Aibu! Benki ya Dunia yaishauri Serikali kupunguza matumizi na kuweka vipaumbele!

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Jana; Taarifa ya Habari Radio One saa 2 na saa 4 usiku, Radio 1 walitoa Habari WB imeishauri Serikali ya Tz kubana matumizi na kuweka vipaumbele.
Ukweli ni kwamba nilijisikia aibu sana kwamba hadi wafadhili wetu, wanaotudai mamilioni ya dola (ingawa kihalisia wao wangefanya biashara kwa kuzidi kutukopesha) wanaiona Serikali yetu imejaa ubadhirifu kwa matumizi makubwa yasiyo ya lazima na kushindwa kuweka na kuzingatia vipau mbele.
Kama tungekuwa na viongozi wenye haya, ushauri huo wa WB ni udhalilishaji.
 
Kwanza Rais anaongoza nchi zaidi ya moja (Tanzania na nchi za nje), maana ndani ya miaka sita ya uongozi wake amesafiri miaka mitatu, atapunguza matumizi wapi kwenye safari au?
 
Wameamua kumfikishia ujumbe kiaina.
 
Jana; Taarifa ya Habari Radio One saa 2 na saa 4 usiku, Radio 1 walitoa Habari WB imeishauri Serikali ya Tz kubana matumizi na kuweka vipaumbele.
Ukweli ni kwamba nilijisikia aibu sana kwamba hadi wafadhili wetu, wanaotudai mamilioni ya dola (ingawa kihalisia wao wangefanya biashara kwa kuzidi kutukopesha) wanaiona Serikali yetu imejaa ubadhirifu kwa matumizi makubwa yasiyo ya lazima na kushindwa kuweka na kuzingatia vipau mbele.
Kama tungekuwa na viongozi wenye haya, ushauri huo wa WB ni udhalilishaji.

Benki kuu inashauri dunia nzima,nazani umezoea kusikiliza radio za bongo tu,wb hiyo ndo kazi yao na siyo lazima nchi inayoshauriwa ifanye yote wanayo taka wao.
 
Inakua vipi Benki Kuu ya Dunia idese mawazo yaliojadiliwa humu JF kiundani zaidi mnamo 2011 na kutumia mawazo hayo hayo kuishauri serikali hii ya CCM yenye sikio zito sana na huku sisi hapa serikali hii hii ikawa imegoma kutusikiliza tangu hapo mwaka jana???????????
 
Kwa nini wameshauri badala ya kuikemea serikali? Au wamepewa tani ya dhahabu?
 
Inakua vipi Benki Kuu ya Dunia idese mawazo yaliojadiliwa humu JF kiundani zaidi mnamo 2011 na kutumia mawazo hayo hayo kuishauri serikali hii ya CCM yenye sikio zito sana na huku sisi hapa serikali hii hii ikawa imegoma kutusikiliza tangu hapo mwaka jana???????????
WB wanashauri upunguze matumizi lakini wanatoa conditions zikiwemo huko kubana matumizi kusiadhiri ajira na kukua uchumi! Hapa Tz utasikia hawaajiri na uchumi unaporomoka! Badala ya kuondoa posho za kijinga na kununua magari ya kifahari kwa wakubwa wote hadi mawilayani!
 
Jana; Taarifa ya Habari Radio One saa 2 na saa 4 usiku, Radio 1 walitoa Habari WB imeishauri Serikali ya Tz kubana matumizi na kuweka vipaumbele.
Ukweli ni kwamba nilijisikia aibu sana kwamba hadi wafadhili wetu, wanaotudai mamilioni ya dola (ingawa kihalisia wao wangefanya biashara kwa kuzidi kutukopesha) wanaiona Serikali yetu imejaa ubadhirifu kwa matumizi makubwa yasiyo ya lazima na kushindwa kuweka na kuzingatia vipau mbele.
Kama tungekuwa na viongozi wenye haya, ushauri huo wa WB ni udhalilishaji.

mkuu acha waseme labda serikali yetu itaamuka kidogo.
 
ukisoma habari ya world bank inatoa ushauri kwa nchi zote duniani, napata tabu kuelewa kuwa mleta hii thread ameiandika kuonesha kuwa ni Tz tu peke yake kwa makusudi au kwa kutokuelewa.
 
Kwa wanao tetea serikali hivi wanafikiri hata england wanapwewa wazo hilohilo la priorities? Kwa nini iwe tz tuu?
 
ukisoma habari ya world bank inatoa ushauri kwa nchi zote duniani, napata tabu kuelewa kuwa mleta hii thread ameiandika kuonesha kuwa ni Tz tu peke yake kwa makusudi au kwa kutokuelewa.
Botswana wana jeuri ya kukataa ushauri wa WB. Wana manage mambo yao vizuri tu. Sisi je?
 
Benki kuu inashauri dunia nzima,nazani umezoea kusikiliza radio za bongo tu,wb hiyo ndo kazi yao na siyo lazima nchi inayoshauriwa ifanye yote wanayo taka wao.

* Wewe umezoea kuskiliza redio za wapi?,sisi za bongo,wewe za masaburi?.
* Na je kama sio lazima kufuata ushauri wao WB,kikwete huwa anafuata nini huko ulaya na Amerika?, kama sio ushauri wa hao anaowaita wakubwa,
*Je kwa nini serikali huwa inafurahia mikopo yao na kuziiweka kwenye headline za magazeti na tv zote nchini habari za mikopo yao kwetu.?

Haya amka hujachelewa bado asubuhi,
 
Back
Top Bottom