Kila mtu akianza mambo ya sisi kabila letu ni hivi hatutafika, kwani haramu kwenye kabila lenu yaweza kuwa halali kwenye kabila letu vile vile halali kwenye kabila letu yaweza kuwa haramu kwenye kabila lenu. Kuongea wakati mtu mwingine anaongea awe mkubwa au mdogo awe na cheo au asiwe nacho awe mwanamke au awe mwanaume haifai, kwani huondoa usikivu. Hii hutokea pale mzungumzaji anayeongea kutosikika vizuri au kuzungumza kitu tofauti na matarajio ya watu au aliyezungumza kabla kukatishwa kabla ya kumaliza maelezo yake hivyo mzungumzaji aliyekatishwa kuendeleza maelezo ili angalau walioko jirani waelewe ulichomaanisha au ulichotaka kuzungumza hasa pale akihisi kutopata muda mwingine wa kujadili au kueleza jambo hilo.Na mtu kuongea wakati mtu mwingine anaongea ni jambo la kupitiwa tu ambalo karibu watu wengi hilo kama ni kosa tumewahi kulifanya wala isichukuliwe kwamba ni utovu wa nidhamu, ndiyo maana Halima hakuhamaki alipoambiwa hivyo, alicheka tu kwani alijua amepitiwa tu.
Cha msingi; kila mtu ajaribu kuzuia hisia zake hasa unapokuwa unaongea na watu kwani hakuna asiye na hasira.Jaribuni kutumia maneno yasiyo makali lakini ujumbe ufike.Mfano mwanasheria angesema" Halima nasubiri umalize kuzungumza ili niendelee kuongea" unadhani Halima asingenyamaza!