Ahsante Mungu kwa kutupa Rais Magufuli

mtarimbo

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
1,709
4,211
Kwanza kabisa ntampa saluti JPM kwa kufanikiwa kuziba mianya mingi ya ufujaji mkubwa na wa kihistoria wa mali za wananchi/umma uliokua unafanywa na viongozi ambao bila uzalendo na utu walitumia nafasi zao kufuja mali za wananchi.

Pili nampa saluti kwa juhudi anazofanya kwa kukubali kufuata ushauri wa wanauchumi wetu ju ya kupunguza pengo kubwa la wenye nazo na wasio nacho, mpaka hivi sasa wale waliozoea kufanya shopping supermarket tunapigana vikumbo Buguruni hii itawnufaisha wakulima wetu wenye uchumi duni pia kwa mama ntilie huko ndo usiseme tunapigana vikumbo si utani hii inawapa ahueni ya maisha, ukiangalia maeneo ya afya kwa sasa upatikanaji wa dawa kwa unafuu unazid kupaa kwa kipind kifupi famasi 7 tayari zinafanya kazi kule dawa ya 200 madukani wanauza 1500 ,mpaka 2020 tutakua na famasi kila wilaya.

Tatu na mwisho nampa saluti kwa hatua aliyochukua kuondoa mtandao wa kiutawala ambao ulikua umejengwa ndani ya nchi kwa nia ya kulindana pasipo kuangalia maslahi ya umma alilofanya ni mapinduzi ambayo

Kwa nchi nyingine yanafanyika kwa mtutu ni ujasiri wa hali ya juu napenda sana kuwakumbuka maraisi katika sala ila kwa huyu nilifunga siku 3 nikimshukuru mola ampe ulinzi kwani aliyofanya ni dhahiri ana maadui hatari(deadly) ambao kufanya chochote si kitu kwao.

Rais wa wanyonge amepatikana
 
Wasiompenda Magufuli wajinyonge. Jana nilikuwa kwenye daladala nikitoka uwanja wa Taifa kuangalia mpira kati ya Yanga na Medeama. Kwenye hilo basi uliibuka mjadala hasa baada ya Mashabiki wa Simba kuwashangilia Medeama kwa nguvu zao zote bioa kuvaa jezi za timu hiyo tofauti na walivyofanya kwa TP Mazembe. Sababu kubwa ya mashabiki wa Simba kutovaa jezi za Medeama ni kwa vile zinafanana na za mahasimu wao Yanga kwani jana walivaa jezi za Njano. Akaibuka jamaa mmoja alitoa bonge la comment. Akasema kwamba, mapenzi ya Mtu hayapo kwenye mavazi. Akasema mbona mimi ni shabiki wa Simba na CCM ila hata siku moja siwezi kuvaa jezi za kijani zinazovaliwa na Yanga na CCM. Akasema kuwa wapo wengi ndani ya UKAWA hawakumpigia kura Magufuli ila kwa sasa wanamuunga mkono na 2020 watampa kura kwa vingi. Hakika hili lilinipa funzo kubwa sana
 
Wasiompenda Magufuli wajinyonge. Jana nilikuwa kwenye daladala nikitoka uwanja wa Taifa kuangalia mpira kati ya Yanga na Medeama. Kwenye hilo basi uliibuka mjadala hasa baada ya Mashabiki wa Simba kuwashangilia Medeama kwa nguvu zao zote bioa kuvaa jezi za timu hiyo tofauti na walivyofanya kwa TP Mazembe. Sababu kubwa ya mashabiki wa Simba kutovaa jezi za Medeama ni kwa vile zinafanana na za mahasimu wao Yanga kwani jana walivaa jezi za Njano. Akaibuka jamaa mmoja alitoa bonge la comment. Akasema kwamba, mapenzi ya Mtu hayapo kwenye mavazi. Akasema mbona mimi ni shabiki wa Simba na CCM ila hata siku moja siwezi kuvaa jezi za kijani zinazovaliwa na Yanga na CCM. Akasema kuwa wapo wengi ndani ya UKAWA hawakumpigia kura Magufuli ila kwa sasa wanamuunga mkono na 2020 watampa kura kwa vingi. Hakika hili lilinipa funzo kubwa sana
Only crazy can vote for JPM again
 
