Agenda mbaya ya Bernad Membe vyuo vikuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Agenda mbaya ya Bernad Membe vyuo vikuu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ommytah, Apr 30, 2012.

 1. O

  Ommytah Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza napenda kumpongeza sana waziri wa mambo ya nje bw. Bernad Membe. Hajawahi kuwa na kashfa nzito kama hizi zinazopelekea mheshimiwa rais kupangua tena baraza la mawaziri. Kwa upande wake kiukweli amejitahidi sana na ahsante kwa hilo.

  Membe anapoanza kupotea ni pale anapoutafuta urais 2015 kwa nguvu zote hata kwa kutumia pesa za wizara yake kwa usiri mkubwa. Hivi sasa ameanzisha kampeni kubwa ya kuwateka vijana hasa wale wenye UWEZO WA USHAWISHI KWA WENZAO ambao wanapatikana vyuo vikuu. Anataka kutumia nafasi ya kutengeneza makongamano katika vyuo ili kuanza mapema kujitengenezea jina zuri ifikapo 2015.

  Habari nyeti zinasema kuwa bwana Membe akishirikiana na viongozi wa CCM katika vyuo vikuu, anafanya ajenda ya siri kuwarubuni viongozi wa serikali za wanafunzi ( marais wa vyuo) kwa kuwapa pesa ili waandae makongamano yatakayowaunganisha wanafunzi ili apate mwanya wa kutoa hotuba zake za kujiweka safi zaidi.

  Hivi karibuni anaandaa kongamano kubwa kwa kuwatumia wanaCCM vijana wa vyuo vikuu Morogoro (Mzumbe, SUA,St. Jordan, Muslim na Ardhi). Anatumia mwanya huo akijifanya anazungumzia mambo ya ajira na uchumi, maana ameshajinadi sana kuwa yeye ni bingwa sana wa uchumi. Pia amejipanga kuwatumia watu wengine mashuhuri nchini km wafanyabiashara wakubwa, wanamichezo, wanaharakati nk ili kuambatana nao katika hayo makongamano yasiyo na tija kwa vijana. Amepanga bajeti kubwa mno kuweza kuwagharimia usafiri wa bure kutoka vyuoni mwao mpaka pale atakapotaka kuwakusanya hao maelfu ya wasomi wasio na hatia ambao wataingizwa katika wimbi la siasa bila wao wenyewe kujijua. Kwa sasa kongamano kubwa la kuwakutanisha wanavyuo wa Morogoro amepanga kulifanya chuo kikuu Mzumbe katika ukumbi wa NAH (New Assembly Hall), huku akiambatana na mfanyabiashara mkubwa ili kusingizia kuwa ndiye aliyetoa wazo na mapesa kwa ajili ya makongamano hayo.

  Hatukatai mawaziri au wanasiasa kuhutubia katika vyuo vikuu kwani nao kimsingi ni wananchi tena wenye taaluma zao. Lakini kwa nini kuharibu upeo wa kufikiri wa vijana kwa kuwaingiza kwenye siasa?.kwa nini kuwatumia viongozi wa serikali za wanafunzi kueneza itikadi za mtu binafsi ama chama? je, vyuo vikuu vikiongozwa kwa kuangalia itikadi za chama fulani cha siasa, nchi hii itazaa wasomi wa namna gani? tatizo la RUSHWA je, litakwisha kweli ikiwa hawa vijana waddogo viongozi wa vyuo wanafundishwa kuwa MAFISADI? tatizo la elimu Tanzania litakwisha kweli ikiwa siasa ndiyo inayotawala katika taasisi za elimu? kwa hapo Membe amekosea na wanaharakati pamoja na wanahabari wanatakiwa kulipigania kwa nguvu zote swala hilo nyeti sana.

  Vijana ni "thinking tank of the nation". Sasa ikiwa akili zao zitakua "corrupted" na porojo za kisiasa tokea awali katika hatua za mwanzo kabisa za ukombozi wa fikra, je hii si balaa kwa taifa? MBAYA ZAIDI ni pale wanafunzi wa vyuo wanapopoteza muda wao wa kujisomea na kuanza kujadli mambo ya siasa. Ndiyo maana wanavyuo wetu watazidi kuwa maMBUMBUMBU miaka yote kwa sababu ya mitizamo waliyojengewa kuwa SIASA ndio mlango pekee wa kutokea na kufanikiwa kimaisha, hivyo kwa nini tushangae sasa kuona vijana wetu wakikimbilia siasa? MEMBE AMEKOSEA NA AFIKIRIE MARA MBILI KABLA YA KUAMUA

  Enzi zangu nilipokua nasoma chuo kikuu pale Mlimani miaka ya 90 mwanzoni, elimu yetu haikuchanganywa na siasa hata kidogo, na mpaka nimekwenda nchi za magharibi hawana "longolongo" kama hawa wanasiasa wa bongo. Kule ni vitendo zaidi na wanafunzi wanajielewa na hawataki kurubuniwa. kwani kama Membe anawapenda sana wanafunzi basi si angejikita katika utatuzi wa TATIZO LA MIKOPO ELIMU YA JUU kwa kutumia uzoefu wake wa Mambo ya nje? si angechukua mifano hiyo?, nawaomba sana wanahabari msipuuze ujumbe huu ili jamii iweze kuelewa ukiritimba anaotaka kuufanya. Kwa nini tuwe wazalishaji wa MAJANGA kila siku badala ya NEEMA? Mara utasikia DOWANS, RICHMOND, NISHATI NA MADINI nk sasa ni kuzaa BALAA LA SIASA VYUONI? Tusikubali hata chembe. Pia wadogo zangu vyuoni acheni kuwa wafuasi wa wanasiasa ,igeni mifano ya wasomi wenzenu katika nchi zilizoendelea wanavyofanya. Vinginevyo yatatokea yale ya SOMALIA, SYRIA, LIBYA, JORDAN nk.

  Chuo kikuu Dodoma (UDOM) kila siku migogoro, ni nani asiyejua kuwa chanzo chake ni siasa? Taratibu turuhusu ujinga huu kupenyeza kwa vyuo vingine vinavyotegemewa sana nchini kama Mzumbe na SUA (Sokoine University of Agriculture)?? Membe awaache hawa vijana wajisomee, wamechakachua UDOM sasa yatosha . Vinginevyo vijana wakigundua hizi hila za wanasiasa kuwa ndiyo chanzo cha wao kutofanikiwa naamini kabisa kuwa WORLD WAR III itaanzia Tanzania. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki wanafunzi wa vyuo vikuu.

  NB....wanahabari mnaweza mkaichapa hii habari kwenye magazeti ama mkaihariri kwa kutumia upeo na taaluma zenu..
   
 2. bona

  bona JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  napata wasiwasi na iyo degree yako, yaani kila waziri au kiongozi wa serikali anayezungumza na kundi la watu fulani kwenye jamii ni kutafuta urais? kwa iyo kwa sasa kila kiongozi wa serikali ajifungie tu ofisini kwake kuogopa akizungumza na watu atakua anaonekana anatafuta urais, mzee pamoja na harakatu za watu kutafurta uraus issue za maendeleo lazima ziendelee!
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,819
  Likes Received: 36,932
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli basi anapoteza muda na pesa yake bure, ktk vyuo vikuu mwana-CCM yeyote ni kituko.
   
 4. g

  gotolove Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tupo ktk kipindi cha majaribu, tuweke jazba pembeni kisha tutafakari ili tufanye maamuzi sahihi na dunia itambue CHADEMA ni chama makini." BY Mh. Freeman MBOWE.

  Kazeni buti kama TMK wanaume family aka Mheshimiwa Temba, mtafika tu magogoni. Nchi yenyewe imeshauzwa hii, bado kusafirishwa kama walivyosafirishwa Twiga wetu kupitia KIA. Jiulize sasa, usalama wa taifa, uhamiaji, polisi wako pale, Hawakuona hao twiga wakitoroshwa? Au walipewa miongozo na mkubwa wa nchi wakatulia. Maige we iba tu kama na mkubwa mwenyewe amelala usingizi wa pono utafanyaje we mtoto mdogo? Kuleni vichwa mawaziri, msilale, nafasi ndio hii. Ila wakiingia hao Magwanda nina mashaka kama wizi huu utaendelea. Kila kukicha mara mishahara hewa, mara ubadhirifu. Siku hizi mpaka vyuo vikuu kwa wasomi nako wezi.
   
 5. g

  gotolove Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila mtoa mada usitupotoshe, UDOM chanzo ni shotiii, sio siasa. Siku akiondoka yule utasikia pale kama kutakuwa na vurugu yeyote. Shotiii wa UDOM noma, usipime.
   
 6. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,459
  Trophy Points: 280
  kama ni kweli nahisi anapoteza muda yan hawezi kupata hata nafasi ya kuwa mgombea mwenza hahaha.
  Yani hata nguvu ya kufanikisha alitakalo si kwenye cchama tu hata kwa watanzania ana influence yoyote
   
 7. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Kikwete ameleta balaa Tanzania. Kila mtu sasa anawaza urais na anajiona ana uwezo wa kuongoza. Laiti Mkapa angetumia ubongo wake kufikiri akatumia mbinu za medani kumwengua leo hii watu wangekuwa wanafikiri namna nyingine..
   
 8. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Sio lazima uonyeshe ''hekima'' yako kila mahali.....
   
 9. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,042
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Natofautiana na wewe. Siasa na vyuo ni kitu kimoja enzi zile ilikua uwezijiunga na chuo mpaka uwe na kadi ya magamba. We umejuaje kama anaenda kufanya kampeni. Mbona lowasa anaenda kanisani utumii nguvu kubwa hivyo au kwa sababu kambi yako ? Mtafutieni lingine hilo mmechemka
   
 10. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  We Ngoja akipita kamanda Lema huko atamaliza kila kitu, fedha nyie chukueni lakini akili mkichwa. Hatudanganyiki ng'oooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo. Raisi gani hata kuongea hajui, yahani tutakuwa tunatoa gogo tunaingiza kuni.
   
Loading...