AGAPE TELEVISION "mizinguo"

AGAPE TELEVISION "mizinguo"

Ziroseventytwo

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
9,375
Reaction score
17,699
WanaJF, Mimi nasikitishwa na hii television ya ATN. Kwanza kabisa ile ni chanel ya mambo ya dini,lakini kwa tamaa yao ya pesa wamebidi waingie mikataba ya kishetani,kwa mfano wanapoomba kuonyesha mashindano makubwa kama Uefa champions league,mashindano ambayo yanadhaminiwa na kampuni ya kutengeneza pombe hii manake nn? Mimi naamini kabisa shughuli zote za michezo na burudani ni vitengo vya shetani. Pili, wanacho niuzi zaidi wamekuja na kingamuzi chao wanachokiita "TING' Wanatunyima haki ya ligi ya mabingwa ulaya,mpaka uwe na kingamuzi chao,ambapo hawana mtandao kwa mikoani. Huku ni kutunyima haki na kama wameshindwa wauze haki zao za kuonyesha ligi hiyo kwa chanel nyingine.
 
Nyakati za Mwisho watu watakuwa wenye kupenda pesa kuliko

Ufalme wa mbinguni utatekwa na wenye pesa (mmmmh sijui kama nimekumbuka vizuri hapa yale mahubiri ya Jumapili ileeeee)
 
Mimi siipati kwenye satelite dish kama wiki hivi sijui ndio wamebadilisetting au ni lazima kwenda kwa TING sasa???
 
Mimi siipati kwenye satelite dish kama wiki hivi sijui ndio wamebadilisetting au ni lazima kwenda kwa TING sasa???

mkuu hawa jamaa hawapatikani kwenye setelite dish, mpaka uwe na kingamuzi. Mimi nipo mkoani juzi na jana cjaona ligi ya mabingwa. Sasa hii ndo nini?
 
Nadhan UBC wanaonyesha kama unaweza kuwapata kwenye dish kubwa maana mie huwa nawapata kwenye king'amuzi cha Star times.
 
kwenda kwa TING sasa?​

  • us.jpg
 
Mbona tunawapata sisi acha lonolongo wewe uliza sisi hackers wa kimataifa tunaingia kwenye mitandao ya ccm. Cia nin ting ulia kupe mavituzi
 
wakikuombeni changizo la fedha ili walipane posha za kujikimu na bili za umeme na hata kununua mitambo mnakuwa mabahiri, kisha unataka uone bure. Hata mbinguni wavivu wapenda vya bure hawatakiwi
 
Mimi siipati kwenye satelite dish kama wiki hivi sijui ndio wamebadilisetting au ni lazima kwenda kwa TING sasa???
Wamehama kutoka Intelsat 64e na kwenda Eutelsat hivyo kuwapata lazima uwe na king'amuzi au uwe na decoder MPG4 mana hata mimi siwapati mana nina decorder MPG2.
 
Uongozi wa agape television network lazima wawe makini kwenye matangazo yao.wametoa namba nyingi sana za simu kwa ajili ya wale watu wanaohitaji vingamuzi lakini cha kushangaza nikipiga zile simu hazipatikani,mpaka sasa sijui ninunue wapi hicho kingamuzi chao
 
Back
Top Bottom