SoC02 Afya ya Akili na Malezi

Stories of Change - 2022 Competition

Peace21

New Member
Sep 7, 2022
1
0
SOC AFYA YA AKILI NA MALEZI

Katika maisha yote tulio ishi hapa duniani tumekuwa tukiamini kwamba hakuna kitu kinachotokea chenyewe lazima kuna kuna hatua amabyo huleta matokeo fula yawe mazuri au mabaya.Usemi huu wa ukiona vyaelea ujue vimeundwa huleta maana kwasababu mtu kuwa vile alivyo ni matokeo ya hatua fulani ambayo imemfanya awe hivyo alivyo na kuna mambo mengi sana ambayo humtengeneza mtu kuwa vile alivyo ikiwepo elimu, chakula, jamii mtu anayoishi na mazingira yake kwa ujumla. Sababu nyingi za kimazingira mwanadamu anauwezo wa kujitengenezea matokeo chanya au hasi. Afya ya akili pia ni moja ya kitu ambacho kinaweza kutengezwa au kuharibiwa na hutegemea hatua fulani na muda ili kuifanya iwe vile ilivyo.

Afya ya akili ni ya muhumi sana kwa binadam kama inavyoaminika kuwa afya ni mali hujumua sha afya ya akili pia. Moja ya kitu amabacho huchangia kutengeneza afya ya akili ya mtu ni malezi. Husaulika na watu wengi na mara nyingi umuhimu wake hauonekani wala kutotambulika na jamaii zetu ni kwasababu hakuna mtu anaechagua azaliwe wapi, azaliwe na nani na alelewe na nani ni kitu amabacho kiko nje ya matakwa yetu.

Mjadala huu unatuleta tufahamu zaidi nini maana ya malezi na ni nini maana ya afya ya akili?
Na jinsi gani vinaweza kuhusiana. malezi ya mtoto ni mchakato wa maandalizi ya mtoto utakaomuwezesha kukua, kukubarika na kushiriki katika shughuli za jamii na kiutamaduni kwa kumlinda, kumjamiisha na kumpatia huduma za msigi. Afya ya akili ni hali ya kuwa sawa kihisia, kiakili na kisaikilojia. Ina tufanya tufikiri vile tunavyofikiri na jinsi tunavyo kabiliana na mabadiliko katika mazingira yetu.

Safari ya malezi ya mtoto huanzia akiwa tumboni kwa mama. Wakati huu ni wa muhimu sana kwa mtoto kwasababu viungo vya mwili kama ubogo na uti wa mgongo vinakuwa katika hatua ya utengenezaja wake hivyo ni muhimu mama awe kaka hali mazingira mazuri yatakayo wezesha hatua hii iende sawasawa. Mtoto anakuwa na uwezo wa kutambua mabadiliko ya kimazingira na yakihisia ya mama yake anakuwa na uwezo wa kutambua furaha na uzuni.

Mama anapokuwa na msongo wa muda mrefu unaweza kumsababisha mtoto kuzaliwa kabla ya muda na akiwa na uzito mdogo sana. Mtoto aliyezaliwa kabla ya muda anaweza kupata changamoto katika kujifunza na maranyingi huchelewa kuanza kuongea na mzazi asipojua sababu mtoto anaweza kuitwa mjinga kwasababu anashindwa kuwa sawa na watoto wa rika lakinu kumbe ni matokea ya changamoto ya malezi alipokuwa tumboni. Tafiti zinaonyesha mtoto anauwezo wa kukumbuka sauti na melodi za mziki alizosikia mara kwa mara akiwa tumboni hivyo mtoto uweza kuanza kujifunza akiwa bado yuko tumboni hivyo mimba inayolelewa katika upendo na kujaliwa humfanya mtoto kuhisi yuko katika mazingira salama ndio aana wazazi ushauliwa kuanza kuongea na watoto wao wakiwa bado wako tumboni ili waweze kuisi upendo wa wazazi wakiwa bado tumboni.

Watoto walionusurika kutole wakati wa mimba wanaweza kupata madhara au kuonyeasha matatizo ya kitabia wakiwa wakubwa kwa kusumbuliwa na hisia za kuona awaitajiau awapendwi na wazazi au walezi wao, hisia za kujiua na hata kutaka kujiua, kuwa na hisia kuwa kuna kitu wamepungukiwa bila wao kuelewa hivi vyote vinatokea wapi na kama mzazi au watu wakaribu hawana ufahamu wa saikolojia si rahisi kujua chanzo cha haya matatizo .

