Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,764
Yaani nilikuwa naangalia kipindi cha mapishi mida mchache uliopita ,wakionyesha sijui wanaita Bif diana ,sasa kubwa ambalo niliona aibu wakati nikiwa na wageni zangu kutoka Ulaya tukiangalia ,aibu yenyewe ni jamaa ambae akiitwa akijijulisha kwa jina la Shefu Asha akisaga nyama ,aloo sauti iliyokuwa ikitokeza wakati akiigonga hiyo nyama utadhani wapo gereji ya magari ,ukiangalia kipande cha nyama akifiki ata robo kilo ,haya weka mbali kubwa ambalo ndio hapo niliona aibu ya aina yake ni kikaangio ,aloo kimechoka na hakina mkono, Nikawaza na kujisemea hawa watu wanafikiri hii Tv wanatazama peke yao,hivi hawaoni kama hizi Tv za hapa nchini zinatuwakilisha na wengine huwa tunajilabu ,yaani kwa hili la leo nimeona aibu kubwa sana na jamaa walitucheka,aloo kikaangio hakina mkono nafikiri mhusika na mtayarishaji inabidi wapewe onyo. Hebu waangalie vipindi vya nchi jirani waone ,vyombo vyao ni vipya kabisa ,yaani ni spesho kwa kuonyeshwa kwenye TV ,sasa hapa ITV mnaonyesha matangazo kienyeji .Nie vipi ?