Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,494
- 113,590
Wanabodi,
Nchi zote zinazoheshimu katiba, zinaendeshwa kwa mujibu Katiba, sheria, taratibu na kanuni na sio kwa kauli za viongozi tuu ambazo kauli nyingine zinakwenda kinyume cha katiba, sheria, taratibu na kanuni!.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndie mkuu wa nchi, head of state, ndie mkuu wa serikali, Head of the Government, Mkuu wa Mhimili wa the Executive na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama , ambaye pía ni sehemu ya Bunge kwa kulizindua, kulivunja, na kuidhinisha miswada kuwa sheria na kuteua mtendaji mkuu wa Bunge, (Katibu wa Bunge), na pia rais ni sehemu ya mahakama kwa kumteua Jaji Mkuu, Mkuu wa Mhimili wa Mahakama, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, kuteua Majaji, kuidhinisha adhabu ya kifo na kutoa msamaha kwa wafungwa. Rais kama Mwenyekiti wa Chama Tawala, ndie hupitisha jina la Spika na majina ya wabunge wote watakaokuwa mawaziri.
Hivyo kwa muundo huu, rais wa JMT ndio kila kitu. Hii inamfanya rais kila agizo analolitoa lihesabiwe kama amri ni sheria, atakayekiuka anatumbuliwa!.
Serikali inaendeshwa kwa mujibu wa kitu kinachoitwa "Government Standing Orders" lakini sasa tunashuhudia baadhi ya standing orders zikiwekwa pending na badala yake sasa serikali yetu inaendeshwa kwa kauli za viongozi!.
Kikatiba, kisheria, kitaratibu na kikanuni, sio kila maagizo ya rais ni sheria kiasi cha kupelekea kila anayekwenda kinyume cha maagizo ya rais anahesabiwa amefanya kosa la insubordination ambayo adhabu yake ni summary dismissal kwa kuwa condemned unheard.
Ili kauli ya rais iwe ni sheria, kauli hiyo ikiishatolewa lazima ifuatiwe na maandishi, au a Presidential Decree ambayo ndio amri rasmi ya kiRaisi kuhusu jambo lolote ambalo rais ameliagiza, hiyo predidential decree inapata nguvu ya kisheria baada ya kuchapishwa kwenye gazeti la serikali, Government Gazzette, hivyo atakayekiuka agizo hilo itampasa hukumu.
Hata lile tangazo la kufuta maandimisho sherehe za uhuru, kiukweli kabisa, mwanzo lilotolewa kienyeji enyeji!, baada ya sisi kulipigia kelele humu, Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'! ndipo ikulu wakatoa a decree na kui back date!, hivyo agizo hilo lilifuatiwa na maandishi huku yakieleza ni kwa mujibu wa mamlaka gani, sheria gani, kifungu gani, taratibu gani na kanuni gani au a presidential decree.
Tangazo la taasisi za umma kuhifadhi fedha zake BOT pekee pia lilitakiwa kufuatiwa na decree ili liwe ndio sheria mpya ya hifadhi ya fedha za umma. Sikumbuki kuona deceee yoyote ya rais kwenye hili!
Kwa mujibu wa Gavana wa BOT, Prof.Benno Ndulu sio makosa kwa taasisi za umma kuweka fedha kwenye Fixed Deposit
https://www.jamiiforums.com/threads/gavana-bot-kufungua-akaunti-maalum-si-kosa hivyo kama rais ameitumbua bodi ya TRA kwa kosa la kukiuka maagizo yake, ametumia his appointment powers to hire and fire as he pleases lakini bodi hiyo haina kosa lolote kisheria kufungua hiyo FDA.
Kwa vile all banking transactions zinafanywa transparently na all the records ziko in black and white, kama kuna wakuu wowote waliozipiga fedha za FDA then wachukuliwe kama majizi mengine yoyote na wizi ni kosa la jinai halina limitation of time, hivyo wahusika watafutwe na kushitakiwa regardless walifanya wizi huo lini, lakini kama bodi ya TRA ilifanya kwa nía njema, tangazo la rais la sababu za kuivunja bodi ya TRA ni udhalilishaji kwa waliokuwa wajumbe wa bodi hiyo kuonekana kuwa kumbe walitaka kutuibia akiwemo Gavana Ndulu. Ningekuwa mimi kesho yake tuu angeikuta barua yangu mezani kwake.
Presidential powers to appoint hazimtaki rais kutoa sababu zozote kwanini amemteua fulani na akiamua kumtengua uteuzi halazimishwi kutoa sababu zozote kwa nini amemtengua fulani kwa sababu teuzi na tengua, zinafanyika at his pleasures, sasa kama raus aliamua kutosema sababu siku alipoamua kutengua, alipaswa asiseme kabisa hizo sababu forever na sio leo anatengua hasemi sababu halafu kesho anasema sababu, huku ni kuwadhalilisha watenguliwa kwa kila anayetenguliwa kuonekana ni jipu!, hii inconsistency is not good for presidential institutions kwa vile rais ni taasisi anaoaswa afanye mambo ki taasisi na sio kiutashi, na akifanya maamuzi ya kiutashi yafuatiwe na kutaasishwa ili yawe ya kitaasisi.
Hata rais aliposema atafuta mishahara ya peponi, watu tulisema humu, Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote
Hili swali nililo muuliza rais Magufuli pale ikulu, ile November 4, Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli ni swali very valid!. Japo rais alipiga chenga kulijibu, ilipaswa wasaidizi wake waje wamjibie siku za usoni, baadhi ya hizi amri za rais zinazokwenda kinyume cha katiba, rais Magufuli anazitoa kwa mamlaka gani kwenye kifungu gani na sheria gani?. Akitoa amri yoyote ambayo haipo kikatiba, kisheria, kitaratibu na kikanuni, atoe a presidential decree to support it!.
Najua rais wetu Mhe. Dr John Pombe Joseph Magufuli anayafanya haya yote kwa nía njema, in good faith ila katika kuyafanya haya lazima azingatie katiba, sheria, taratibu na kanuni na pia sio tuu kwa kufanya the right thing at the right time, but he got to do it right.
Paskali