African University Ranking | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

African University Ranking

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mwanjelwa, Jan 30, 2009.

 1. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Inakuwaje Universities za South Africa tu ndiyo zinakuwa top katika Africa?
  Hata hivyo UDSM nao wapo wapo sana....!

  Source: Ranking of African Universities on the web - Best Universities in Africa

  The InternetLab Ranking of 30 Top African Universities
  Rank University Country World Rank
  1 University of Cape Town South Africa 398
  2 Universiteit Stellenbosch South Africa 566
  3 Universiteit van Pretoria - University of Pretoria South Africa 718
  4 University of the Witwatersrand South Africa 720
  5 Rhodes University South Africa 738
  6 University of South Africa South Africa 1,449
  7 University of the Western Cape South Africa 1,553
  8 American University in Cairo Egypt 1,826
  9 Noordwes Universiteit - North West University South Africa 1,857
  10 University of KwaZulu-Natal South Africa 2,214
  11 University of Johannesburg South Africa 2,323
  12 University of the Free State South Africa 2,369
  13 Université de La Reunion France 2,387
  14 Nelson Mandela Metropolitan University South Africa 2,542
  15 University of Dar Es Salam Tanzania 2,819
  16 University of Zimbabwe Zimbabwe 3,072
  17 Al Akhawayn University in Ifrane Morocco 3,174
  18 Cape Technikon South Africa 3,414
  19 University of Mauritius Mauritius 3,682
  20 University of Zululand South Africa 3,724
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mimi nashindwa kuamini hii kitu..kwani niliona University of Morgadishu iko juu ya University of Ghana!

  Sijui kama kuna walakini!

  Ndo hivyo tena!
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  nina uhakika iko juu ya Udsm pia....
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Teh teh teh!

  Mogadishu ya Somalia?
   
 5. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  UDSM iko juu eehh, pamoja na misukosuko yoote! South Africa imeendelea sana kama tukiitoa, UDSM inakuwa first- kwani kile cha Egypt kinaonekana ni cha wamarekani na cha Reunion cha wafaransa.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Jan 30, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Mogadishu kuna university?
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Somalia vyuo vyao ni best kuliko vya tanzania......
  NN Mogadishu vyuo sio kimoja na watu wanakula nondo angalia Mogadishu University

  Hujawahi kukutana na wasomali walio kula nondo somalia?

  Sasa angalia hiki University of Somalia University of Somalia hata ada yao ni affordable na mamikopo ya kumwaga ada $400 kwa mwaka....

  Mimi nafikiri tuache kulia lia kwenye balozi za wazungu na kujidhalilisha kuomba Visa huku kuna sehemu wanatoa elimu bora kama Somalia
   
 8. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Somalia vyuo vyao ni best kuliko vya tanzania......
  NN Mogadishu vyuo sio kimoja na watu wanakula nondo angalia Mogadishu University

  Hujawahi kukutana na wasomali walio kula nondo somalia?

  Sasa angalia hiki University of Somalia University of Somalia hata ada yao ni affordable na mamikopo ya kumwaga ada $400 kwa mwaka....

  Mimi nafikiri tuache kulia lia kwenye balozi za wazungu na kujidhalilisha kuomba Visa huku kuna sehemu wanatoa elimu bora kama Somalia
   
 9. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2009
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Siioni Univ of Cheikh Anta Diop, Senegal. Wala Univ of Ghana nadhani vyuo vingi vya west vinatupiga bao....

  I am surprised kuhusu UCT kushika nafasi bora zaidi ya Wits...
   
 10. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
 11. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nemewahi kujaribu kucheki rank mbalimbali still udsm hakijavuka 30.Katika baadhi ya ranks kwenye top 100 of Africa only Udsm and SUA ndo vipo.sijui kwa wengine hasa mzumbe inakuwaje.Still we have work to improve our education Quality.
   
 12. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  179 University of CAPE TOWN South Africa
  319 University of the WITWATERSRAND South Africa
  CAIRO University Egypt
  University of KWAZULU-NATAL South Africa
  University of PRETORIA South Africa

  Hizo ndo zipo kwenye top 500 Duniani, kazi ipo tena na hii migomo ya UDSM sidhani kama imesaidia.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Japo sijui vigezo rasmi vya hizo ranking, UDSM ingestahili kupata a better ranking kama sio baadhi ya matatizo ya kujitakia yanayosabaishwa na wahadhiri wetu.
  Nitatolea mfano Kitivo cha Sheria, UDSM. Kwa miaka zaidi ya 15, kitivo hicho hakijawahi kutoa 1st Class ya Sheria. Wakati nikiwa UD, kuna baadhi ya wanafunzi were really bright tuliwategemea 1st Class lakini wapi. Niliwahi kuwauliza wahadhiri kulikoni, nilijibiwa in short wanafunzi wa siku hizi, hawasomi.

  Conclusion binafsi nimeifikia kuwa japo kunawanafunzi wazuri wangeweza kupata 1st Class lakini walimu wanawabania. Matokeo yake ni chuo kinachofelisha. Kukosekana kwa 1st Class kumepelekea hakuna Mtanzania aliyekwenda kusomea advanced degree sheria kwenye the best law universities for the past 15 years. Hivyo kuchangia kudharaulika kwa LL.B ya UDSM. Kwenye EAC. Zamani the best law students walitoka UDSM, now Makerere na Nairobi wanamwaga ma 1st Class na kupeleka vijana Yale kiasi cha kufanya LL.B yetu isahaulike kwenye medani za kimataifa. 1st Class 3 za mwisho za LL.B, UDSM ni Dr. Asha Rose Migiro, Prof. Palamagamba Kabudi na Dr. Hamoud Majamba. Naamini kumetokea vijana wazuri tuu ila maticha waliwabania na wataendelea kuwabania kisa kwanini wao wapate?.

  Niliwahi kutembelea UN, HQ pale New York. Nikauliza taratibu za kupata kazi UN. Sifa ya kwanza ni Advanced Degree ambapo 1st Degree lazima iwe 1st Class ama Upper 2nd with Honours. Ajira hizo huzigawa kwa Zones mbalimbali. Tanzania iko The Eastern & The Horn of Africa. Tuko kundi moja kwa nchi za Afrika Mashariki, Somalia, Ethiopia na Eritrea. Asilimia kubwa ya nafasi hizo zimeshikwa na Wasomali wakifuatiwa na Wakenya, Waganda, Waeritrea, Waethiopia na sisi Watanzania ndio wa mwisho.
  Nikamuuliza mwenyeji wangu, mtu wa foreign hii inakuwaje?. Au inamaana Watanzania ni vilaza?.Akanijibu hapana akasema tatizo la Watanzania hawaombi hizo nafasi zinapotokea.

  Utafiti wangu ukagundua kila zinapotokea nafasi, wenzetu wanazitangaza hizo nafasi kwenye local media zao kwa raia wao na kuwaencourage waombe, sisi foreign wanazibania kupeana na matokeo yake wanakosa na wenzetu wanazijaza, kisa kwanini wewe upate. Japo nafasi hizo ziko open kwenye net, pnp yenye ufs foreign office ina matter sana.
  Katika kubaniana academically, tunajikuta tunashusha rank za vyuo vyetu.
   
 14. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Huu ndio aina ya uzalendo Watz tunataka!

  Ahsante Mkuu!

  Quality or quantity? Ipi muhimu ndugu?
   
 15. K

  Koba JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  .....flatout lie,practically nawajua waliotoka hapo Law faculty na ningeweza kuweka majina yao hapa lakini privacy issue haziruhusu,na wamesoma to the one of the best law schools in the World from Columbia NY,Northwestern Chicago sasa sijui wewe hizo data zako ni za wapi? na nani kakuambia 1st class nyingi ndio ubora wa chuo?
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Hmmm! Pamoja na UDSM kufungwa karibu kila mwaka kutokana na migogoro bado kinashika nadasi ya 15!!!!
   
 17. N

  Njimba Nsalilwe JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2009
  Joined: Mar 23, 2008
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Sio kielimu nafikiri ni website yake.
  Kwa hiyo hata kama wao wakigoma website ipo hewani.

  Njimba
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Hakuna ubishi umuhimu wa quality dhidi ya Quantity ila ili chuo chako kipande hadhi, kuna issue unatoa best students wangapi wanaojoin top graduate schools. Kama sheria UDSM hatujatoa 1st class for more than 15 consecutive years, sisi bongo tunajua UDSM inatoa good lawyers lakini wakenya wakipeleka wanafunzi Yale kila mwaka, then inaonekana kenya ndiyo yenye briliant output.
   
 19. T

  Tango Member

  #19
  Jan 31, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Nafikiri si website, kuna wakati nilikuwa nafikiri hivyo lakini nikafanya utafiti kidogo nikaona aah wapi. Nairobi wana website nzuri sana very informative lakini wapi. Pia Mzumbe na OUT wanawebsite nzuri sana lakini wapi.

  Nafikiri hizi ranking mara nyingine zina kaukweli kwani kuna mtu alikuja nimtafutie kazi pale Dar akasema amesoma BSc. Mathematics na computer science ya Fort Hare University huko SA. Nikamwambia akascan docs zake akaniuliza kuscan nini? Nikamshangaa sana.. yaani Computer science lakini hajawahi kuscan kitu. Akanionyesha CV yake..duh. Kituko kitupu hakuna cha field attachment hakuna cha nini. Course zenyewe hazijaeleweka vema na akasema yeye alipokuwa third year alipewa kazi ya u-tutor kwa mwaka wa kwanza kwa sababu alikuwa ndio kipanga wa darasa.
  I think Mlimani wanajitahidi wanatakiwa tu waondoe vitu vichache vichache na wakazanie zaidi quality kuliko number.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Its not fair kusema flatout lie. Nimetolea mfano kitivo cha sheria, UDSM, nimekuambia for more than 15 hatujatoa 1st class ya sheria. The top law school inaongozwa na Yale
  Ikifuatiwa na Havard, bila 1st class no admission. Hakuna mtanzania amesoma huko sheria toka UD. Wakenya na waganda wapo. Uwongo wangu upi.?.
   
Loading...