SoC02 Afya katika maendeleo ya Tanzania 🇹🇿

Stories of Change - 2022 Competition

kennedy nkya

New Member
Aug 8, 2022
2
4
AFYA: Ni hali ya kujisikia vizuri kimwili kiakili na kiutu bila kusubuliwa na kitu chochote. Pia afya inaeza kuelezewa kwa hali ya ubora wa kiumbe hai kuweza kufanya vizuri katika mazingira yake, Vilevile shirika la afya ulmwenguni(WHO) limeelezea afya kwa maana ya kuunganishwa na hali ya ustawi wa mwili,kiakili na kijamii na sio tu ukosefu wa magonjwa. Neno afya limetokana na neno la kilatini “SALUTIS’ ambalo linamaanisha wokovu lakini pia salamu kwa hiyo kitenzi cha kusalimu kinamaanisha afya nyingine. Afya imekuwa ni mojawapo ya kitu kinachomsaidia mwanadamu katika shughuli zake. Afya imekuwa ikiathiriwa na mambo mbali mbali katika mwili wa binadamu sababu hizo ni kama zifuatazo;

Mazingira: Mazingira yamekuwa mojawapo ya changamoto zinazoathiri afya ya binadamu kwa namna moja ama nyingine. Ikiwemo watu wanao ishi karibu na viwandani huwa waathirika kiafya kupitia makelele ya viwandani pia moshi unaotoka viwandani umekuwa ukidhorotesha afya za wanadamu pia kwa wale wanaokaaa karibu na sehemu za takataka wanaathirika pia katika kipindi cha mvua na pia harufu za maeneo ya karibu na hapo huwa sio rafiki na hao.

Mtindo wa maisha: Mtindo wa maisha umekuwa mojawapo ya changamoto kubwa sana wa kuathiri afya za binadamu hii ikiwemo unywaji wa vitu vya ngano na sukari kwa wingi, ambavyo vimechangia udhoroteshaji wa afya pia hali ya uzingatiaji wa mazoezi umekuwa changamoto kwa baadhi ya bindamu ambayo imepelekea udhoroteshaji wa afya zao.

Afya ya uzazi: Afya ya uzazi inahusisha ufikiaji wa haki za kijinsia kwa wanawaake na wanaume ambayo inamanisha kuwa wana uwezo wa kufurahia maisha ya ngono ya kuridhisha bila hatari ya magonjwa pamoja na uchaguzi wa bure katika afya yao.

Afya ya kimwili: Inamaanisha mazingira ya kimwili na utendaji wa miili yao. Mtu mwenye afya bora ya kimwili anaweza kujumuika vizuri katika jamii kukuza uwezo wao na kuchangia ustawi wa jamii kwa ujumla. Ushawishi wa sababu za kibaolojia, mazingira na kijamii zina athari kwa afya ya mwili lakini mtindo wa maisha pia una jukumu la msingi.

Afya ya kiakili: Ni hali ya usawa na ustawi wa kiakili, kihemko na kijamii ambao mtu anafahamu uwezo wake na anaweza kukabiliana na mahitaji ya kawaida ya maisha na kuwa na tija kwa jamii. Afya ya kiakili inahusu hisia, hisia za mtazamo na tabia za mtu na uhusiano wake kwa jamii. Kujiona huru na ustawi binafsi jinsi mtu anafikiria anavoishi, yana ushawishi moja kwa moja kwenye afya ya akili.

Afya ya binadamu inaweza kuaribiwa kwa njia mbali mbali ikiwemo, Matumizi mabaya ya dawa za kulevya: Madawa ya kulevya ni kemikali ambazo zingiazo mwilini na kuathiri ubongo wa mtumiaji na kumsababishia kuwa na matendo, hisia, fikra na muoekano tofauti na matarajio kamili. Kemikali izi hutokana na mimea na madini ambayo ni mali ghafi muhimu kwa mahitaji mengine ya mwanadamu. Dawa za kulevya ni kama tumbaku, pombe, bangi, mrungi na coccine ambazo zikitumika na binadamu znapelekea binadamu kuathirika vibaya ubongo wake.

