EJM_
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 3,836
- 2,093
MSHITAKIWA Rajabu Athumani (20) jana amehukumiwa kifungo cha siku 14 kwa kosa la kuonekana mahakamani akiwa amevalia kaptula chini ya makalio maarufu kama mlegezo.
Athumani ambaye alifika katika Mahakama ya Wilaya Ilala kwa ajili ya kusikiliza kesi nyingine inayomkabili ambayo kwa mujibu wa karani wa Mahakama hiyo ni ya ubakaji, alionekana akiwa amevalia hivyo huku nguo za ndani zikionekana.
Mtu kuvaa suruali chini ya makalio ikiwa sio maadili yetu na tamaduni zetu Waafrika hasa kwenye shughuli za Serikali na kuonesha nguo zake za ndani, anachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo, alisema Hakimu.
Katika hatua nyingine, Mawazo Nelson Kigalu (34) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na shitaka la kuiba tairi za behewa zenye thamani ya Sh milioni 1.5.
Mbele ya Hakimu Jannet Kinyage , Mwendesha Mashitaka Denis Muyumba alidai Desemba 13 mwaka jana muda usiojulikana usiku katika yadi ya reli katika Wilaya ya Ilala, Nelson aliiba tairi mbili za behewa zenye thamani ya Sh milion 1.5 mali ya kampuni ya reli.
Mshitakiwa alikana shitaka na kurudishwa rumande hadi Aprili 3 mwaka huu shauri hilo litakapotajwa tena.
Kaaazi kweli kweli!