Ahsante mheshimiwa Zitto, lakini huyo ni mbuzi kwenye gunia!

@ Facebook: by William Malecela on Wednesday, June 15, 2011 at 10:57pm

@ NEW YORK CITY - USA: Ujira wa Wabunge wetu wanapokuwa bungeni kutuwakilisha wananchi, je ni mkubwa sana kuliko uwezo wetu Nationally, au ni just another political stunt aiming at gaining temporary political populism? I mean Mh. Zitto anahitaji heshima kwa kuibua hii debate, lakini at the same token ni haki yetu wananchi kuuliza maswali magumu on the ishu ili tusiishie kuuziana mbuzi kwenye magunia. Binafsi ninasema kwamba I am very troubled na this ishu of what exactly is the logic behind it on Mheshimiwa's side, kwa sababu toka isemwe nimejaribu kuangalia what is the long term to our National interest on it to no avail kabisa , WHY? Tanzania ndio kwanza tumetoka kwenye siasa za the Doomed Communism, we are still in the transition or work in progress towards Capitalism and then kabla hatujaenda mbaali sana recently kumekua na vilio vya kutaka kurudi kwenye Azimio La Arusha na the so called maadili ya uongozi, now here comes this which in the large picture ni kupunguziana ujira makazini. Hapa ndipo huwa ninauliza hivi: Hili taifa tulilogwa na nani?


- People, look here I don't care what, haya ni mambo ya kurudishana tulikotoka yaani kwenye maisha ya Usawa usawa nonsense ambayo ndio yamelifkisha hili taifa hapa tulipo! I mean kama kiongozi mmoja ameamua kwamba hela anazolipwa ni nyingi sana kwake hazihitaji tena, great azichukue na kupeleka kokote anakotaka, lakini trying to make a National policy out of it ni misguided thinking na the answer is NO! Wa-Tanzania tumetoka mbali sana na matatizo ya ujira makazini, taifa letu limepoteza wataalamu wakubwa sana waliobobea kwenye fani mbali mbali Duniani kwa sababu ya kuogopa kwao kufanya kazi Tanzania kisa cha ujira mdogo sana kulinganisha na ujuzi walionao ambao sisi as a Nation tuliuhitaji sana, ni only miaka ya karibuni ndio pole pole tumeanza kuwa na National progress on ujira infact mpaka sasa we can claim having a Middle Class, ambayo ni simply the results of ajira zenye ujira nafuu makazini. Sasa why now throw this Mheshimiwa Zitto's thing in the mix? I mean ukianza na posho za wabunge leo, kesho utaanza kuingilia Madakitari, sasa where would you draw the fine line na standards za ujira? Ndio maana ninasema kwamba the idea ni only temporary political populism stunt, lakini haina anything good on the long term and permannet National interest na itaishia kutukimbizia wananchi wataalamu as it has done in the past, ambao hili taifa tunawahitaji sana sasa kuliko wakati wowote mwingine toka tupate uhuru.


- Tulipoingia siasa za vyama vingi as a nation, tulikubaliana kimsingi kwamba Viongozi wetu wa taifa tuwalipe kulingana na hali halisi ya maisha, ili kuwaondoa kwenye tamaa za Rushwa, huenda Mheshimiwa hakuwepo wakati huo au alikuwa mdogo sana kiumri, lakini anapaswa kuelewa kwamba huo ujira uliwekwa kwa sababu za kimsingi sana zilizojali maisha ya Viongpozi wetu kama sisi wananchi wengine wote, ambao in the wake of ujira mdogo wakati tunalitumikia taifa inaweza kutupelekea kufanya maamuzi mengi against taifa kuelekezea kwenye matumbo yetu zaidi kwa sababu ya ujira mdogo sana kutoka kwenye taifa letu wenyewe tunalolitumikia usiku na mchana. Hakuna taifa Duniani lililopata maendeleo kwa haraka sana kwa kupounguza ujira wa Viongozi wake wa Taifa, na if the point ni political symbolism zaidi then wananchi wa chini twafwa, kwa sababu ni lazima upunguze ujira wa kila sekta katika taifa, huwezi kuishia kwenye Wabunge tu. Na the worst of all the idea inapanda mbegu za kuanza kuongozana kwa kutumia mob rule au mob justice in the process badala ya natural justice ambayo ni hatari sana kwa our future National political Stability, yaani hii ya kiongozi yoyote kukurupuka tu na misguided hojas bila hata kuki-consult chama chake cha siasa, wananchi tuzikatae siasa za namna hii kwenye taifa hatuzihitaji kabisaa, ndio maana tuna sheria ya vyama vya siasa.


