuri then 40 wao wakatoka nje ya kufahamiana na watu wa Uhamiaji.There is problem in our system and it is big problem.Wewe kwa kuwa upo kwenye system na ndugu yako amepata basi povu linakutoka.Ipo siku mambo yatabadilika na yakishabadilika you will know what am talking lakini kwa sasa hata huwezinielewa.Just enjoy your days
 
Bornagain,
Hizi taarifa haziko sahihi na mwisho wake ni watu kuchanganyikiwa.#

Uhamiaji kulikuwa na makundi matatu ya kazi ambayo ni:
1. Waliomaliza vyuo vikuu ambao waliomba nafasi za kuwa Wakaguzi wasaidizi.
2. Waliomaliza form six ambao waliomba nafasi za kuwa Konstebo wa Uhamiaji
3. Waliomaliza form four ambao waliomba nafasi za kuwa koplo wa Uhamiaji

. Kundi namba moja ndilo hilo liliwekwa uwanja wa taifa wakiwania nafasi 70. Usaili wake uliendeshwa na wizara yenyewe ya mambo ya ndani na majina ya waliochaguliwa ni haya hapa:
http://www.immigration.go.tz/news.pdf

2. Kundi la pili la hao form six wao usaili wao uliendeshwa na idara ya uhamiaji yenyewe na nasikia walioomba hawakuwa wengi sana. Nafasi zilikuwa 100 na waliochaguliwa wako hapa:
http://www.immigration.go.tz/downloads/Tangazo-.pdf

3. Kundi la mwisho ni la form four ambao nao usaili wake uliendeshwa na Uhamiaji na nafasi zilikuwa 100. Waliochaguliwa hawa hapa:
http://www.immigration.go.tz/downloads/Tangazo-.pdf

Wakati watu waliwekeza nguvu zote kwenye nafasi zile za uwanja wa taifa, idara ya Uhamiaji ilikuwa na nafasi zingine 200 za walalahoi. Pamoja na kutangazwa, hili kundi halikuchamgamkiwa sana kama lile la wahitimu vyuo vikuu. Hili kundi la vijana 200 ndio kuna majina kama 30 ambayo inaonekana yana uhusiano wa aina moja ama nyingine na baadhi ya wafanyakazi wa idara ya Uhamiaji.

Taarifa zikiwa sahihi ni rahisi kujadili hii habari. Je vijana wetu wangapi wenye sifa waliomba hizi nafasi za watu 200 na wakakosa? Unajua siku hizi kila mtu anakimbilia vyuo vikuu na baadhi ya nafasi za form four na form six wanaojua ni wale wenye uhusiano wa aina fulani na nafasi hizo. Vijana wengine wanafikiria kwenda vyuo vikuu tu.

Niliomba nina sifa na nimekosa.
 
Hamjaelewa maisha yalivyo ndugu zangu..yan ipo ivi ukiwa hauna kitu au umekosa unakuwa wa kwanza kupiga kelele..sasa ukishapata unaungana na waliofanikiwa kuwapinga wale wasichonacho....unaongea na watu walichonacho eti tulete mabadiliko nchini wakati wao wameshiba..wazir,wabunge,na hao wakuu wa taasisi wameshiba..sasa sisi huku ndo kelele nyingi mana tuna njaa..tukipewa vitengo kimyaa..kama ishu zimegoma tafuta ishu nyingine..haya ukifatilia vizur utakuta wengine pale ndani ni watoto/ndugu wa mawaazir au wabunge na hao wakuu wa takukuru mnaowategemea wawasaidie..NARUDIA KUSEMA HII NI SERIKALI MOJA..KESI YA NYANI HUWEZI KUMPA NGEDERE ASULUHISHE..ATAKWAMBIA NISUBIRI NIKAANGALIE NYANI AMEKULA MAHINDI KIASI GANI KUMBE ANAENDA KUMALIZIA
 
Je tangazo hili hapa chini lina uhusiano gani na hiyo habari ya gazeti la Tanzania Daima?

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
TANGAZO
KUITWA KWENYE AJIRA
NAFASI YA MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI (ASSISTANT INSPECTOR OF IMMIGRATION)
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, anawatangazia wafuatao waliofaulu usaili wa
kujaza nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji (Assistant Inspector of Immigration) wanatakiwa
kuripoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Mtaa wa Loliondo Kurasini, Dar es Salaam tarehe
29 Julai 2014, saa 2:00 asubuhi.
Aidha, wahusika wote wanaelekezwa kufika kwa wakati wakiwa na vyeti halisi vya masomo na vya
kuzaliwa.
1 Abel Md. Maganya
2 Absolum Stafford Bashigwa
3 Agnes P. Mlay
4 Ali Musa Abdallah
5 Angela Kagaruki
6 Antony J. Nyagilo
7 Asteria Kiyanga
8 Awadhi Issa
9 Aziza Kaku
10 Bakari M. Khamis
11 Baraka Estomihi
12 Beatrice K. John
13 Bernard K. Mwampashe
14 Binasra J. Sabri
15 Charles M. Swai
16 Cosmas J. Mbuguni
17 Dativa J. Ndyetabura
18 David Muna
19 Doroth Ngai
20 Dotto Tabu
21 Emmanuel Gelison
22 Ezekiel A. Kibona
23 Fahamu Saidi
24 Farida Sued
25 Felix Mkemwa
26 Forget N. Charles
27 Frida N.Masomhe
28 Gabriel M. Kamugisha
29 Gath E. Nyansambo
30 Gerald Moses
31 Gideon Kihoko
32 Godson Mwanawima
33 Grace C. Nyarata
34 Hamza Sanga
35 Hassan A. Mziray
36 Ibrahim Ally
37 Idd Mgoi
38 Joachim Joseph
39 John G. Mgayambasa
40 Joseph Gregory
41 Kennedy John
42 Khamis Moh'd Khamis
43 Kombo M. Ame
44 Kwame Charles
45 Lawi E. Kumburu
46 Mabrouk H. Thabit
47 Mangunda A. Kaporo
48 Marco Zacharia
49 Maria Agapith
50 Mateso Msigala
51 Meshack Mwaisela
52 Michael John
53 Miriam Mwakamele
54 Mlalama Fortinatus Amlima
55 Mussa Hemedi
56 Mwita Mwikwabe
57 Neema R. Mrope
58 Nyangoma Martin
59 Oscar Philip
60 Pasaka Wilson
61 Pastory Packshard Mkongwa
62 Reagan H. Kawa
63 Rose Nseka
64 Senga Ally
65 Silvia Ngasoma
66 Sixtus Stephano Burashahu
67 Steven L. Kweka
68 Wendy Y. Mwalukasa
69 Witness Lwambo
70 Zulu P. Charles
Aidha, ni muhimu kufahamu kuwa uchaguzi wa walioitwa kwenye ajira umezingatia yafuatayo:
-Vipaumbele vya Idara ya Uhamiaji;
-Kutoa nafasi kwa waombaji kutoka Zanzibar;
-Ufaulu kuanzia alama 50 asilimia na kuendelea;
-Jinsia
Wasailiwa ambao majina yao hayamo kwenye orodha hii wafahamu kuwa hawakufanikiwa.
Atakayesoma tangazo hili amjulishe na mwenzake.
Tangazo hili limetolewa na:
Katibu Mkuu

Halina. Hujaelewa.
 
Lkn huoni kuwa Huyo mkurugenzi wa Uhamiaji km kapendelea na kuwapa watu wadhifa wasiostahili basi Kapendelea WAGALATIA wengi kuliko WAISLAMU?

Na Kawaida ya nyie wagalatia ni kuwa Mnafurahi sana pale mnapoona kuwa nafasi nyeti nyingi au zote zinachukuliwa na Wagalatia regardless ya kuwa wana Elimu au Hawana!
Au sio hivyo?

off point
 
Mkuu,
Uliomba nafasi gani? Wakati mwingine watu tunakuwa waoga sana kwa kuhofia upendeleo na mwisho wake hatuombi hizo nafasi.

Any way kama uliomba pole sana. Ila endelea kutafuta maanakukosa kazi moja kusikufanye ukaamini kazi zote zinatolewa kwa upendeleo maana ukiamini hivyo kweli utaendelea kukosa.

