Nimewapita wakina mama pasi na salamu kwenye uchochoro, nikafumukia chooni

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Habari za asubuhi ndugu zangu wapendwa katika Bwana!

Basi bhana, jioni ya jana ikawasili, ka jua fulani hivi ka rangi ya machungwa kakatanda. Muda huo nina buku teni tu mfukoni

Si ndio kupanda daladala! Siku ya jana sijametisha aisee. Nikiwa ndani ya daladala nakutana na mrembo. Nikaona wacha nisikae kimayai mayai nikaanza kumtupia nyavu. Hiyo, akakwepa! Rusha tena, akachomoa! Mara, Vuu Pah! Imo! Binti kajikuta analopoka jina hadi namba ya simu mapeema, Maghreth! Nikajikuta napata mfadhaiko wa moyo, nikajikuta napanga bajeti upya!

Hili buku teni sasa, nauli ya watu wawili buku, nitamwachia kichangamsha damu a.k.a kivutio 3,000. Buku jero la kamnyweso, hiyo 4,500 ya meza! Issue ya sijui itatosha usiku, sijui itatosha hadi kesho mchana (yaani leo) atajiongeza juu kwa juu, hence, kesho naamka mapeeeema natokomea kusikojulikana, na simu yangu naiwekea kandege.

Muda huo tumefika katikati ya safari nashangaa kuona kiganja cha konda kimebebelea vipande vya bati, kacha! kacha! "Babu apo!" Ikabidi Maghreth anitizame kwa mara nyingine usoni, "Aahaa, kumbe ni utani wa konda", ilisikika sura yake huku ikiambatana na tabasamu

Si ndipo binti kufungua kipochi manyoya alichokuwa amekibebelea! We acha nione hiyo mirundo. Yaani ni teni teni zimepangana, kama vile anafanya kazi ofisi ya sponsa, nikajikuta namkumbuka Julieth pale UDSM miaka kadhaa iliyopita! Nikajitia umwamba nikamwambia, "Usihofu ntakulipia", akatabasamu na kusema "Ntashukuru", huku vidimpoz na tumacho goroli kama amemeza wida tukiliangaza daladala zima lililokuwa limechoshwa na mwendo, yaani limebakiza dakika chache likojoe petrol.

Baada ya kuingiza kiganja mfukoni, konda alibaki akishangaa jinsi ambavyo macho yamenitumbuka! Nikajikuta ninastand atizi attenshen, nusra nimkanyage Maghe vidole vya miguu, nikajipiga sachi ya maana, muda huo hata mkono wa kuume hauuamini mkono wa kushoto. Nikamgeukia Maghe na kusema, "Au wewe ndo umeniibia teni langu nini?", lakini kimoyomoyo.

Konda akabadili gia juu kwa juu na kumwambia mtoto mzuri! "Na wewe huna chochote kitu ili mkalale kwangu?" Binti akamtukana konda kwa kidhungu. Kisha akachomoa uteni mmoja akamwambia, "kata ya mtu mmoja". Ghafla redio ya moyo wangu ikasikika ikijitune na kuanza kushusha verse za wimbo wa Majaribu wa Bahati Bukuku, muda huo haisi linapiga wimbo wa wanangu mi mtu mbadi.

Nikajeuza shingo langu huku na huku na huko na hapo kutazama kama labda nitakutana na sura ya mzee wa busara, awapi! Wazee wa busara wenyewe ni njaa njaa tupu! Baada ya konda kumaliza sensa ndani ya daladala lake ndipo kunipandishia kibesi, na mimi nikajivika umemba wa jukwaa la siasa, alisikika mzee mmoja wa busara akisema, "konda we, kama anashindwa kuwa mpole mpige chini" Ndipo kushushwa ndani ya lile daladala

Basi bhana,
Baada ya kutupwa nje ya daladala lile chakavu kama mzigo wa dhambi, nikaona isiwe soo. Nikafungua google map, siyo kwamba njia sihifahamu, ni kwa vile tu nilitaka kujipa moyo. Nilichokigundua ni kuwa, barabara hii ina umbo la "U" ili kufika niendapo, nikaona isiwe kesi, kama nitakatisha hapa katikati kutoka kwenye ncha moja ya U kwenda nyingine itakuwa ni rahisi kulinganisha na kuizunguka U nzima

Nilipogeuka kushoto kwangu nikaona nyumba nyingi za kiswazi, nikajikuta natamka kwa sauti kuu "CHOCHO KWA CHOCHO" nikanyoosha mkono wangu wa kuume kivita, nikaamua kufuatisha kinjia ambacho kimebanwa na nyumba pande zote mbili ili nitokee kwenye ncha nyingine ya U

