SoC01 Afya ya Akili: Mambo 12 ya kuyafahamu

Stories of Change - 2021 Competition

dom1

New Member
Jul 15, 2021
3
11
Maana ya afya ya akili kisaikolojia:

Afya ya akili ni ustawi wa fikra, tabia na hisia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku katika maisha ya mwanadamu.Wakati mwingine watu hutumia neno ''afya ya akili'' kumaanisha kutokuwepo kwa shida ya akili ( retrieved on 16/07/2021 through Medicalnewstoday.com).

Umuhimu wa kuifahamu Afya ya Akili:

Moja, kuweza kutambua changamoto ndogondogo ambazo zaweza kupelekea tatizo la akili,mfano ,msongo wa mawazo usipopatiwa ufumbuzi hupelekea tatizo la akili liitwalo Sonona.

Pili, Kuitambua afya ya akili kunasaidia kupambana na shida ya kiwewe(Post traumamatic stress problem) inayosababishwa na majanga mbalimbali. Hapa namaanisha majanga mfano mtu anapopatwa na majanga katika maisha, mfano mtu anapofiwa na mpendwa au mtu wake wa karibu hupatwa na kiwewe kiakili ambapo asipopatiwa msaada wa Kisaikolojia humpelekea kupatwa na tatizo la akili na hatimaye ugonjwa wa akili. Ukiona mtu barabarani anaokota makaratasi au amechanganikiwa ujue tatizo lilianza dogo, waswahili husema ''hata mbuyu ulianza kama mchicha''.

Tatu, Kuifahamu afya ya akili husaidia kujua namna ya kuitunza afya ya akili.Mtu mwenye ufahamu kuhusu afya ya akili itamsaidia kujua namna ya kuitunza afya yake ya akili, mfano, mtu atajua umuhimu wa kulala kwa ratiba ya kuweleka kuliko kulala bila mpangilio ambapo hupelekea kuathiri ustawi wa akili, binadamdu anatakiwa alale kuanzia masaa 6-8 ili kuisaidia akili kua imara. Mtu akishindwa masaa ya kutosha hupelea mlundikano wa sumu mwilini na pia kupelekea baadae tatizo la akili kama vile ugonjw wa kusahau (insomnia), pia itampelekea mtu kujua umuhimu wa mlo kamili na umuhimu wa mazoezi ya mara kwa mara kwa ustawi wa afya ya akili.

Nne, kuifahamu afya ya akili kutasaidia watu kuepuka migogoro katika maisha. Migogoro hupelekea mtu kua na hasira na kinyongo ambapo hupelekea magonjwa ya mshtuko wa moyo,magonjwa ya moyo na kiharusi. Mfano migogoro katika ndoa na sehemu za kazi.

Tano, Kuifahamu afya ya akili huleta furaha,upendo na amani ya nafsi. Mtu anayeifahamu afya ya akili humsaidia kepuka vitu vinavyomuondolea furaha,upendo na amani,nfano,Hasira,migogoro na chuki.

Sita, Kuifahamu afya ya akili kutapelekea mtu kujua ni wakati gani mtu anahitaji msaada wa kisaikolojia. Ni rahisi mtu anayefahamu afya ya akili kujijua kuwa wakati ambapo kiakili hayupo sawa kuitafuta huduma ya kisaikolojia mfano wataalamu wa Ushauri nasaha na Unasihi, wataalamu wa Saikolojia tiba(Clinical Psychologist) ili kuirejesha afya yake ya akili katika hali yake ya kawaida.

Saba, Uelewa wa afya ya akili husaidia malezi mazuri ya watoto. Familia yenye uelewa mzuri wa afya ya akili kutasaidia watoto kulelewa vizuri na wazazi wao kiakili na kimwili, mfano kutambua tabia za watoto, kuwapa watoto uhuru wa kuchezakujieleza, kujifunza, kuwapa upendo, kuvitambua na kuviendeleza vipaji vya watoto, kuwajengea watoto uwezo wa kujieleza na kujiamini, kuwajengea uwezo wa kujitambua, kujikubali na kuthamini uwezo wao.

Nane, Kuifahamu afya ya akili kutapeleakea kutambua na kuwasaidia watoto wanaozaliwa na matatizo ya kisaikolojia.Uelewa wa afya ya akili kutapelekea wazazi kutambua na kuwasaidia watoto wenye matatizo ya kisaikolojia, mfano tatizo la Usonji (Autism) na tatizo la kuvia akili(slow learning ability). Hapa itawasaidia wazazi wenye uelewa wa afya ya akili kutafuta mtaalamu wa Saikolojia ya watoto(Child Psychologist).

Tisa, Uelewa wa afya ya akili utasaidia kupunguza matatizo ya kikatili na uzalilishaji ndani ya jamii. Elimu ya afya ya akili inasaidia kuwasaidia wanajamii wote kulinda afya zao za akili na za wenzao baada ya kujua madhara ya kuwafanyia wengine masuala ya ukatili na uzaliloshaji ambayo yatapelekae kuharibu afya zao za akili na za wengine kwa ujumla,mfano ubakaji,ulawiti,rushwa za ngono na uzalilishaji wa kujinsia.

Kumi, uelewa juu ya afya ya akili husaidia kuondoa tatizo la watu kijiua na kijidhuru. Elimu ya afya ya akili hupelekea kuondoa tatizo la watu kujiua na kidhuru nafsi zao. Jamii nyingi hupoteza watu wao kutokana na matatzi ya kisaikolojia mfano sonona.

Kumi na moja, Elimu ya afya ya akili husaidia kuwapa wanajamii mbinu mbadala za kupambana na matazo ya msongo wa mawazo. Mbinu na mafunzo ya kupambana na matatizo ya msongo wa mawazo hutolewa na wanasaikolojia walobobea katika taaluma ya Saikolojia.

Kumi na mbili, Elimu ya afya ya akili husaidia wanafunzi shuleni kua na tabia njema. Kila shule nchini zinatakiwa iwe na Mwanasaikolojia angalau mmoja ili kuwasaidia wanafunzi kupata mafunzo na muongozo kuhusu afya ya akili na tabia zao kwa ujumal ili kulinda tabia zao na akili zao. Mfano, wanafunzi kujiepusha kjiingiza katika mahusiano mapenzi ya mapema, kuepuka mimba za ututoni,kujiepusha na tabia za madawa ya kulevyan na magonjwa ya kuambukiza kama vile janga la UKIMWI na janga la ugonjwa wa UVIKO (COVID-19).

Hitimisho:
Elimu ya afya ya akili ni muhimu sana ili kuongeza uzalishaji mali, umakini katika kazi, furaha, amani na upendo katika jamii.
 
Mawazo mazuri hasa hilo la 12

Mkuu walimu wa masomo ya kawaida kabisa ya darasani hawatoshi leo uje na wazo la walimu wa saikolojia shuleni kweli?

Tatizo la afya ya akili acha tujitibu kwa miti shamba na mizizi kila mtu kwa nafasi yake

Serikali iongeze walimu shuleni na kuboresha maslai yao na kuwatambua walimu kwa Elimu zao yaani astashahada, stashahada, shahada, uzamili na uzamivu

Haya yakifanyika kwa ufasaha afya ya akili itakuja yenyewe maana hata mojawapo ya tatizo la afya ya akili ni msongo wa mawazo wanaopata walimu kwa kuzidiwa na kazi za WANAFUNZI na kutotambuliwa Elimu zao (added advantage)
 
Uzi mzur Sana tatizo mtiririko wa idea zinajirudia kiusanifu..

Lkn afya ya akili ni muhimu San kitandani
 
Back
Top Bottom