Pia njia nyingine inayo athiri afya ya binadamu ni vidudu toka katika taka za binadamu: Vidudu hivi hueneza magonjwa kwa watu kupitia maji ya kunywa yaliochafuliwa, chakula kilichovunwa katika mchanga uliochafuliwa, dagaa zilizovunwa kutoka katika maji machafu, kuoga na kurudi katika maji machafu ambayo hupelekea magonjwa kama salmonella ya bakteria, girdia ya vimelea vya wadudu wa udongo.

Pia athari nyingine ni kama vimelea vya magonjwa ya kuambukiza: Magonjwa ya kuhara, homa ya matumbo na kipindupindu, ndio wasi wasi mkubwa wa kiafya unaohusisha uchafuzi wa maji machafu na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu hii ilionekana mnamo mwaka 2017 takribani watu million 1 walifariki kwa magonjwa hayo. Pia vimelea vya wadudu kwenye chanza cha samagamba husababisha ugonjwa wa hepatitis A na E kila mwaka pia gonjwa la uviko-19 limekuwa gonjwa kubwa la kuambukiza ambalo limepoteza mamilioni ya watu duniani.

Vile vile hali ya kutozingatia uzazi wa mpango umekuwa ukiathiri afya ya binadamu hii ni sababu ya kutozingatia uzazi mzuri wa mpango. Mtu anaeza akawa na watoto wengi ambao hataeza pia kumudu kuwalisha wote na hivyo mtoto kukosa lishe hivyo basi hupelekea kuduma kwa afya yake na kupelekea kupata magonjwa kama vile “kwashakor”.

Hivyo basi baada ya kuona hayo yote ili mtu kuwa na afya bora anatakiwa azingatie yafuwatayo: Uzingatiaji wa malezi ya mwili na lishe, pia ulaji wa mlo kamili ambapo unahusisha aina tatu za matunda na mboga kwa siku, pia kula nyama za kusindikwa kwa nadra, Bila kusahau kuyapa mazoezi kipaumbele sababu yanasaidia sana katika afya ya binadamu na kusaidia katika kujenga mwili kuwa imara na kuondoa msongo wa mawazo.

Maisha bora ya kiafya huleta tofauti kwa jamii na mtu mmoja mmoja hii ikiwa na maana ya kwamba mtu anaezingatia afya bora na mlo kamili hupunguza kwa kiasi kikubwa magonjwa yasioambukizwa kama vile shinikizo la damu na kisukari.

Hivyo kwa kuona hayo yote serikali ina nafasi kubwa katika kudumisha afya ya wananchi wake kwa kujenga vituo vingi vya kiafya: Vituo vya kiafya vinapelekea kupunguza athari za kina mama kujifungulia nyumbani pia husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza athari ya magonjwa ya kuambukizwa na yasio ya kuambukizwa kwa binadamu.

Pia serikali ina dhumuni la kuanzisha taasisi ndogo zitakazo kuwa zinatoa elimu kwa jamii juu ya afya bora na mlo sahihi pia na uzazi wa mpango ili kupunguza uenezaji wa magonjwa yanayosababishwa na kukosa mlo sahihi kwa watoto na watu wazima. Pia husaidia kupunguza wimbi la magonjwa ya kuambukiza kama kipindupindu na ukimwi sambamba na janga linalokumba dunia la uviko 19.

Vile vile serikali ingeweka sheria ili kuwabana wote watakao fanya vitendo vya kuharibu mazingira ambayo ingepelekea kudhorotesha afya ya jamii ikiwemo na faini mbali mbali juu ya hao wote watakaofanya hivyo. Jambo hili litapelekea kupunguza wimbi kubwa la uchafuzi wa mazingira yetu pia uchafuzi wa vyanzo vya maji hivyo kupelekea afya bora kwa wanajamii wote.

Hivyo basi kwa kuzingatia ayo yote tutapata jamii bora na taifa lenye watu wenye nguvu na walio tayari kabisa kulitumikia taifa lao ili kujenga uchumi wa nchi yao, na kuhamasisha maisha bora kwa kila mwananchi.
By

Kennedy Nkya.​
 

Attachments

  • AFYA.docx
    20.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom