Agizo la Rais kwa Spika "kuwaminya" Wapinzani, inathibitisha ile "maagizo toka juu" husemwa na nani

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Wakuu,kama tulimsikia Rais leo pale Ikulu,amemgusia Lissu
Akasema kuna mtu ni msomi na mtaalamu wa sheria,toka huko nyuma alikuwa mwanaharakati na watu wakam-lebo kama mtetezi wa mazingira.

Lakini kwa sasa,naona "siasa" zinamfanya atofautiane na mimi...Rais akasema,jamani hili jambo haliitaji siasa,tuungane kwa pamoja.

Hapo hapo Rais akajisahau kuwa dakika mbili zilizopita aliomba tuuangane na tuwe wamoja,kidogo akamgeukia Spika na kumuagiza "kuwakomesha" wabunge wa upinzani,akamuagiza awatoe nje ya bunge ili yeye aje awashughulikie huku nje.Kwamba leo wamegawana,mmoja awabane bungeni kw kuwapa adhabu za kuanzia mwezi mpaka mwaka,na mwingine atakuwa nje ya bunge akiwathibiti kwa kuwaweka ndani na kuwapa kesi za hapa na pale.

Kifupi,leo wakuu wawili wa mihimili ya dola wamegawana majukumu ya namna ya kuwashughulikia wapinzani,mmoja kapewa kazi na namna ya kufanya ndani ya bunge,na mwingine kajipangia naman atakavyowaadabisha watakapokuwa nje ya bunge.

Huyu wa bungeni kaagizwa kabisa,kuwa "adhabu" ianzie mwezi mmoja ili hao "waropokokaji" wakose uwanja wa kuihoji na kuikosoa serikali,huyu mwingine kaapa kuwashughulikia wakiwa nje ya bunge.Mkuu wa mhimili anapatana na mkuu wa mhimili mwingine kuwadhibiti watu wa muhimili wake.

Hapa unajiuliza,hii "Separation of Power" ipo wapi?!Hiyo ambayo mwalimu wa somo la Siasa sekondari alitufundisha inaitwa "Check and Balance" iatakuwaje?Yaani mkuu wa muhimili mmoja unapewa maagizo ya namna ya kuwashughulikia watu wa muhimili wako ulio huru na wewe unakubali tena mbele ya kamera??

Yaani ni sawa na leo Spika aamue kumwambia mkuu wa muhimili wa serikali,awaadhibu mawaziri na awatoe ndani ya baraza la mawaziri kwa kuwasimamisha.Kama Rais atakubali,basi kwanza atakuwa amejimaliza yeye na baraza lake la mawaziri,na pia ametii maagizo ya kumuangamiza toka katika muhimili mwingine.

Leo ndio tumethibitisha ile kauli ya "Maagizo toka juu" huwa inatokea wapi,bahati mbaya au nzuri,leo "Maagizo toka juu" yamesemwa hadharani na tumeyasikia.

Spika akumbuke tu kuwa Bunge ni muhimili unaojitegemea,yeye ni mbunge aliyeschaguliwa kuwa Spika,na yeye si sehemu ya serikali bali bunge.Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali na kuiwajibisha,kuikosoa na kuirekebisha.Sio kazi ya serikali kuagiza bunge kuwaathibu wabunge wake,bali bunge lina utaratibu wa kuwaadhibu wabunge wake kwa mujibu wa sheria,taratibu na kanuni za kibunge walizojiwekea.

Wakati mwingine Ngosha anafurahisha mwanzo wa sherehe,pale inapotaka kunoga anatia togwa maji.Sijui ni kujisahau tu au ndio hulka,maana dakika moja anasema mambo haya hayana vyama,dakika tano baadae anatoa kauli ya kuwagawa watu kiitikadi.

Ngosha anaomba umoja wa kitaifa katika kumsakama "adui" makinikia,lakini hapo hapo wale ambao ni sehemu ya kumsaidia kuunganisha Taifa,anawajengea kisasi cha kuwakamata na kuwafukuzisha bungeni.Umoja wa kitaifa,haujengwi kwa visasi na kukomoana.

Kumbe yale ya "adhabu za mwaka mzima nje ya bunge" yanaweza kuwa ni maagizo ya aina hii toka juu.Bunge lijitahidi kujitenga na siasa za "maagizo toka juu".
 
Hili ndio tatizo kubwa la Magufuli ila afahamu tu Watanzania sio wapumbavu yaani anataka yeye na ccm waonekane wema na wapinzani kina Lisu ndio mashetani wakati hao kina Lisu hata access ya kujua wameingia mikataba ipi hawana

Sasa yeye acha awashughulikie huko nje ya bunge kama anavyosema na ukiongeza na matatizo ya ukabila na udini na ushetani mwingine unaonyemelea taifa letu kama mauaji ya Kibiti halafu tuone atauchezaje huo mziki..

Hakuna mtu ana shida na nia yake njema ila shida ipo anapotaka kutuaminisha matatizo ya nchi hii yameletwa na upinzani wakati ni watu anao lala nao na kuamka nao

Na huko anaposema sijui tuungane tuwe kitu kimoja wakati matendo yake hayahakisi anachokisema
 
Kumbe Barafu hauko huru like you marketed yesterday? Unatumiwa na mafisadi
Jana kuitetea ATCL ukaniona nipo "huru",leo kuhoji kauli ya Mkuu kumuagiza spika kushughulikia watu wa muhimili wake unaona sipo "huru"

Na wale waliosema jana nimetumwa na CCM kuitetea ATCL na kuwa nina njaa za Lumumba,leo watakuja hapa na kusema "Kamanda umegonga penyewe".Ili mradi kila mtu anataka usiwe huru kufikiri na kuchangia kwa mtazamo usio na kifungo.

Mkuu Troll JF aina hiyo ya siasa na maisha hayo,mimi nilishavuka,najiweka huru tu kujadili lile ambalo kwa mtazamo wangu naona ni sahihi,sitaki kuinyima uhuru nafsi yangu na uzee huu,kama kujipendekeza,tulijipendekeza sana enzi za Julius na TANU YOUTH LEAGUE,hatimaye Julius akang'atuka na mwisho kafariki.Kuwa huru tu kijana wangu
 
Kumbe Barafu hauko huru like you marketed yesterday? Unatumiwa na mafisadi

366fac4e246feec2ed0e689d04b311d2.jpg
 
Jana kuitetea ATCL ukaniona nipo "huru",leo kuhoji kauli ya Mkuu kumuagiza spika kushughulikia watu wa muhimili wake unaona sipo "huru"

Na wale waliosema jana nimetumwa na CCM kuitetea ATCL na kuwa nina njaa za Lumumba,leo watakuja hapa na kusema "Kamanda umegonga penyewe".Ili mradi kila mtu anataka usiwe huru kufikiri na kuchangia kwa mtazamo usio na kifungo.

Mkuu Troll JF aina hiyo ya siasa na maisha hayo,mimi nilishavuka,najiweka huru tu kujadili lile ambalo kwa mtazamo wangu naona ni sahihi,sitaki kuinyima uhuru nafsi yangu na uzee huu,kama kujipendekeza,tulijipendekeza sana enzi za Julius na TANU YOUTH LEAGUE,hatimaye Julius akang'atuka na mwisho kafariki.Kuwa huru tu kijana wangu
Kila laheri Mkuu katika harakati zenu za kututoa Madarakani mwaka 2115.
 
Hili ndio tatizo kubwa la Magufuli ila afahamu tu Watanzania sio wapumbavu yaani anataka yeye na ccm waonekane wema na wapinzani kina Lisu ndio mashetani wakati hao kina Lisu hata access ya kujua wameingia mikataba ipi hawana

Sasa yeye acha awashughulikie huko nje ya bunge kama anavyosema na ukiongeza na matatizo ya ukabila na udini na ushetani mwingine unaonyemelea taifa letu kama mauaji ya Kibiti halafu tuone atauchezaje huo mziki..

Hakuna mtu ana shida na nia yake njema ila shida ipo anapotaka kutuaminisha matatizo ya nchi hii yameletwa na upinzani wakati ni watu anao lala nao na kuamka nao

Na huko anaposema sijui tuungane tuwe kitu kimoja wakati matendo yake hayahakisi anachokisema
Asante Mkuu, U nailed it.
 
Back
Top Bottom