Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,661
- 46,349
Baada ya sarakasi nyingi kuhusiana na ushiriki wa Putin katika mkutano wa BRICS utakaofanyikia Africa Kusini hatimaye vyombo mbalimbali vya habari duniani vimeripoti taarifa kutoka Ikulu ya Africa Kusini ya Rais Ramaphosa ikisema Rais huyo wa Urusi hataweza kuhudhuria mkutano huo.
Endapo Putin angefika Africa Kusini angejiweka katika hatari kubwa ya kutiwa nguvuni na taifa hilo mwanachama wa ICC.
Hata hivyo Africa Kusini wakati mwingine huwa haitoi ushirikiano kwa mahakama hiyo kama ilivyokataa kumkamata Omar Al-Bashir wa Sudan.
Vyombo mbalimbali vya habari viliripoti pia kwamba nchi hiyo haikuwa inapendelea sana Putin kuhudhuria kutokana na utata wa kidiplomasia ambao ungeibuka.