Agizo la Rais kwa Spika "kuwaminya" Wapinzani, inathibitisha ile "maagizo toka juu" husemwa na nani

Inafurahisha kuona kwamba wabunge wa wapinzani wanapata adhabu kali sana kuliko wanayopata 'ACACIA'! Ndipo ngozi nyeusi tulipofika. Kauli ya 'Maendeleo hayana chama' ni kauli ya kunywea kahawa kijiweni, sio ya kuitilia maanani.

Kwa hili la kukandamiza upinzani, sitakuja kumuunga mkono huyu mzee wetu. Wakati mwingine unaweza ukahisi makinikia ni sarakasi tu, halina dhamira ya kweli ya kukomboa mtanzania. Ni la kupatia kiki na kura. Tukutane 2020 ili tukuonyeshe kuwa kama hutupendi hata sisi hatukupendi.
 
Kumbe Barafu hauko huru like you marketed yesterday? Unatumiwa na mafisadi
Mkuu ukiuvaa ukada unajiwekea kitanzi cha kukukaba koo kuzungumzia ukweli au unachokiamini rohoni mwako. Maana haya mazuri ya JPM usifikiri makada wa CDM hawayaoni, na nyie pia kada wa CCM sio kwamba hamuoni mazuri ya wapinzani. Mimi nimependa mleta mada amekuwa huru kifikra na ametumia lugha ya staha kufikisha ujumbe kwa mlengwa. Ukada ni upofu wa fikra huru.
 
Sq
Jana kuitetea ATCL ukaniona nipo "huru",leo kuhoji kauli ya Mkuu kumuagiza spika kushughulikia watu wa muhimili wake unaona sipo "huru"

Na wale waliosema jana nimetumwa na CCM kuitetea ATCL na kuwa nina njaa za Lumumba,leo watakuja hapa na kusema "Kamanda umegonga penyewe".Ili mradi kila mtu anataka usiwe huru kufikiri na kuchangia kwa mtazamo usio na kifungo.

Mkuu Troll JF aina hiyo ya siasa na maisha hayo,mimi nilishavuka,najiweka huru tu kujadili lile ambalo kwa mtazamo wangu naona ni sahihi,sitaki kuinyima uhuru nafsi yangu na uzee huu,kama kujipendekeza,tulijipendekeza sana enzi za Julius na TANU YOUTH LEAGUE,hatimaye Julius akang'atuka na mwisho kafariki.Kuwa huru tu kijana wangu
safi sana wanafikiri kila mtu ni mfia chama.......ukweli utasemwa tu bila kujali nani kakosea
 
Lisu kiboko ya mabashite yote..haya mvunja nazi kakubali kukaa nao meza moja wezi na shughuli imeisha watu wameanua matanga
Umeasahau Lissu mpenda sifa na mropokaji anataka mchanga tuachie huku tukidai haki zetu lakini mvunja nazi kasema mchanga hautoki na waje wakiri makosa kisha tukae meza moja.
 
Hiyo spika mikataba yote mibovu inamhusu plus wabunge wote wa chama chakavu waliosema ndiyo kupitisha hiyo mikataba.
Hi kashfa haitawaacha chama chakavu salama
 
Jana kuitetea ATCL ukaniona nipo "huru",leo kuhoji kauli ya Mkuu kumuagiza spika kushughulikia watu wa muhimili wake unaona sipo "huru"

Na wale waliosema jana nimetumwa na CCM kuitetea ATCL na kuwa nina njaa za Lumumba,leo watakuja hapa na kusema "Kamanda umegonga penyewe".Ili mradi kila mtu anataka usiwe huru kufikiri na kuchangia kwa mtazamo usio na kifungo.

Mkuu Troll JF aina hiyo ya siasa na maisha hayo,mimi nilishavuka,najiweka huru tu kujadili lile ambalo kwa mtazamo wangu naona ni sahihi,sitaki kuinyima uhuru nafsi yangu na uzee huu,kama kujipendekeza,tulijipendekeza sana enzi za Julius na TANU YOUTH LEAGUE,hatimaye Julius akang'atuka na mwisho kafariki.Kuwa huru tu kijana wangu
Hongera sana kwakuwa "Free minded"..... Mahaba ya vyama yanapofusha.....


WanaCCM na Wapinzani wote wanaangalia maslahi ya vyama vyao kabla ya kuangalia maslahi ya "Mama Tanzania".
 
Umeasahau Lissu mpenda sifa na mropokaji anataka mchanga tuachie huku tukidai haki zetu lakini mvunja nazi kasema mchanga hautoki na waje wakiri makosa kisha tukae meza moja.
Bora mropokaji kuliko aliyenyanyua makwapa na kushangilia upitishwaji wa miswaada ya madini halafu leo anamachungu sijui akili huwa wanaacha kabatini,halafu unamwambia mwizi aje akiri makosa mkae nae meza moja ni akili au matope?
 
Wakuu,kama tulimsikia Rais leo pale Ikulu,amemgusia Lissu
Akasema kuna mtu ni msomi na mtaalamu wa sheria,toka huko nyuma alikuwa mwanaharakati na watu wakam-lebo kama mtetezi wa mazingira.

