African 'one term' presidents: Will Magufuli take a course?

Chadema walishinda lakini CCM waliiba kura
Potea pote. Sasa hawataiba tena? Hii excuse ya kuiba kura hata kama ina ukweli lakini imepitwa na wakati. Kama wanajua wataiba kura halafu wanaridia kufanya yale yale basi hawana maana.
 
Ulitegemea Kinana na Makamba sr watajwe kumhujumu rais na CCM?
Ushabiki au chuki kwa awamu ya sasa kusikufanye usione uhasilia wa siasa! Wewe ulitegea Dr Slaa atoke Chadema na aungane na Magufuli? Ulitegemea Lowassa atoke CCM na apokelewe Chadema kwa mbwembwe zote wakati walikuwa wanasema ni fisadi mkubwa? Wanasiasa hubadilika wanapoona maslahi yao yanatishiwa!
 
Huu ni mjadala mzuri tu wala haunà tatiźo. Binafsi nimekuwa na mawazo hayo hayo ya one term president. Sababu kubwa ni kwambà hakujiandaa na hata baada ya kushawishika kujitosa hakutarajia kushindà. Kwa sababu hizi ametumia nguvu nyingi sana kuongoza hali ambayo imemsababishia maadui wengi wa kisiasa nje na ndani ya chama chake. Mbali na kuchoka pia sidhani karma ccm asilia iko comfortable na style yake ya Uongozi. Dalili ni ukimya wa wazee wengi.
 
Kumbe inawezekana kuwa na one term president?
 
FAO LA KUJITOA

Hao wanyonge wanaotetewa ni akina nani?

Au Lazima nchi iwe na wanyonge milele ili wasaka tonge wapate umaarufu

Mara huku DEGE eco village kigamboni, mara kule majengo hayana wapangaji?

ili mradi tu wametafuna pesa za wanyonge...Kwel laana hii itawapata kuanzia watoto mpaka wajukuu, wallahi
 
Mbona unaongea kitoto sana, eti "Watajibu kwa njia yoyote ile".. What a Lunacy.

Ujinga ujinga kama huu ndio umemfanya huyo Mohammed Morsi awe jela hadi leo akisubiri Kitanzi. Duniani hakuna bingwa.
 

God forbid! Ninaamini kwa dhati kabisa unayedhani unamtetea hakubaliani hata kidogo na mtazamo wako wa kutisha raia wemà. Binafsi sijaona chokochoko yoyote hapo tofauti na maonì binafsi. Nadhani kauli kama hizi ķamwe haziujengi utawala huu. Badala yake zinaufanya kuonekana tofauti kabisa na nyingine zote zilizotangulia; tofauti kabisa na utamaduni wa kisiasa wa nchi hii.
 
Potea pote. Sasa hawataiba tena? Hii excuse ya kuiba kura hata kama ina ukweli lakini imepitwa na wakati. Kama wanajua wataiba kura halafu wanaridia kufanya yale yale basi hawana maana.

Hakuna kilichopitwa na wakati, CHADEMA itaendelea kushinda uchaguzi hata kama haitandangazwa mshindi. Watu wa nje pia wanaona upuuzi unaofanywa na serikali hii nao pia wameanza kuchukua hatua. Kwa mfano Benki ya Dunia imesitisha msaada wa $50 milioni kwasababu ya sheria ya kipuuzi ya takwimu, tutapiga kampeni pia watu wa nje waanze kuweka vikwazo kuhusu matukio ya uchaguzi.
 
Hakuna nchi ya nje itakayofanya chochote! Wako kimaslahi na hawawezi kuvuruga maslahi yao kwa vitu kama hivi. Zanzibar matokeo yalibadilishwa mchana kweupe na hakuna kilichotokea! Watanzania hatuna tabia ya kusoma vitabu. Ungekuwa msomaji ungefunguka macho jinsi nchi za magharibi zinavyofanya kazi.
 

Naamini vikwazo vitafanya kazi na huku kunyimwa $50 milioni ni mwanzo tu. Sikusikia Zanzibar wakiwekewa vikwazo lakini hayo yameshapita, cha msingi sisi tumeshaanza kuwekewa vikwazo na sisi tutazidi kuwaomba wafadhili wazidi kubana. Kama Saddam na Gaddafi waliondolewa hakuna anayeshindikana.
 
Unajua kilichofanya kina Sadam wakaondoka? Naona uko ulimwengu mwingine kabisa.
 
Hahaaaa! Mkuu umenifanya nicheke. Watz tumezidi kulalamika
 
Mkuu huyo Jmc06 haijaanza leo hawezi kuchangia hoja yeyote kazi yake na mwenzake TumainiEli ni kutafuta wachangiaji ndani ya JF na kuwatisha.
 
Kwa vile nchi za nje haziwezi kufanya chochote ndiyo sababu inayokipa kiburi serikali kuendelea kupindua matokeo na kufanya inavyotaka au kuna sababu zingine.
 

Mkuu,

Wewe, Tindo na yule mwenye avatar ya yule msichana wa Pakistani nyote mna mawazo mazuri sana na nnawapenda kwa kuwa na mawazo ya kuchagiza.

Mnachokosea tu, ni namna ya kuyawasilisha mawazo yenu na sijawahi kuona mnatoa matusi wala lugha ya kashfa.

Si ninyi ambao mnafanya hivyo bali wenzenu wenye mawazo kama yenu.

Ondoeni "contents" zenye kuchochea, kukashifu, kutukana, kutisha na kukejeli serikali iliyopo madarakani.

Kwa mfano umeweka kichwa cha mada yako kikielezea viongozi wa Afrika ambao hawakudumu madarakani na ukasema " Will Magufuli take a course?

Unamaanisha kwamba je Raisi Magufuli nae atafuata mkondo?

Sasa kwa tafsiri ya hicho kichwa cha habari na yaliyomo humo ni mapinduzi, kuondolewa kwa nguvu viongozi na hata kuuawa kwa mmoja wa viongozi hao.

Na unamwambia raisi Magufuli kwamba na yeye atafuata mkondo, wamtisha raisi wako? waitishia mamlaka? je watishia taasisi ya uraisi?

Hivyo ndivyo baadhi ya wageni na wanachama wengine watakuwa wanaweza.

Usidhani ni sisi tu wanachama wa JF twasoma hapa wapo watu wengi wa rika tofauti, kazi tofauti na malengo tofauti.

Tumia njia sahihi ya kuwasilisha maoni yako bila kumkwaza mtu, kumuudhi na hata kufanya akuchukie, hatua ambazo zitajenga uadui uso lazima.

Otherwise, I like you guys and your way of thinking!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…