kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,255
- 16,185
Askari hawaoni tabu kumuua Raia mwenzao ambae hana silaha mwenye mawazo tofauti na watawala. Hiyo imegeuka kuwa fasheni yetu sasa Afrika Mashariki.
Viongozi wetu ni kama vile wanatafuta Uhuru upya. Wanapambana na yeyote anayewapinga sawasawa na walivyofanya makaburu na wakoloni kwa watu weusi.
Wanatumia kila fursa hata covid 19 kujinufaisha kisiasa. Wanatumia wabunge waliopitishwa kwa njia za gizani kutunga sheria zenye upogo ili kujibakisha madarakani milele.
Nchi zao nilazima ziongozwe na wao wengine hawawezi wataharibu. Kila anaesema hivyo sivyo anatumiwa na mabeberu. Watampa jina baya ili wahalalisha kumpiga, kumuweka kizuizini, kumuua, kumrushia tears gas, kumfungulia mashitaka, na kila aina ya kumnyamazisha.