Lakini kwa sasa,naona "siasa" zinamfanya atofautiane na mimi...Rais akasema,jamani hili jambo haliitaji siasa,tuungane kwa pamoja.

Hapo hapo Rais akajisahau kuwa dakika mbili zilizopita aliomba tuuangane na tuwe wamoja,kidogo akamgeukia Spika na kumuagiza "kuwakomesha" wabunge wa upinzani,akamuagiza awatoe nje ya bunge ili yeye aje awashughulikie huku nje.Kwamba leo wamegawana,mmoja awabane bungeni kw kuwapa adhabu za kuanzia mwezi mpaka mwaka,na mwingine atakuwa nje ya bunge akiwathibiti kwa kuwaweka ndani na kuwapa kesi za hapa na pale.

Kifupi,leo wakuu wawili wa mihimili ya dola wamegawana majukumu ya namna ya kuwashughulikia wapinzani,mmoja kapewa kazi na namna ya kufanya ndani ya bunge,na mwingine kajipangia naman atakavyowaadabisha watakapokuwa nje ya bunge.

Huyu wa bungeni kaagizwa kabisa,kuwa "adhabu" ianzie mwezi mmoja ili hao "waropokokaji" wakose uwanja wa kuihoji na kuikosoa serikali,huyu mwingine kaapa kuwashughulikia wakiwa nje ya bunge.Mkuu wa mhimili anapatana na mkuu wa mhimili mwingine kuwadhibiti watu wa muhimili wake.

Hapa unajiuliza,hii "Separation of Power" ipo wapi?!Hiyo ambayo mwalimu wa somo la Siasa sekondari alitufundisha inaitwa "Check and Balance" iatakuwaje?Yaani mkuu wa muhimili mmoja unapewa maagizo ya namna ya kuwashughulikia watu wa muhimili wako ulio huru na wewe unakubali tena mbele ya kamera??

Yaani ni sawa na leo Spika aamue kumwambia mkuu wa muhimili wa serikali,awaadhibu mawaziri na awatoe ndani ya baraza la mawaziri kwa kuwasimamisha.Kama Rais atakubali,basi kwanza atakuwa amejimaliza yeye na baraza lake la mawaziri,na pia ametii maagizo ya kumuangamiza toka katika muhimili mwingine.

Leo ndio tumethibitisha ile kauli ya "Maagizo toka juu" huwa inatokea wapi,bahati mbaya au nzuri,leo "Maagizo toka juu" yamesemwa hadharani na tumeyasikia.

Spika akumbuke tu kuwa Bunge ni muhimili unaojitegemea,yeye ni mbunge aliyeschaguliwa kuwa Spika,na yeye si sehemu ya serikali bali bunge.Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali na kuiwajibisha,kuikosoa na kuirekebisha.Sio kazi ya serikali kuagiza bunge kuwaathibu wabunge wake,bali bunge lina utaratibu wa kuwaadhibu wabunge wake kwa mujibu wa sheria,taratibu na kanuni za kibunge walizojiwekea.

Wakati mwingine Ngosha anafurahisha mwanzo wa sherehe,pale inapotaka kunoga anatia togwa maji.Sijui ni kujisahau tu au ndio hulka,maana dakika moja anasema mambo haya hayana vyama,dakika tano baadae anatoa kauli ya kuwagawa watu kiitikadi.

Ngosha anaomba umoja wa kitaifa katika kumsakama "adui" makinikia,lakini hapo hapo wale ambao ni sehemu ya kumsaidia kuunganisha Taifa,anawajengea kisasi cha kuwakamata na kuwafukuzisha bungeni.Umoja wa kitaifa,haujengwi kwa visasi na kukomoana.

Kumbe yale ya "adhabu za mwaka mzima nje ya bunge" yanaweza kuwa ni maagizo ya aina hii toka juu.Bunge lijitahidi kujitenga na siasa za "maagizo toka juu".
Kila kitu kina mwanzo na mwisho ni muda tu.
 
Mtoa Mada una faida ya vitu viwili tu
1-JF kukukubalia kuficha ID yako na kutumia ID fake
2-Endelea kuomba saaanaaa JF ishinde ile kesi yao iliyoko High Court
Kumsingizia RAIS wa nchi kuwa kaweka Amri ya kuwaadhibu wapinzan kuanzia mwezi mmoja hadi mwaka mmoja huku ukijua kuwa hakusema hivyo ni jambo La HATARI Sana kwako...hakuna mpinzan aliyekuwa mentioned pale.. Wala kuonea mtu pale
Ndo Maana nakwambia unapaswa kuomba Sana ILI JF iendelee kuwa kichaka chako.. Otherwise una Wakati mgumu sana best
 
Wakati mwingine ni vyema mtu akawa huru kutoa maoni yake kulingana na aonavyo pasipo kufungwa na upande wowote wa ki itikadi.
 
Ni agizo la kipuuzi sana.
c89003d141531437bdd1e3fd2b9f880c.jpg
 
Back
Top Bottom