:- Kwa hayo yote ninasema hivi Mh. Zitto hongera sana kwa uamuzi wako, lakini tafadhali sana uishie kwako tu, usituuzie hili taifa mbuzi kwenye gunia!- tunataka kwenda mbele sio kurudi nyuma tena tulikotoka, ukiweza pigania kuongezeka kwa ujira makazini lakini sio kupunguzwa kwa sababu at the heart ya hoja yako ni kusonga mbele kwa kurudi kinyume nyume which is impossible!


William Malecela @ New York City; US.

Bill,
With all due respect I will not concur with you on this.....maybe you are miles away....but we on the ground sifuri knows it all....
 
Watu wengi nimegundua kuwa wanaingia kichwa kichwa kwenye hii issue. Kwanza lazima wajue kuwa hii issue siyo ya zitto ila zitto amevalia njungu (Mungu akubariki). Hii issue imekuwa inaongelewa na donors miaka nenda miaka rudi na ni moja ya chanzo cha utendaji mbovu serikalini. CCM na wabunge wake na wale wwanaofaidika na huu unyama always watapenda hii issue iendelee kwa sababu ina wagawa wafanyakazi na kufanya watawalike kirahisi na hawa manjangili.

Issue wenyewe: Hizi posho haramu (sitting allowance) amabzo zitto anazivalia njunga ni posho ambayo mfanyakazi wa serikali analipwa kwa kutekeleza wajibu amabao pia analipwa mshahara kwa mfano. Procurement officer amabye kazi yake ni kuhakikisha kuwa kuna manunuzi yenye tija katika idara yake analipwa posho kwa kukaa kwenye eavaluation board. Huyu procurement officer muda wake anaolipwa mshahara ni saa moja na nusu asubuhi mpaka saa kumi jioni. evaluation board ina kaa saa nne mpaka saa nane mchana, ndani ya muda wake wa kazi anaolipwa mshahara lakini anapewa tena posho. Hii pratice ya serikali inaleta mazara makubwa sana kwa utendaji serikalini na nchi kama kawaida kwa mfano
  • Kuna tija gani kwa daktari kwenda kufanya operation kwa mgonjwa ambako hapati allowance yoyote wakati akitafuta workshop ya customer care analipwa allowance na anaweza kuhudhuria workshop hizo kwa mara 5 kwa 3 years sababu posho haramu
  • Hizi posho zimeweza kutumiwa na serikali kuweza kuwa retain technical staff. Lakini ni kwamba baada ya kuacha ujamaa( mpango wa shetani kuwadanganya watu) salaries siku hizi zinategemea soko na hizi allowance aziwatendei haki wafanyakazi wa nchi hii kwa kuwa ina fanya mishahara iwe chini sana kwa Tanzania. Ukiwa unafanya kazi katika shirika ambalo lina ofisi nchi za kenya na uganda, ni watanzania ndiyo watakao lipwa kidogo kwa kuwa salary marjetyetu imefunikwa na hizi posho.
  • Watanzania wachache wanaolipwa hizi posho mara kwa mara il waendelee kuwepo kwenye hii circle wamekuwa wakiwaabudu viongozi wao ili kuwepo kwenye hii ciecle. kumbuka kuwa si wafanyakazi wote ambao wanafaidikia na hizi posho.
  • mabosi wamekuwa wanatumia hizi posho kama rushwa kwa nyumba ndogo kwa sabubu ni bosi anayetoa ruhusa kwenda kuhudhuria hivi vikao na workshop.
 
Mkuu@NYC, USA, Lukuvi jana wakati anahojiwa na Gabriel Zakaria TBC alikiri mwenyewe kuwa concept ya posho ambayo Chadema wanaipigia kelele iko sahihi. Na yeye akasema wanachopinga ni kuwa Zitto ameipersonalize,kwamba hoja sio kaanzisha yeye ila imeanzishwa na serikali.
Msimamo wa serikali ni kupitia upya mfumo wa kulipana posho ili kuwe na tija serikalini. Na hii itaenda sambamba na mkakati wa serikali wa kupunguza matumizi yake.
Kwa hiyo Mkuu @NYC, USA kimantiki serikali imetambua kuna tatizo kwenye ishu za posho kwa hiyo hukuwa na ulazima wa kupinga.

Then Lukuvi is more foolish than we have ever been told......is it that Zitto is not a Tanzanian or what?......kwa nini wao serikali wasiiseme kabla yeye hajaisema?
 
- Mkuu heshima yako sana loong time, kama nimekusoma vizuri sana, una ishus mbili moja ni ya mabosi na power ya posho, pili ni kwamba posho iondolewe kote mapaka serikalini, hapo ndipo ninapopata tatizo, sasa ukiondoa hizo posho bungeni itabidi uondoe kwenye kila sekta za taifa, ambayo naiona kuwa ni National disaster, kuanzia politically mpaka economically, kwa sababu sasa unaondoa competition makazini na unawafukuza wataalamu wetu wazawa, wananchi wakikosa motisha ya kuyafanyia kazi mashirika yetu kama ilivyokuwa zamani, tutarudia kule kule tulikotoka yaani taifa la kwanza Duniani kuwa na Viwanda vya Sigara na Bia visivyoingiza faida!

William @ NYC, USA.

According to you mzee wa U.S ni kwamba hizi POSHO ziliwekwa ili kuwafanya watu watimize wajibu wao ipasavyo na hasa wataalam wetu wasifikirie kuikimbia nchi. Pia unaitetea POSHO kwamba ikiondolewa kwenye kila sekta ya taifa basi tunarudi tulikotoka kwenye zama za ujima.

Kwa tafsiri yangu wewe unatetea mfumo wa KIBEPARI na unataka kuifananisha Tanzania hii na nchi zilizoendelea kwamba mwenye nacho aongezewe mara dufu na asiyenacho hana nafasi yoyote kumiliki hata percent moja ya uchumi wa nchi yake. Alichokifanya Zitto ni uzalendo tu na bila uzalendo ndugu zangu itakuwa vigumu watanzania kusonga mbele as nation. leo hii tupo gizani sababu ya suala hili hili la uzalendo na hakuna nchi ambayo imepiga hatua bila kuwa na uzalendo.

Wewe unataka tuwaache watanzania wenzetu ambao wengi ni wakulima wa vijijini wapatao 73% na tusonge mbele na katabaka haka kadogo ka watu 27%. Umesahau Tanzania ilipotoka? kwa mawazo yako haya napata wasiwasi kama ukija kuwa kiongozi basi utatuteketeza wote.

Bado Zitto ana hoja nzito ambayo wewe na wenzako (CCM) bado hamjaweza kuipiku, chief wazo la Zitto ni la kitaifa na wala hakutaka kujipaisha kisiasa kwani hakuna mtanzania asiyemjua Zitto na ufanisi wake wa kazi na sisi wananchi wote tunamuunga mkono. Nakuomba uwaandike CCM uwashauri wawe wazalendo na wakubaliane na hili wazo, kama mishahara yao haiwatoshi mpaka watake na hizi posho je huyu mwalimu anayepata sitini elfu kwa mwezi yeye naye.

Hiyo dhambi ya umimi itatutafuna ndugu zangu, hii nchi ni yetu sote tugawane kilichopo kwa usawa na mtu tukimchagua basi atuongoze kwa haki. lets us all be proud to be born in TZ.

Wasalimie hapo nyu yoki mkuu, nimekutumia CV yangu na mimi naikimbia nchi shida zimezidi. lol

 
- Mkuu wangu una hoja nzito sana, lakini basically naona kama unaongeelea serikali kuwa na sound supervision na utakelezaji wa sheria zake, maana sheria za kuwabana hao unaowasema zipo, lakini hazifuatwi wala kusimamiwa sasa hali haliwezi kuwa kosa la viwango vya ajira unless kama siajkuelewa lakini otheriwse una hoja nzito sana mkuu!

William @ NYC, USA.

Mkuu nachokiongelea hapa ni kwamba "in the name of the POSHO" kuna hela nyingi sana za serikali zinapotea, inshort ni kaaina flani ka ufisadi halali ndani ya serikali. Sasa hili limezoeleka mpaka imekuwa mess kama nilivyosema mwanzo. Ni bora kama ni nyongeza ya mshahara iongezwe lakini sio haya mambo ya posho, posho everwhere, anywhere na anyhow.

Hawa wakuu wa serikali huwa sometimes wanajisahau hata wakialikwa sekta binafsi wanataka wapewe posho. In short hizi posho ndiyo zimefifisha ufanisi kuliko kuuongeza na any right minded proffesional hawezi kuvutiwa kwenda kufanya kazi serikalini eti kwa sababu ya posho ambayo ni subjective na bosi wako, idara, sometimes kujipendekeza kwako. Wakati sekta binafsi tunaongea unapoingia tunamalizana baada ya hapo kazi kwenda mbele.

Nakumbuka kipindi flani mwaka 1999 nikiwa nafanya kazi kampuni moja ya utafiti kanda ya ziwa, kampuni iliwaalika viongozi wa kijiji tulipokuwa tunafanyia shughuli zetu. Main ishu ilikuwa ni kuzungumzia namna gani kampuni inaweza kusaidia shughuli za maendeleo ya pale kijijini as part of the Corporate Social Responsibility, maajabu ya Musa baada ya mkutano huo ambapo kampuni ilijikomiti kiasi cha kama $100,000, viongozi wa kijiji wakawa wanataka posho. Sasa angalia namna hii desturi ilivyokwenda na kuharibu kabisa utaratibu, yaani mimi nakuita tujadili namna ya kukusaidia halafu unaniomba posho?????

Nachojaribu kukiongelea ni kwamba hili suala la posho ni kubwa maradufu zaidi ya hizo posho za wabunge na Zitto alichofanya ni kulipa attention na ofcourse limepata attention more than ever. The necessary attention.
 
Na kwa kweli hili suala la serikali 'kujaribu' ku remunerate watumishi wake kwa njia ya posho in a long term linawaathiri watumishi wenyewe. Juzi hapa nilimsikia Rt Gen. Sarakikya analalamika mafao ya uzeeni madogo! Ukiangalia sana watu kama hawa walipokuwa kazini walikuwa na mishahara midogo lakini posho na marupurupu lukuki ambayo yalikuwa hayapitii kwenye payroll. Jambo hili athari yake kubwa ni kwamba posho na marupurupu hayo hayachangii kwenye mafao ya uzeeni (kama NSSF, PPF, PSPF etc) ya mtumishi.

Pengine haikuwa rahisi kwa watu kama Sarakikya kuona impact ya posho na marupurupu hayo kutopita kwenye payroll na vivyo hivyo watumishi wa sasa hawaoni athari yake! Ingalikuwa vema kuondoa posho na marupurupu hayo na kuboresha mishahara. Na kama wengine walivyokwisha sema tatizo la posho hizo, si watumishi wote wananufaika nazo.
 
Na kwa kweli hili suala la serikali 'kujaribu' ku remunerate watumishi wake kwa njia ya posho in a long term linawaathiri watu mishi wenyewe. juzi hapa nilimsikia Rt Gen. Sarakikya analalamika mafao ya uzeeni madogo! Ukiangalia sana watu hawa walipokuwa kazini walikuwa na mishahara midogo lakini posho na marupurupu lukuki ambayo hayapitii kwenye payroll. Jambo hili atahri yake kubwa ni kwamba posho na marupurupu hayo hayachangii kwenye mafao ya uzeeni (kama NSSF, PPF, PSPF etc) ya mtumishi.

Pengine haikuwa rahisi kwa watu kama Sarakikya kuona impact ya posho na marupurupu hayo kutopita kwenye payroll na vivyo hivyo watumishi wa sasa hawaoni athari yake! Ingalikuwa vema kuondoa posho na marupurupu hayo na kuboresha mishahara. Na kama wengine walivyokwisha sema tatizo la posho hizo, si watumishi wote wananufaika nazo.
Mkuu SMU hapa tunajitaidi kumuelimisha mtu ambaye kesha goma kuelimika, ukisoma badiko la huyo malechela utaona kuwa hajui hata msingi wa hoja ya Zitto kabsaa amekalia kubisha tu.
Ishu ya Zitto ni kupinga sitting allowance ambayo madhara ya hiyo posho yammekua makubwa kuliko na vile vile inabagua wafanyakazi wengine! huwezi kujadili swala linalohusu kazi yako then tukulipe wakati unalipwa mshahara.
ukimsoma malechela utaona kua anafikiria tumbo na sio kichwa kwakweli
 
Na kwa kweli hili suala la serikali 'kujaribu' ku remunerate watumishi wake kwa njia ya posho in a long term linawaathiri watu mishi wenyewe. juzi hapa nilimsikia Rt Gen. Sarakikya analalamika mafao ya uzeeni madogo! Ukiangalia sana watu hawa walipokuwa kazini walikuwa na mishahara midogo lakini posho na marupurupu lukuki ambayo hayapitii kwenye payroll. Jambo hili atahri yake kubwa ni kwamba posho na marupurupu hayo hayachangii kwenye mafao ya uzeeni (kama NSSF, PPF, PSPF etc) ya mtumishi.