Wanajamvi nimemaliza kuangalia marudio ya kipindi chaMagufuli ITV akiwa bandarini akiongea na wafanyakazi, nimemsikiliza kwa makini sana, pamoja na kazi nyingi nzito na za hatari ambazo amekwisha pambana nazo, nimefikia hatua yakumkubari sana huyu kiongozi.

Hakika ni mtu aliyetumwa na MUNGU. Nchi yetu tulikuwa tumefika pabaya mno, taratibu heshima inarejea.

Hakika tupo pamoja na ww kila hatua.Mungu azidi kukulinda nasi dua zetu zinakukinga na kila hira za wanafiki wako.
 
hahahahaaaaaaaaaaaaaaaa,mtupisheeeeeeeee!!!erick omondi akae chini kwanza.hahahaaaaa. CCMmmmm???mnatuchekesha bana yatosha.,!!!
 
Ukiikana roho ya chuki na roho ya kushikiwa akili au kutumika lazima umpongeze rais wetu kwa kazi anayoifanya mungu ampe maisha marefu kwakweli amejitoa 100% kuikomboa nchi yetu pamoja na wtz sasa hivi watu wanajua umuhimu wa kazi ,nidhamu ya pesa na uwajibikaji
You've have said it all.

 
Mtaani kwenu wananchi hawalii njaa?
Wananchi wanalia njaa miaka yote,Kuna watu hawataki kujishughulisha Kabisa wapo kila mtaa wa nchi Hii wataacha kulia njaa?,au we mmojawapo?,. USA inaitwa Land Of Opportunity ila ina omba omba zaidi ya mil 2 wanalala chini ya madaraja,Waweza ilaumu serikali yao?.. Fanyeni kazi na kuwa mbunifu kijana,zama zimebadilika sana.
 
Lo hiyo video clip inatisha mkuu meli 60 undocumented,flowmeter za mafuta zimezimwa kwa miaka zaidi ya 5,Scanner hazifanyi kazi zipo kama geresha.Dry containers za binafsi zilipewa kipaumbele kuliko yard za bandari.Pesa za kununua scanner mpya na flowmeter zipo lakini wameziba masikio licha ya Waziri mkuu kutoa agizo miezi 8 ya nyuma.TICS na mkataba ndani ya mkataba,vyeti fake vya viongozi wa juu bandarini.Raisi yupo sahihi japo itachukua muda.Na hiyo bandari ni mfano mmoja tu,sehemu nyingi za nchi ni labda ovyo kuliko hata bandari.Kawauliza swali mmoja wangekuwa wao kwa nafasi ya raisi wangefanyaje?
 
Wanaoiuwa nchi hii ni wasomi. Niliipenda hii statement sana.
 
Watu walikuwa wapiga dili aisee, pamoja na hela kuwa scarce resouce lkn ilifikia hatua kwa baadhi ya watu Bandarini nawapiga dili wengine hela ikawa cyo tatizo bali tatizo ikawa matumizi, mtu akifanya kazi bandarini miezi 6 tu huyo cyo mwenzako, na ilikuwa kupata kazi hapo kama hujatoa hongo angalau ya 5m cjui kama unaweza fikiriwa japo kwa interview! Hata mtaani mtu akisema anafanya kazi bandarini lazima umwogope! Watu wamekuwa mabilionea kwa miaka 2 ya wizi Bandarini. Tunakuomba sana JPM endelea kuwafyeka na kuwapeleka mojakwa moja mahakama ya wezi uliyoianzisha ikiwemo kufilisiwa mali zote za wizi. Tuko nyuma yako.
 
Back
Top Bottom