barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,863
Wakuu,kama tulimsikia Rais leo pale Ikulu,amemgusia Lissu
Akasema kuna mtu ni msomi na mtaalamu wa sheria,toka huko nyuma alikuwa mwanaharakati na watu wakam-lebo kama mtetezi wa mazingira.
Lakini kwa sasa,naona "siasa" zinamfanya atofautiane na mimi...Rais akasema,jamani hili jambo haliitaji siasa,tuungane kwa pamoja.
Hapo hapo Rais akajisahau kuwa dakika mbili zilizopita aliomba tuuangane na tuwe wamoja,kidogo akamgeukia Spika na kumuagiza "kuwakomesha" wabunge wa upinzani,akamuagiza awatoe nje ya bunge ili yeye aje awashughulikie huku nje.Kwamba leo wamegawana,mmoja awabane bungeni kw kuwapa adhabu za kuanzia mwezi mpaka mwaka,na mwingine atakuwa nje ya bunge akiwathibiti kwa kuwaweka ndani na kuwapa kesi za hapa na pale.
Kifupi,leo wakuu wawili wa mihimili ya dola wamegawana majukumu ya namna ya kuwashughulikia wapinzani,mmoja kapewa kazi na namna ya kufanya ndani ya bunge,na mwingine kajipangia naman atakavyowaadabisha watakapokuwa nje ya bunge.
Huyu wa bungeni kaagizwa kabisa,kuwa "adhabu" ianzie mwezi mmoja ili hao "waropokokaji" wakose uwanja wa kuihoji na kuikosoa serikali,huyu mwingine kaapa kuwashughulikia wakiwa nje ya bunge.Mkuu wa mhimili anapatana na mkuu wa mhimili mwingine kuwadhibiti watu wa muhimili wake.
Hapa unajiuliza,hii "Separation of Power" ipo wapi?!Hiyo ambayo mwalimu wa somo la Siasa sekondari alitufundisha inaitwa "Check and Balance" iatakuwaje?Yaani mkuu wa muhimili mmoja unapewa maagizo ya namna ya kuwashughulikia watu wa muhimili wako ulio huru na wewe unakubali tena mbele ya kamera??
Yaani ni sawa na leo Spika aamue kumwambia mkuu wa muhimili wa serikali,awaadhibu mawaziri na awatoe ndani ya baraza la mawaziri kwa kuwasimamisha.Kama Rais atakubali,basi kwanza atakuwa amejimaliza yeye na baraza lake la mawaziri,na pia ametii maagizo ya kumuangamiza toka katika muhimili mwingine.
Leo ndio tumethibitisha ile kauli ya "Maagizo toka juu" huwa inatokea wapi,bahati mbaya au nzuri,leo "Maagizo toka juu" yamesemwa hadharani na tumeyasikia.
Spika akumbuke tu kuwa Bunge ni muhimili unaojitegemea,yeye ni mbunge aliyeschaguliwa kuwa Spika,na yeye si sehemu ya serikali bali bunge.Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali na kuiwajibisha,kuikosoa na kuirekebisha.Sio kazi ya serikali kuagiza bunge kuwaathibu wabunge wake,bali bunge lina utaratibu wa kuwaadhibu wabunge wake kwa mujibu wa sheria,taratibu na kanuni za kibunge walizojiwekea.
Wakati mwingine Ngosha anafurahisha mwanzo wa sherehe,pale inapotaka kunoga anatia togwa maji.Sijui ni kujisahau tu au ndio hulka,maana dakika moja anasema mambo haya hayana vyama,dakika tano baadae anatoa kauli ya kuwagawa watu kiitikadi.
Ngosha anaomba umoja wa kitaifa katika kumsakama "adui" makinikia,lakini hapo hapo wale ambao ni sehemu ya kumsaidia kuunganisha Taifa,anawajengea kisasi cha kuwakamata na kuwafukuzisha bungeni.Umoja wa kitaifa,haujengwi kwa visasi na kukomoana.
Kumbe yale ya "adhabu za mwaka mzima nje ya bunge" yanaweza kuwa ni maagizo ya aina hii toka juu.Bunge lijitahidi kujitenga na siasa za "maagizo toka juu".