Pengine haikuwa rahisi kwa watu kama Sarakikya kuona impact ya posho na marupurupu hayo kutopita kwenye payroll na vivyo hivyo watumishi wa sasa hawaoni athari yake! Ingalikuwa vema kuondoa posho na marupurupu hayo na kuboresha mishahara. Na kama wengine walivyokwisha sema tatizo la posho hizo, si watumishi wote wananufaika nazo.

William Malecela haelewi hilo kwani mzee Tinga Tinga kaondoka na Nssf, PPF nk za kwake na wajukuu zake. Yeye alijikatia share yake na ukoo. Hivyo hizo check hazimuhusu wala hataki kujua kuhusu watanzania wengine wakistaafu itakuwaje. Mimi ndugu zangu wanapata 45,000 kwa mwezi toka nssf. kweli mtu ataishi? na alipokuwa anafanyakazi alikuwa analipwa vizuri ila cha juu chote kilikuwa allowance sijui ndo posho au nini. Mimi mwenyewe hapa kazini mshara ni moja ya nane ya take home. Mwajiri kakimbia kulipa kodi na makato ya nssf. sasa ananijazia allowance za kumwaga ili fedha ifikie tulipokubaliana, sasa naanza kutia akili miaka sitini ikifika nitatia aibu.
 
Mkuu Willy, sisi wengine tuanjua baba zetu waliishi vipi katika utumishi wa taifa hili. Natunajua fika msukumo wao na upendo wao katika kulijenga taifa.Kipato chao kilikuwa kidogo sana tena sana na bado wakalitumikia taifa kwa moyo mmoja.
Wale waliokuwa na mioyo midogo ndiyo wakaingia mikataba hii ya kupewa "kitu kidogo" ili kujiongezea kipato.
Tunakumbuka vyema lile basi la zebra la UDA miaka hiyo.Basi ambalo alipewa kwa kificho mtu aliyeenda kuweka sahihi mkataba.
Kuna mifano mingi tu lakini kimsingi kipato kina uhusiano na utendaji wa mtu.Mlipe mtu vizuri na unaweza kumdai kazi nzuri.
Tunakumbuka vile vile miaka ya mwishoni mwa 1960's Mwalimu alipojipunguzia mshahara, ilikuwa na trickle down effect kwa nchi nzima.
Kweli Mh. Zitto hajalifanyia utafiti suala hili.
My take ni mlipe mtu vizuri na umdai kazi kwa malipo hayo

Lole una hoja lakini kinachoendelea in the field sicho unachokidhania. Malipo mazuri ni yale ambayo mtu ameyatolea jasho. Posho zinazozungumziwa very likely hao wazazi wetu wangekuwa huko serikalini leo hii bado inawezekana wasingefaidi chochote unless kama wangekuwa kwenye ile top 15%. Leo hii pamoja na hiyo miposho maisha ya karani wa mahakama bila rushwa hayawezi kwenda hata kwa wiki moja, wauguzi, walimu wanafaidije hizo posho?

Anachokiongea Zito ni kwamba toa hiyo posho ya waheshimiwa kufanya majukumu yao lete huku chini na ndiyo maana kima cha chini cha mshahara kinaongezeka mpaka 315,000.00
 
@ Facebook: by William Malecela on Wednesday, June 15, 2011 at 10:57pm

@ NEW YORK CITY - USA: Ujira wa Wabunge wetu wanapokuwa bungeni kutuwakilisha wananchi, je ni mkubwa sana kuliko uwezo wetu Nationally, au ni just another political stunt aiming at gaining temporary political populism?

mishahara na marupurupu manono yalianza baada ya serikali zilizofuatia ile awamu ya kwanza ya Nyerere kuamua kuboresha maslahi ya viongozi wa juu. viongozi waliokuwa wanastaafu kutoka awamu ya Nyerere walionekana wanasota mtaani. hii ni kwa sababu mwelekeo wa serikali ya Nyerere ulikuwa ni kuboresha maisha kwa wote, hasa walala hoi walio wengi. serikali iliwekeza sana kwa njia ya ruzuku katika maeneo mbalimbali. baada ya kukubaliana na IMF na World Bank, ruzuku hizo ziliondolewa na kwa sababu mbalimbali maisha yalikuwa magumu kwa walio wengi na viongozi wakuu waliokuwa wanastaafu walipata kibano hicho sawia. hawa viongozi wa awamu zilizofuatia waliamua kuboresha maslahi yao ili wasije adhirika kama hawa. yaani wajilinde wao na wengine waendelee kusota. protect and provide for the few. miswada ilipoletwa bungeni, wabunge nao wakagoma kupitisha kwa sharti na wao wawekwe humo. serikali ikaona naam! hapa pazuri, maana kama bunge ndio linaloidhibiti serikali kwa mujibu wa katiba, kama nao watajiunga katika ulaji basi watakuwa washiriki katika ufisadi wa kitaasisi. serikali itakuwa na freehand. ndio ukawa mwanzo wa mwelekeo wa kuboresha maslahi ya wachache walio katika mamlaka na kuacha wengine. hii ime-trickle down mpaka katika ngazi za chini. kila sekta inajiboreshea mambo yake wanavyoona. ni mzigo kwa taifa sio tu kwa kuangalia tu hiyo "sitting allowances" bali angalia impact ya mwelekeo mzima wa wakubwa kujiboreshea mambo yao, na hiyo trickle-down effect ya uozo, halafu jenga picha.

Tanzania ndio kwanza tumetoka kwenye siasa za the Doomed Communism, we are still in the transition or work in progress towards Capitalism and then kabla hatujaenda mbaali sana
Tanzania haikuwa na haijawahi kuwa nchi ya kikomunisti. ni kweli sera za Nyerere zilikuwa na mapungufu yake, lakini mwelekeo mzima ulikuwa focus kwa walio wengi. kuwapa fursa za kuboresha maisha yao. lakini basi afadhali kama tungeelekea kweli katika Capitalism. maana capitalism inazo taratibu zake. sheria ni kali na ndio maana hata CITIBank ya Marekani ilikataa kutoa dhamana kwa kampuni feki ya Richmond. kodi zinakusanywa - angalia wachezaji/wasanii maarufu duniani wanavyolipa kodi. angalia jinsi marekani walivyoishughulikia BP kutokana na kuvuja kwa mafuta Gulf of Mexico. linganisha na uvujaji wa maji machafu ya migodini kule Nyamongo. Marekani mwekezaji hawezi kupiga risasi raia ovyo, kama hapa kwetu Tanzania. au huu ni Ubepari wa Tanzania tu? ubepari una miiko yake ya kibepari - ni mfumo ambao unaweza kuukosoa, lakini Tanzania hatufuati ubepari wala ujamaa wala ukomunisti. ni vurugu na holela.

recently kumekua na vilio vya kutaka kurudi kwenye Azimio La Arusha na the so called maadili ya uongozi, now here comes this which in the large picture ni kupunguziana ujira makazini. Hapa ndipo huwa ninauliza hivi: Hili taifa tulilogwa na nani?
Hata mabepari wana maadili yao. kuna mambo ambayo kiongozi wa kitaifa hawezi kuyafanya akiwa madarakani. kama unafikiri maendeleo ni majengo marefu na mabilionea wachache, basi tunatofautiana sana. kwangu mimi maendeleo ni maendeleo ya watu katika sekta mbalimbali kiafya, kielimu, kisayansi, kiutendaji, ufugaji,nk.

NO! Wa-Tanzania tumetoka mbali sana na matatizo ya ujira makazini, taifa letu limepoteza wataalamu wakubwa sana waliobobea kwenye fani mbali mbali Duniani kwa sababu ya kuogopa kwao kufanya kazi Tanzania kisa cha ujira mdogo sana kulinganisha na ujuzi walionao ambao sisi as a Nation tuliuhitaji sana

Kinachopigiwa kelele ni kipengele kimoja tu katika mwelekeo mbovu wa watawala kuwahonga wabunge ili wafanye watakaavyo. ningependa tuuangalie upya na kuuchambua huu mwelekeo uliozaa ndoa ya maslahi kati ya bunge na serikali. bunge libaki kuwa ni bunge, ambapo mbunge analipwa kiasi kidogo tu kwa ajili ya kutimiza majukumu yake. anacholipwa sasa ni hongo. kumbuka maslahi katika sekta mbalimbali muhimu hayajaboreshwa, mifumo ni mibovu, na ndio inachangia sasa watalaamu wetu kuondoka. ila maslahi katika kazi za siasa yako juu sana. hiyo sio sawa hata kidogo.

