Afrika Kusini yatishika na waranti ya Putin ya ICC

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,621
46,268
Kumekuwepo na taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwamba kutokana na waranti ya ICC iliyotolewa kwa Putin Africa Kusini isingependelea Putin ashiriki mkutano wa wakuu wa nchi wa BRICS utakaofanyika katika nchi hiyo mwezi wa nane mwaka huu.

Makamu wa Africa ya Kusini amepenedkeza waziri wa mambo ya nje wa Urusi kuiwakilisha nchi hiyo badala ya Putin.

Africa Kusini ni mwanachama wa ICC na anapaswa kutoa ushirikiano kwa mahakama hiyo japo wakati mwingine imekuwa haifanyi hivyo kama ilivyotokea kwa waranti ya Rais wa Sudan Omar Al-Bashir. Hata hivyo jambo hilo limekuwa likizua migogoro mikubwa ya kidiplomasia.
 
Shida kuwa ipo siku Africa Kusini watashitaki ICC alafu wakataka mhalifu aliefanya uhalifu mchini mwao anatakiwa kukamatwa na taifa nyingine.
 
Jana nimecheki WION, Kremlin wenyewe wamedai lazima ahudhurie hio summit, so SA wawe wapole sana.
Sema kinacho hofiwa ni shambulizi la kigaidi.
 
Back
Top Bottom