Niliomba nina sifa na nimekosa.
 
Wabongo wachonganishi sana.
Mbona haya majina hayafanani na yakwenye magazeti?

Wewe ndo mchonganishi. Umeangalia majina ya walioitwa kazini nafasi za Corporal na Constable?
 
Mkuu,
Uliomba nafasi gani? Wakati mwingine watu tunakuwa waoga sana kwa kuhofia upendeleo na mwisho wake hatuombi hizo nafasi.

Any way kama uliomba pole sana. Ila endelea kutafuta maanakukosa kazi moja kusikufanye ukaamini kazi zote zinatolewa kwa upendeleo maana ukiamini hivyo kweli utaendelea kukosa.

umesha'prove kwamba huu ni uongo?
 
Wana JF,
Lengo la habari kama hizi ni kuchonganisha na kuchafua. Sitashangaa kuona hii habari haina ukweli kabisa.

Binafsi niseme wazi namfahamu vizuri sana kamishna mkuu wa Uhamiaji na nimewahi kuongea naye juu ya suala hili la ajira za Uhamiaji.

Ukweli ni kwamba kwenye ajira za graduates, idara ya Uhamiaji haikuhusika. Zoezi zima limesimamiwa na wizara mama ya Mambo ya ndani. Wao Uhamiaji walisema waletewe majina tu tayari Kwa kuwapokea vijana na kuwapeleka mafunzo.

Wao Uhamiaji walisimamia zoezi la ajira za waliomaliza form four na form six.

Najua TZ ya leo ajira ni tatizo na wakubwa wanapenda watoto wao waende Uhamiaji. Lakini nina wasiwasi na ukweli wa habari.

Kamishna mwenyewe mara kadhaa amewahi kusema juu ya pressure ya wakubwa wakiwemo mawaziri kutaka watoto wao waingie Uhamiaji na majibu anayowapa.

Kama kungelikuwa na upendeleo kiasi hicho basi hao vijana wa mawaziri na makatibu wakuu wangejazana hapo.

Pressure nyingine ni ya ndugu na hata watu toka Kyela ambao wanajua Ambokile anatoka huko. Pia nao anajua namna ya kuwajibu na ukiangalia majina hayo sioni uhusiano wowote na Ambokile wala kule anakotoka.

Sasa kweli mtu wa namna hiyo ataruhusu maafisa wake wajaze watu wao huku yeye mwenyewe kawakatalia ndugu zake na maboss wake? Wangejazana akina Mwa hapo naona mungesema sana. Ambokile yuko fair sana. Msianze kumchafua Kwa mambo ya kupikwa.

Majina yetu yanafanana sana. Watu wasio ndugu wala kufahamiana wanaweza kuwa na majina yanayofanana.

Any way mimi nimemplekea huu ujumbe kama alikuwa bado hajaupata.

Hivi kwa ushahidi ulioletwa humu bado unapinga, eti majina yanafanana my ass...
 
Mkuu Remote,
Endelea kuamini unachoamini. Ukweli ndio huo. Ukiamini upendeleo kila siku kweli utaendelea kuamini hivyo mpaka kufa. Kama hao 30 wamependelewa katika 270 na hao 240 wamepatikana kwa njia zipi?
Hivi kwa ushahidi ulioletwa humu bado unapinga, eti majina yanafanana my ass...
 
Hivi watoto hao kama wana sifa hawaruhusiwa kuomba nafasi hiyo kwa sababu Baba, Mama, shangazi, Mjomba anafanya kazi au ni mtumishi wa Idara ya Uhamiaji??????????????????????

Kuna wakati mnatakiwa kuwa na akili za kwenu si za kushikiwa.....

Ni kweli ndugu wa wafanyakazi wanaruhusiwa, lakini NOT TO THAT EXTEND YA UHAMIAJI...
 
Kwa wale wenye majina mengine kutoka idara mbali mbali watupie humu.., yaani unaweka surname ya alieajiriwa na yule ndugu aliefanikisha kupata ajira.., hii operesheni ni muhimu sana.., naskia BOT yalishatupiwa humu..!
 
Back
Top Bottom