- Tulipoingia siasa za vyama vingi as a nation, tulikubaliana kimsingi kwamba Viongozi wetu wa taifa tuwalipe kulingana na hali halisi ya maisha, ili kuwaondoa kwenye tamaa za Rushwa, huenda Mheshimiwa hakuwepo wakati huo au alikuwa mdogo sana kiumri, lakini anapaswa kuelewa kwamba huo ujira uliwekwa kwa sababu za kimsingi sana zilizojali maisha ya Viongpozi wetu kama sisi wananchi wengine wote, ambao in the wake of ujira mdogo wakati tunalitumikia taifa inaweza kutupelekea kufanya maamuzi mengi against taifa kuelekezea kwenye matumbo yetu zaidi kwa sababu ya ujira mdogo sana kutoka kwenye taifa letu wenyewe tunalolitumikia usiku na mchana.
Nimechambua hapo juu msingi wa wakubwa kulipana vizuri. na historia inaonesha kwamba hata kama ukimlipa mtu vizuri, haina maana kwamba hatataka zaidi. kinachotakiwa ni checks and balances. maadili. misingi ya utaifa. ni kwa nini watu zamani walilipwa kidogo lakini walifanya kazi sana? sasa hivi mishahara katika baadhi ya sekta ni mikubwa lakini utendaji sio mzuri. lakini katika mashirika binafsi na hasa yale ya kimataifa, utendaji ni mzuri kwa sababu usimamizi ni mzuri, of course mshahara pia ni mzuri. lakini mtu unaweza ukampa mshahara mzuri lakini kusiwepo usimamizi, basi atatumia muda wa kazi kufanya mambo mengine ili kupata fedha zaidi na zaidi

 
Two of William's siblings are direct beneficiaries of this posho thing......one a DG the other a Judge...thats why he is so bitter....if we look at it that way....how could he advocate that someone should be paid allowances for a job that one is also salaried as well beats me!
 
Nakumbuka kipindi flani mwaka 1999 nikiwa nafanya kazi kampuni moja ya utafiti kanda ya ziwa, kampuni iliwaalika viongozi wa kijiji tulipokuwa tunafanyia shughuli zetu. Main ishu ilikuwa ni kuzungumzia namna gani kampuni inaweza kusaidia shughuli za maendeleo ya pale kijijini as part of the Corporate Social Responsibility, maajabu ya Musa baada ya mkutano huo ambapo kampuni ilijikomiti kiasi cha kama $100,000, viongozi wa kijiji wakawa wanataka posho. Sasa angalia namna hii desturi ilivyokwenda na kuharibu kabisa utaratibu, yaani mimi nakuita tujadili namna ya kukusaidia halafu unaniomba posho?????
Yaani hapo mkuu umenena. hii kansa ya posho imetrickle down mpaka vijijini na kutuvuruga kwelikweli! nakumbuka hapa Dar kuna jamaa walikuja kutoa training ya technology moja muhimu sana. waalikwa kutoka institutions si wakataka wakatiwe bahasha. na walipoona hakuna bahasha wakasepa. hawakuonekana tena! na hao ndio ma-instructor wetu ambao wanatakiwa kutumia nafasi hiyo kujifunza tekinolojia mpya. jamaa walipokwenda South Africa nasikia watu walikuwa walijaa tena kwa kulipia fee, wakati hapa kwetu ilikuwa free. siku hizi bila bahasha watu hawaendi kwenye semina au warsha. suala ni posho tu, na si kingine. hata hao wabunge, watoa semina wengi wamelalamika kwamba unapokwenda kutoa training kule kwa wabunge, tena training ya kuwasaidia wao, unaambiwa uwalipe na posho! huu ni ungonjwa mbaya sana unaohitaji kutafutiwa tiba tena ya haraka. suala sio tu posho za wabunge, bali mfumo mzima wa wizi wa kitaasisi kama alivyosema Mbowe
 