Dakika tano mbele, niliamua kunyenyua shati langu juu na kuibana simu yangu kwenye bokisa, hii ni baada ya kuona mazingira siyaelewi elewi vile, maake sio kwa huo moshi wa ubani wa vijana wa kileo ulivyokuwa unachochwa mithili ya zile ndege za akina Nyerere zilizokuwa zinatumia makaa ya mawe

Nilikutana na vishawashishi vingi ikiwemo mitego ya khanga moko kutoka kwa wanawake wa mitaa ile, kuna muda nilikuwa natokeza kwenye vyumba vya watu, wakati mwingine nilisikia sauti za migegedano, kuna muda nilikutana na vijana na mabinti wakichapana bakora za kiutu uzima wazi wazi. Kuna muda nilikatiza kwenye Gesti bubu na kukuta mwanamke na mwanamke wakizichapa wakiwa watupu. Yote kwa yote, hayo hayakunihusu, tuendelee na safari yetu

Baada ya kama dakika 20 hivi, nilikutana na wakina mama wakiwa nahisi ni kwenye kikundi, kipochi au kikoba. Kwa kuwa binafsi huwa ninaloose confidence ninapokutana na umati wa wanawake nikaamua kuwapita pasi na kuwasemesha chochote kitu. Walikaa kimya kwa muda wa dakika moja kisha mmoja wao alisikika akisema "Awee, usinambie", walifuatiwa na "hehe heee alooo". Nikaona potelea pote. Hapo hapo katika harakati za kuduwaa nikaskia, "Ashura mpelekee na maji kwenye ndoo, mwambie asiache kimba juu ya sink"

Nilipopinda kona kuona labda nitatokeza eneo la wazi, nikajikuta nachomozea PUTO, yaani choo cha majirani, muda huo huo maji yakanifuata, kisha kile kitoto kikatokomea. Nikajikuta natabasamu na kusahau kabisa suala zima la shida ya maji katika nchi yetu. Hapo hapo kakaja katoto ka kiume kakanambia, "Mama anauliza kuwa, au unataka kukojoa kiutu uzima?". Nikaamua kukafukuzia mbali. Sekunde chache nikasikia watu wakianguka kicheko. Dah! Nikahesabu kuanzia 9 kurudi nyuma. Baada ya hapo walishtukia tu mtu keshafika kwenye lami mahali alipoanzia safari, tayari kwa kufuata barabara ile ya lami

Nilifika nyumbani saa tatu hivi nikiwa nimechoka sana na kupokelewa na mke wangu, Mwa J na wanangu wawili
 
😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Habari za asubuhi ndugu zangu wapendwa katika Buwana

Basi bhana, jioni ya jana ikawasili, ka jua fulani hivi ka rangi ya machungwa kakatanda. Muda huo nina buku teni tu mfukoni

Si ndio kupanda daladala! Siku ya jana sijametisha aisee Nikiwa ndani ya daladala nakutana na mrembo. Nikaona wacha nisikae kimayai mayai nikaanza kumtupia nyavu. Hiyo, akakwepa! Rusha tena, akachomoa! Mara, Vuu Pah! Imo! Binti kajikuta analopoka jina hadi namba ya simu mapeema, Maghreth! Nikajikuta napata mfadhaiko wa moyo, nikajikuta napanga bajeti upya!

Hili buku teni sasa, nauli ya watu wawili buku, nitamwachia kichangamsha damu a.k.a kivutio 3,000. Buku jero la kamnyweso, hiyo 4,500 ya meza! Issue ya sijui itatosha usiku, sijui itatosha hadi kesho mchana (yaani leo) atajiongeza juu kwa juu, hence, kesho naamka mapeeeema natokomea kusikojulikana, na simu yangu naiwekea kandege

Muda huo tumefika katikati ya safari nashangaa kuona kiganja cha konda kimebebelea vipande vya bati, kacha! kacha! "Babu apo!" Ikabidi Maghreth anitizame kwa mara nyingine usoni, "Aahaa, kumbe ni utani wa konda", ilisikika sura yake huku ikiambatana na tabasamu

Si ndipo binti kufungua kipochi manyoya alichokuwa amekibebelea! We acha nione hiyo mirundo Yaani ni teni teni zimepangana, kama vile anafanya kazi ofisi ya sponsa, nikajikuta namkumbuka Julieth pale UDSM miaka kadhaa iliyopita! Nikajitia umwamba nikamwambia, "Usihofu ntakulipia", akatabasamu na kusema "Ntashukuru", huku vidimpoz na tumacho goroli kama amemeza wida tukiliangaza daladala zima lililokuwa limechoshwa na mwendo, yaani limebakiza dakika chache likojoe petrol

Baada ya kuingiza kiganja mfukoni, konda alibaki akishangaa jinsi ambavyo macho yamenitumbuka! Nikajikuta ninastand atizi attenshen, nusra nimkanyage Maghe vidole vya miguu, nikajipiga sachi ya maana, muda huo hata mkono wa kuume hauuamini mkono wa kushoto. Nikamgeukia Maghe na kusema, "Au wewe ndo umeniibia teni langu nini?", lakini kimoyomoyo

Konda akabadili gia juu kwa juu na kumwambia mtoto mzuri! "Na wewe huna chochote kitu ili mkalale kwangu?" Binti akamtukana konda kwa kidhungu. Kisha akachomoa uteni mmoja akamwambia, "kata ya mtu mmoja". Ghafla redio ya moyo wangu ikasikika ikijitune na kuanza kushusha verse za wimbo wa Majaribu wa Bahati Bukuku, muda huo haisi linapiga wimbo wa wanangu mi mtu mbadi

Nikajeuza shingo langu huku na huku na huko na hapo kutazama kama labda nitakutana na sura ya mzee wa busara, awapi! Wazee wa busara wenyewe ni njaa njaa tupu! Baada ya konda kumaliza sensa ndani ya daladala lake ndipo kunipandishia kibesi, na mimi nikajivika umemba wa jukwaa la siasa, alisikika mzee mmoja wa busara akisema, "konda we, kama anashindwa kuwa mpole mpige chini" Ndipo kushushwa ndani ya lile daladala

Na ndipo safari ya(lengo la) uzi huu linapoanzia. Narudi baadaye kidogo. We Subscribe uzi, tukutane baadaye!
Pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee😁
 
Habari za asubuhi ndugu zangu wapendwa katika Bwana!

Basi bhana, jioni ya jana ikawasili, ka jua fulani hivi ka rangi ya machungwa kakatanda. Muda huo nina buku teni tu mfukoni

Si ndio kupanda daladala! Siku ya jana sijametisha aisee. Nikiwa ndani ya daladala nakutana na mrembo. Nikaona wacha nisikae kimayai mayai nikaanza kumtupia nyavu. Hiyo, akakwepa! Rusha tena, akachomoa! Mara, Vuu Pah! Imo! Binti kajikuta analopoka jina hadi namba ya simu mapeema, Maghreth! Nikajikuta napata mfadhaiko wa moyo, nikajikuta napanga bajeti upya!

Hili buku teni sasa, nauli ya watu wawili buku, nitamwachia kichangamsha damu a.k.a kivutio 3,000. Buku jero la kamnyweso, hiyo 4,500 ya meza! Issue ya sijui itatosha usiku, sijui itatosha hadi kesho mchana (yaani leo) atajiongeza juu kwa juu, hence, kesho naamka mapeeeema natokomea kusikojulikana, na simu yangu naiwekea kandege.

Muda huo tumefika katikati ya safari nashangaa kuona kiganja cha konda kimebebelea vipande vya bati, kacha! kacha! "Babu apo!" Ikabidi Maghreth anitizame kwa mara nyingine usoni, "Aahaa, kumbe ni utani wa konda", ilisikika sura yake huku ikiambatana na tabasamu

Si ndipo binti kufungua kipochi manyoya alichokuwa amekibebelea! We acha nione hiyo mirundo. Yaani ni teni teni zimepangana, kama vile anafanya kazi ofisi ya sponsa, nikajikuta namkumbuka Julieth pale UDSM miaka kadhaa iliyopita! Nikajitia umwamba nikamwambia, "Usihofu ntakulipia", akatabasamu na kusema "Ntashukuru", huku vidimpoz na tumacho goroli kama amemeza wida tukiliangaza daladala zima lililokuwa limechoshwa na mwendo, yaani limebakiza dakika chache likojoe petrol.

Baada ya kuingiza kiganja mfukoni, konda alibaki akishangaa jinsi ambavyo macho yamenitumbuka! Nikajikuta ninastand atizi attenshen, nusra nimkanyage Maghe vidole vya miguu, nikajipiga sachi ya maana, muda huo hata mkono wa kuume hauuamini mkono wa kushoto. Nikamgeukia Maghe na kusema, "Au wewe ndo umeniibia teni langu nini?", lakini kimoyomoyo.

Konda akabadili gia juu kwa juu na kumwambia mtoto mzuri! "Na wewe huna chochote kitu ili mkalale kwangu?" Binti akamtukana konda kwa kidhungu. Kisha akachomoa uteni mmoja akamwambia, "kata ya mtu mmoja". Ghafla redio ya moyo wangu ikasikika ikijitune na kuanza kushusha verse za wimbo wa Majaribu wa Bahati Bukuku, muda huo haisi linapiga wimbo wa wanangu mi mtu mbadi.

Nikajeuza shingo langu huku na huku na huko na hapo kutazama kama labda nitakutana na sura ya mzee wa busara, awapi! Wazee wa busara wenyewe ni njaa njaa tupu! Baada ya konda kumaliza sensa ndani ya daladala lake ndipo kunipandishia kibesi, na mimi nikajivika umemba wa jukwaa la siasa, alisikika mzee mmoja wa busara akisema, "konda we, kama anashindwa kuwa mpole mpige chini" Ndipo kushushwa ndani ya lile daladala

Na ndipo safari ya(lengo la) uzi huu linapoanzia. Narudi baadaye kidogo. We Subscribe uzi, tukutane baadaye!
Dah we jamaa
 
Kwa akili zako ulidhani dada atamwambia konda kata za wawili? Ili umgande mtakaposhuka kisa umeona teni teni?

Pambana na 1200 yako.
 
Ha ha ha haaaaa... Na linapigwa goma la oya me mtu mbad....

Tuache hayo,.. hivi huku Dar kuna daladala zinakimbia kama za Gongo la Mboto Kawe au Gongo la Mboto Masaki? Maana Dah.. hao jamaa wa hizo njia wanamwaga moto sio wa nchi hii
 
πŸ˜„ wewe una alfu kumi tu unazurura nayo bila kuigawa kweli wewe sio mtu mbadi. Ukiwa na buku kumi ungetakiwa uichenji na Kila mfuko ukae chenji yake🀣🀣🀣
Hapo ungejikuta unaimba kwaya za mapambio
 
MUENDELEZO HUU HAPA:
Basi bhana,
Baada ya kutupwa nje ya daladala lile chakavu kama mzigo wa dhambi, nikaona isiwe soo. Nikafungua google map, siyo kwamba njia sihifahamu, ni kwa vile tu nilitaka kujipa moyo. Nilichokigundua ni kuwa, barabara hii ina umbo la "U" ili kufika niendapo, nikaona isiwe kesi, kama nitakatisha hapa katikati kutoka kwenye ncha moja ya U kwenda nyingine itakuwa ni rahisi kulinganisha na kuizunguka U nzima

Nilipogeuka kushoto kwangu nikaona nyumba nyingi za kiswazi, nikajikuta natamka kwa sauti kuu "CHOCHO KWA CHOCHO" nikanyoosha mkono wangu wa kuume kivita, nikaamua kufuatisha kinjia ambacho kimebanwa na nyumba pande zote mbili ili nitokee kwenye ncha nyingine ya U

Dakika tano mbele, niliamua kunyenyua shati langu juu na kuibana simu yangu kwenye bokisa, hii ni baada ya kuona mazingira siyaelewi elewi vile, maake sio kwa huo moshi wa ubani wa vijana wa kileo ulivyokuwa unachochwa mithili ya zile ndege za akina Nyerere zilizokuwa zinatumia makaa ya mawe

Nilikutana na vishawashishi vingi ikiwemo mitego ya khanga moko kutoka kwa wanawake wa mitaa ile, kuna muda nilikuwa natokeza kwenye vyumba vya watu, wakati mwingine nilisikia sauti za migegedano, kuna muda nilikutana na vijana na mabinti wakichapana bakora za kiutu uzima wazi wazi. Kuna muda nilikatiza kwenye Gesti bubu na kukuta mwanamke na mwanamke wakizichapa wakiwa watupu. Yote kwa yote, hayo hayakunihusu, tuendelee na safari yetu

Baada ya kama dakika 20 hivi, nilikutana na wakina mama wakiwa nahisi ni kwenye kikundi, kipochi au kikoba. Kwa kuwa binafsi huwa ninaloose confidence ninapokutana na umati wa wanawake nikaamua kuwapita pasi na kuwasemesha chochote kitu. Walikaa kimya kwa muda wa dakika moja kisha mmoja wao alisikika akisema "Awee, usinambie", walifuatiwa na "hehe heee alooo". Nikaona potelea pote. Hapo hapo katika harakati za kuduwaa nikaskia, "Ashura mpelekee na maji kwenye ndoo, mwambie asiache kimba juu ya sink"

Nilipopinda kona kuona labda nitatokeza eneo la wazi, nikajikuta nachomozea PUTO, yaani choo cha majirani, muda huo huo maji yakanifuata, kisha kile kitoto kikatokomea. Nikajikuta natabasamu na kusahau kabisa suala zima la shida ya maji katika nchi yetu. Hapo hapo kakaja katoto ka kiume kakanambia, "Mama anauliza kuwa, au unataka kukojoa kiutu uzima?". Nikaamua kukafukuzia mbali. Sekunde chache nikasikia watu wakianguka kicheko. Dah! Nikahesabu kuanzia 9 kurudi nyuma. Baada ya hapo walishtukia tu mtu keshafika kwenye lami mahali alipoanzia safari, tayari kwa kufuata barabara ile ya lami

Nilifika nyumbani saa tatu hivi nikiwa nimechoka sana na kupokelewa na mke wangu, Mwa J na wanangu wawili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom