Ahsante Mungu kwa kutupa Rais Magufuli

Ahsante Mungu kwa kutupa Rais Magufuli

Natamani ungeweka kichwa cha habari cha kuvutia watu wengi waingie wasome uzi huu. Kwa jinsi watu walivyo na hasira, na kichwa cha uzi wako wachache sana wataingia kuusoma ujumbe huu uliyojaa hekima na ushauri kedekede
Nadhani mods watanisaidia
 
Aiseee Great thinker bado wapo kumbe safi sana..Kuna watu hawazitaki tena akili zao wamekua na usahaulifu kuliko hata mbwa pitbull.. thumbs up
 
Natamani ungeweka kichwa cha habari cha kuvutia watu wengi waingie wasome uzi huu. Kwa jinsi watu walivyo na hasira, na kichwa cha uzi wako wachache sana wataingia kuusoma ujumbe huu uliyojaa hekima na ushauri kedekede
Ungechekewa ningeshauri ivoivo..
 
Nnesoma huu uzi nmekujikuta nafarijika sana!

Kuna wakati huwa najiuliza, watanzania wana akili za namna gani? Acha Magufuli atubadilishe kufikiri, kuongea pengine na hata kutembea kwetu.
 
Naungana nawe kwa dhati kabisa maana kiongozi wetu hana upendeleo ameshughulika na watu wote bila kujali chama kama ilivyodhaniwa mwanzo naamini kuwa ana akili timamu na hata swala la Paul makonda atakuwa amejiridhisha vya kutosha ndio maana bado yupo madarakani Bwana wetu amtie Nguvu daima wote tuseme Amina.
 
Kwan magufuli kafanya nn jaman.?
Tatizo la ukawa bhana ni kuwa wanaanzisha mada na kujijibu wenyewe na kujipa matumain wenyewe kwa wenyewe wakidhan ukipigia saut sikio la kushoto bas saut itatokea pia sikio la pili.

Magufuli yupo imara na tunamuamin na tutampa kura tena kama tulivyofanya 2015.
 
Kwan magufuli kafanya nn jaman.?
Tatizo la ukawa bhana ni kuwa wanaanzisha mada na kujijibu wenyewe na kujipa matumain wenyewe kwa wenyewe wakidhan ukipigia saut sikio la kushoto bas saut itatokea pia sikio la pili.

Magufuli yupo imara na tunamuamin na tutampa kura tena kama tulivyofanya 2015.
Usisome kwa mhemko hebu rudia tena kusoma
 
Wakuu habarini

Wakati ninamalizia kitabu changu pendwa cha purposefull driven life (Maisha yanayoongozwa na malengo) kilichoandikwa na Rick Warren, hasa nilivyofika kipande kinachoeleza, kila jambo linalotokea ni kusudi la Mungu, kumbe hata kujikwaa ni kusud la Mungu kukumbusha kitu fulani, nilijikuta natafakali kuhusu tanzania kwa upana wake na kutafakali kusudi la Mungu Juu ya tanzania, nilitafakari back ground ya nchi Yetu na mambo ambayo yalikuwa yanafanyika, nchini nimekuja kugundua kuwa Mungu anadhamira nzuri na nchi Yetu kwa kumleta Rais John Pombe Magufuli, unaweza kujiuliza kwa nn nimesema ivyo? Inamaana sioni mambo yanayotokea?

hapana naona na ninatambua, na ninaamini huu ni wakati wa mabadiliko kwa Tanzania kuanzia katiba na watu wenyewe watabadilika,

Huu ni wakati wa Watanzania kusimamia haki, kwenye malumbano ndipo haki inapopatikana, tuliona kipindi cha nyuma wabunge wa ccm walikuwa wazee wa ndioooo, hii ilipelekea hata katiba haikupita kwa sababu ya maslahi binafsi, wabunge walikuwa kwa ajili ya chama na maisha yao, leo hii wanapinga baadhi ya maamuzi ya serikali na pia naamini wanajutia maamuzi yao, katiba iliyopo inampa madaraka makubwa rais, mpaka anaonekana kama mungu mtu haya ni matokeo ya dhambi waliyoifanya watu wa ccm kipindi cha katiba mpya, hebu fikilia wakati ule katiba ingepitishwa na rais akapunguziwa baadhi ya madaraka na akaruhusiwa kushitakiwa je, haya yote yangetokea, me naamini na bado tutayaona Mengi sana tutaona jinsi watu wanavyotumia madaraka waliyopewa na hata kukataa kutoka madarakani

Magufuli ameletwa na Mungu ili kubadilisha fikra za watanzania, na fikra za wanaccm wenye akili timamu siyo kila kitu useme ndioo, hamna mtu anajua kesho yake, nani alitarajia kuwa nape atakuwa na msimamo kiasi hiki, nape yule wa kipindi cha kampeni ndiyo huyu kweli? (hili swali najiuliza) je, makonda yule aliyempiga warioba na kumfunga viatu rizyone ndiyo huyu kweli??? Mmmh hapana

Tanzania mpya italetwa na watanzania wenyewe baada ya kugundua udhaifu wao siyo ccm wala chadema au chama chochote cha siasa, hebu fikilia leo hii angekuwa raisi kama maraisi waliopita tusingeona misimamo ya wanaccm, na pia wanaccm wasingefanya makubaliano na chama pinzani, ila kwa sababu tunarahisi mwenye maamuzi yake tunaona jinsi watu walivyo

Nimalizie kusema ya kwamba Tanzanua itajengwa kwa watanzania (wananchi) kwa kubadilisha fikra zao, kupata katiba mpya inayowabana viongozi wasiwe juu ya sheria
Bado Mungu anakusudi na Tanzania tuendelee kuvumilia
 
Ukiamini Mungu yupo sitashangaa usipoweza kuona ubaya wa Magufuli.
 
Back
Top Bottom