Bilioni 900 kwa kulipia posho hivi bajeti yetu inategemea wahisani kwa kiasi gani? Hiki ni kichekesho yaani tukope na kuombaomba ili tulipe posho za wabunge badala ya kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo? Hivi viwango vya posho ni kinyume na uwezo wetu; bunge lenyewe limekuwa ni kama rubber stamp halina tija; siasa ni wito kama wapo kutaka kujinufaisha wende shule wakafute fani; wameweka maslahi yao mbele; hizi posho ndizo zinazosababisha bunge letu kukosa mvuto wa kisiasa wabunge wanaishia kulala ndani ya vikao vya bajeti huku wengine wakikosa kuhudhuria vikao hawana wasiwasi posho zinaingia; ni AIBU kuona wabunge wetu hawapo tayari kutetea maslahi ya watanzania wengine, mbunge hata umlipe kiasi kama hana kanuni na miiko ya uongozi atachukua rushwa na kujiingiza kwenye ufisadi mifano hai ipo.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
I quite agree with you there William,hawa vijana waliopata umaarufu hawajui taifa hili limetoka wapi.
Idadi ya ma Engineer, Madaktari na wataalamu wengi tu waliotimkia nchi za nje kwa sababu moja tu-mishahara midogo nafikiri Mh Zitto hili halijui.
Atalijuaje wakati hata uzoefu wakazi kwake ni bungeni tu?
Ni vizuri kealipa watu vizuri na kuwawajibisha katika utendaji.
Nakubaliana na hapo penye nyekundu, ila hapo pa bluu sio kweli kabisa. Lakini hizi posho si ndio zinazopunguza mishahara mizuri? Nadani ya serikali na taasisi zake nyingi, wanaolipwa hizi allowance ni chini ya % 5, nao ni wale wakuu wa vitengo na wanaofanana na hao. Unajua katika hospitali ya wilaya anaeweza kuwa anapata hizi "sitting allowances" anaweza kuwa mganga mkuu, pamoja na wale macoordinators wa miradi mbalimbali kama HIV/AIDS n.k? Unafahamu kuwa hawa wala hawatekelezi majukumua yao ya msingi kwa sababu ya kuhanja kwenye mikutano yenye hizi posho?

Hizi posho zinalipwa kwa wale wenye mishahara ya mamilioni, na wala sio watendaji wa kazi. Kwanini ushishauri hizi posho zikaelekezwa kuongeza mishahara duni ya waliowengi?
 
Wjm anapotosha ukweli makusudi.hakuna asiyeelewa suala la posho na marupurupu mengi yasiyo na maana tameiharibu nchi.
Rushwa imekuwa ni jadi ya siasa madaktari engineers,walimu na wataalamu wengi wamekimbia fani zao kukimbilia siasa kwa sababu ya makosa yaliyofanyika.
Huyu mtoto wa malechela anatetea ufisadi na rushwa katika kutafuta ubunge.
Mbunge ni kiongozi na uongozi haunu nuliwi.hata mshahara wa mbunge napendekeza upunguzwe ili tupae viongozi wenye uchungu na nchi kama t sanga,mzindakaya,j.malchela( kabla hajaharibiwa na mfumo wa sasa) na wengineo waliojitolea kulitumikia taifa.na ndio hapo tutawatoa wafanyabiashara waliohonga ili wawe wabunge wapate vip pas.
Bunge limejaza takataka nyingi zinazotafuna hela za walipa kodi masikini,wanatunga sheria za kulinda makampuni yao ya mafuta.
Wewe wjm una lako jambo na nakuhakikishia hutafanikiwa kwani serikali ya chama chako imeshalibaini hata kama ni kinafiki kama walivyozoea sisi hatulali mpaka kieleweke.mishahara kwa wafanyakazi iongezwe.
Tunataka madaktari ,maengineer,maprof,walimu waache kukimbilia ubunge warudi kufanya kazi walizosomea ili pamoja tulikomboe taifa.
Turudishe 110 kwa wabunge ili heshima ya madaktari,walimu irudi
tuache unafiki wa huyu kijana anayatetea kitu kisicho na maslahi kwa uma yeye anachanganya fani ya mtu na siasa.
 
Inatia kinyaa kuabudu last name. Hata wakileta upupu hapa kila mtu anajadili kwa sababu babake alikuwa fisadi. Tuanze kujadili vile vyenye manufaa bila kujali jina la mwisho.
 
Back
Top Bottom