Ahsante sana rafiki yangu wa mtandaoni

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
"Ahsante sana RAFIKI YANGU wa mtandaoni."

Hii ni special kwako wewe rafiki yangu wa mtandaoni. Rafiki yangu ambae mitandao ya kijamii imetufanya tuwe karibu zaidi kama watu tuliopitia historia moja ya maisha.

Tangeni, Mzumbe - Morogoro ndipo nilipozaliwa na kusoma shule ya msingi kabla ya kuhamia mjini. Lakini wewe umekuwa ukisoma post zangu, kukoment na kulike ukiwa huko ulipo kijijini, mjini au hata nje ya Tanzania. Ahsante sana rafiki.

Ahsante wewe rafiki yangu ambaye kupitia mitandao ya kijamii tumejenga urafiki wa kweli, kubadirishana mawasiliano kisha kuwasiliana na kujuliana hali mala kwa mala.
Ubarikiwe sana rafiki.

Ahsante wewe rafiki yangu ambaye mitandao ya kijamii imewezesha hadi tukaonana na kuwa familia. Hata wewe ambaye hatujawahi kuonana nafarijika kuona unaniamini na unapendezwa na ninachokifanya.

Ahsante wewe rafiki yangu ambaye, umewahi kuniomba ushauri tukashauriana na kutatua changamoto. Uniwie radhi kama ushauri wangu haukuweza kufikia lengo ulilotarajia lakini naamini kuna kitu utakuwa umekiongeza kwenye maisha yako. Nami pia nimeweza kujifunza kupitia wewe. Ahsante sana rafiki.

Ahsante wewe rafiki yangu ambaye umeilinda heshima yangu, hukupanga kunichafua hata pale tulipokoseana bado tulisameheana na kuendelea kuishi kwa amani na upendo. Wewe ni mtu muhimu sana kwangu.

Ahsante wewe rafiki yangu ambaye unaitumia vizuri hii mitandao ya kijamii na hauitumii kujidharirisha au kudharirisha wengine. Wewe ni mtu smart hivyo nikuombe uendelee hivyohivyo usije kubadirika na kupoteza utu wako au kushusha utu wa watu wengine. Watumiaji wa mitandao ya kijamii sisi ni familia moja.

Kila mmoja huku katika mitandao ya kijamii anaweza kujifunza na kufundisha wengine au kuburudika na kuburidisha wengine lakini hili linawekana endapo tutaendelea kuzingatia sheria, maadili na utamaduni wa nchi yetu pendwa Tanzania. Hakika wewe ni rafiki wa mfano.

Mimi ni mtu ambaye hobby yangu kubwa ni sanaa. Napenda sana kuandika. Huku mitandaoni nimerusha makala nyingi sana za mada mbalimbali kama vile simulizi, mada za kisheria na mafunzo mbalimbali. Hivyo, uniwie radhi kama nimewahi kukukwaza kwa namna moja au nyingine kupitia maandishi yangu.

Ahsante wewe rafiki yangu ambaye umeweza kuvumilia madhaifu yangu, hakuna binadamu aliye mkamilifu. Kikubwa ni kujua namna ya kuishi na watu kulingana na jinsi walivyo.

Kuna kipande fulani cha wimbo mmoja kinasema "furaha ni kuwa na marafiki, furaha ni kulewa na marafiki" nami najivunia kuwa na rafiki kama wewe unayesoma ujumbe huu.

Upendo na uzidi kutawala kati yetu na tuendelee kudumisha urafiki wetu wa thamani.

Tukiwa tungali tunaishi naamini kuwa tunaweza kufanya makubwa na mazuri kupitia urafiki wetu uliotukuka.

Nakupenda sana rafiki yangu. Mwenyezi Mungu akubariki na kunyoosha mapito yako. Nakuombea upate mafanikio makubwa sana katika maisha yako ili rafiki zako tuweze kujivunia uwepo wako katika maisha yetu.

Japo nina mengi ya kuendelea kuandika lakini kwa leo niishie hapa.

Share furaha kwa kuweka comment, like na kushare ujumbe huu kwa marafiki bila kuchoka.

Ni mimi rafiki yako mwaminifu, mwanasheria na mwalimu wa maisha.

A Lawyer and LifeCoach
Mr. George Francis
WhatsApp: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
Thank you very much.

Facebook Group:
KITABU CHA SIMULIZI ZA MAISHA | Facebook

Telegram Group la sheria: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓

Pia unaweza kujiunga na magroup yangu ya sheria ya WhatsApp.

You're most welcome.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom