Afrika Kusini yapendekeza nchi zitoe majeshi yatumike kuvusha misaada Rafah watu wasiendelee kufa

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,186
10,922
Bi Naledi Pandor, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini ameshangazwa na matumizi ya maneno pekee kutaka misaada ifikishwe Gaza bila vitendo huku watu wakidondoka mitaani kwa njaa.

Amesema wale wale wanaipa Israel silaha iendeleze maangamizi ya Wapalestina kama hawana undumilakuwili kuhusiana na maafa ya Gaza basi wana wajibu wa kufikisha misaada hata kwa kutumia majeshi yao ili vyakula viingie Gaza kuokoa maisha ya watu.

Pamoja na pendekezo hilo, Bi. Naledi ametaka Umoja wa Mataifa ufanyiwe marekebisho makubwa na kiwe chombo cha kidemokrasia zaidi. Kwanza ametaka utaratibu wa veto wa mataifa matano tu uondoshwe na kuwepo na uwakilishi wa kimabara kwenye baraza la Usalama la taasisi hiyo.

Mbona yupo kimya wakati kichapo kilipokuwa Yemen
 
Mtakufa sana, temaneni na Wayahudi, hubirini dini yenu kwa amani, yule Myahudi Mungu wake ana nguvu nyingi kumshinda wenu, na hajaanza kudhihirisha ukuu wake leo.
 
Africa kwenye lindi la umaskini na viongozi wa hovyo hamna tofauti na huko Gaza ambako viongozi wake wanapenda vita kuliko kitu chochote.
 
Mtakufa sana, temaneni na Wayahudi, hubirini dini yenu kwa amani, yule Myahudi Mungu wake ana nguvu nyingi kumshinda wenu, na hajaanza kudhihirisha ukuu wake leo.
Acha kurudia rudia kufru zako
 
Natamani na Tanzania yetu itoe sauti hata kidogo, na sio kuwakubatia makafiri hao
 
Naunga mkono hoja, Tena nakazia UN ni chombo Cha wahuni wachache Kwa Maslahi Yao.

UN ni sawa na katiba ya CCM hapa Bongo lala
 
Hypocrite kiwango Cha lami ameshindwa kupeleka jeshi kwa majirani zetu tu hapo Sudani
 
Kwa hiyo baada ya kuua, kubaka na kuteka wayahudi Bado hakuna sababu ya kuwapiga?
Kama wanawajua Hamas walipo wapambane nao .Kinyume cha hivyo wasiue watu ovyo na kuwazuilia chakula watapata laana zaidi za Mungu.
 
Back
Top Bottom