Aiba Mguu wa Maiti toka Kaburini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aiba Mguu wa Maiti toka Kaburini

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, May 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Daniel Wayne Staley
  Kijana mmoja wa Kimarekani ametiwa mbaroni na polisi baada ya kuiba mguu wa maiti ya msichana wa kiyahudi toka kwenye makaburi ya wayahudi nchini Marekani. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 aliyetambulika kwa jina la Daniel Wayne Staley, alitiwa mbaroni ijumaa alfajiri akiwa ameubeba mguu wa binadamu aliouiba toka kwenye makaburi ya wayahudi mjini Dallas.

  Polisi waliwasili kwenye eneo la tukio majira ya saa tisa na nusu usiku baada ya kupewa taarifa na mtu aliyeshuhudia tukio hilo.

  Daniel alikamatwa akiwa amebeba mfuko wa rambo ambao ndani yake kulikuwa na mguu wa binadamu.

  "Nilifukua kaburi na kuuchukua mguu wa maiti ya msichana ya kiyahudi kwakuwa nilikuwa nikitaka mguu", Daniel aliwaambia polisi.

  Daniel amefunguliwa mashtaka ya wizi wa maiti ya binadamu na huenda akatupwa jela mwaka mmoja na kupigwa faini ya dola 4,000, limeripoti gazeti la The Dallas Morning News.

  Daniel hakusema mguu huo alikuwa akiuhitaji kwa shuguli zipi. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=4460430&&Cat=2
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hatari!
   
 3. s

  sammie Member

  #3
  May 12, 2010
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ana wazimu nini?
   
 4. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Oh! Mungu amrehemu jamani NI MAPEPO HAYO!
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Asije kuwa mmarekani mwenye asili ya kipalestina
   
Loading...