Baada ya mtoto kuzaliwa safari ya malezi uendelea na wakati huu upitia hatua kuu tatu ambazo akiwa na umri katika ya na miaka 0 mpaka miaka 5 mtoto anakuwa tayari kujifunza na ubongo wake unazidi kukuwa pale unapokuwa ukitumika anapopata kuyaelewa mazingira yale ikiwemo kuzungumza, kuelewa kuhusu hisia zake nazawatu waliomzunguka na pia anakuwa anapenda kujifunza vitu vipya.

Na moja ya kitu kikubwa kwa mtoto kujifunza katika umri huuu ni mahusiano kwasababu yanamsaidia yeye kuelewa Zaidi mazingira yake kwa mfano mazingira salama yanafananaje ,inamaanisha nini kupendwa, ni nani anaempenda na nini utokea pale anapocheka au anapolia. Kama wazazi watashindwa kumsaidia mtoto kuelewa kuhusu mahusiano inaweza kumletea shida baadae anapoanza kwenda shule na hata ukubwani kwa kuonyesha kuto kujiamini na kushindwa kuamini watu. Anapofika miaka mitano mtoto anakuwa tayali kuanza darasa la awali na baadhi ya watoto wanaweza kuonyesha wasiwasi mkubwa wanapotenganishwa na wazazi wao na inatokea kwa namna tofauti kwa kila mtoto na kabiliana na iyo hali tofauti kutokana na msaada unatoka kwa mzazi na mwalimu.

Mtoto anapokuwa miaka 6 mpaka 12 ni umri wa kuwa shule uwezo wakutengeneza mahusiano humsaidia kukabiliana mazingira ya shule kwa kuweza kujiamini na kufanya mambo yake mwenyewe bila usimamizi mkubwa ila wazazi wanatakiwa kuwa na mfumo mzuri kwa kumuadabisha mtoto wao pale anapokosea bila kuharibu kujiamini kwa mtoto na pia ni vizuri kwa wazazi kumsifia mtot pale anapofanya vizuri. Ikitokea mtoto anapewa adhabu kubwa sana mara kwa mara bila pongezi pale anapofanya vizuri huaribu kujiamini kwakwe na kumfanya mtoto kushindwa kutambua sauti yake juu ya mambo tofauti tofauti na wakati mwingine wanaweza kutafsiri kuwa awapendwi na kuhisi kuwa wazazi awawajali na kwa wazazi wengi wa kitanzania wanaamini adhabu pekee hutatua matatizo ya kitabia ya watoto.

Muda wa muhimu sana kwa mtoto ni pale anapoelekea hatua ya utu uzima ambayo ujulikana kama balehe wakati huu hleta matatizo makubwa kwa watoto, wazazi na famiia kwa ujumla na kama mzazi hana ufahamu mkubwa kuhusu wakati huu uweza kuleta migogoro mikubwa kati ya wazazi na mtoto lakini mzazi akiweza kuutumia vizuri unaweza kutengeneza urafiki mkubwa kati ya mzazi na mtoto.

Changamoto kubwa mtoto ukutana nayo mabadiliko ya kimwili na mara nyingi watoto wa kiume upend asana kutendeneza mahusiano na watu wa rika lake wa wa nje ya familia. Mara nyingi shida tokea kwasababu mzazi anatakwa awena na nafasi ya kuongoza maisha ya mwamae kama alivyokuwa mdogo lakini mtoto huaitaji uhuru zaidi. Mzazi anatakiwa kumuacha awe huru na kumuweka karibu ili aweze kumsaidia na changamoto za balehe na mttoto aweze kuona sehemu salama ambayo anaweza kupata majibu ya maswali yake ni kwa mzazi wake na si kwa mtu mwingine yeyeto.

Mahusiano yakiwa mazuri wazazi wataweza kusaidia kupunguza matumizi ya madawa ya kulevya katika jamii zetu, mimba za utotoni, na itasaidia kutengeneza mzazi mwingine bora wa baadae na kila mtu katika jamii atakuwa na afya bora ya akili.
 
Back
Top Bottom