Afungasha kimba kwenye shati

IrDA

JF-Expert Member
Aug 26, 2010
743
350
Kuna jamaa mmoja kutoka bara baada ya kuingia jijini Dar, siku moja katika matembezi yake aliingia katika choo cha kulipia. Kwa vile alikuwa amekula ugali wa mtama, alishusha mzigo ‘kimba’ la haja. Baada ya kujisaidia ilibidi ‘aflashi’ kimba lile lililokuwa kama mguu wa mtoto.


Lakini kila alipoliflashi kimba lilizama chini na kuibuka zima zima, kitu kilichomfanya jamaa aflashi tena, ulikuwa mchezo ule ule kwani mzigo ulizama na kuibuka.


Wakati jamaa akichanganywa na kimba lile lililoonekana bishi, nje wateja nao walikuwa kwenye hali mbaya na kuanza kupiga kelele kuomba atoke.


Jamaa alijikausha na kujaribu kwa mara nyingine lakini habari ilikuwa ile ile, kimba kuzama chini na kuibuka juu. Jamaa aliona udhia aliamua kuvua fulana aliyovaa ndani na kuchukua kimba na kulifunga kwenye fulana kisha akatoka nalo.


Mpaka jamaa anatoka alikuwa amemaliza saa nzima chooni, ilibidi mwenye choo amlipishe muda wa kufidia. Baada ya kutoka, alitafuta sehemu na kulitupa lile kimba huku akijuta kula vyakula vigumu.
 
Tusilisifie tu kimba kwa ukubwa,pia tuyasifie masaburi ya jamaa kuweza kulitoa kimba zima zima!
 
Wewe mwenyewe mtu wa bara kwan umekuwa mtu wa Pwan wewe ? Kwanza nauhakiki huyo jamaa utakuwa wewe mwenyewe unazuga tu.
 
Wewe mwenyewe mtu wa bara kwan umekuwa mtu wa Pwan wewe ? Kwanza nauhakiki huyo jamaa utakuwa wewe mwenyewe unazuga tu.

Alaa,ntake radhi mi mtu wa pwani,shangani bana...habari hizo sinaga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom