African 'one term' presidents: Will Magufuli take a course?

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Afrika inajulikana kuwa na marais wanaokaa madarakani kwa muda mrefu kama, Yahya Jammeh wa Gambia, Robert Mugabe wa Zimbabwe, na Yoweri Museven wa Uganda, Kwa Afrika ni nadra sana rais kuondolewa kidemokrasia kwa sanduku la kura kabla ya kipindi chake kuisha.

Lakini kuna marais wa Afrika waliodumu madarakani kwa kipindi mfupi kati ya siku mbili hadi miaka minne au muhula mmoja kwa sababu mbalimbali kama mapinduzi ya kijeshi, kifo, uchumi, kuuawa (assassination), utawala mbovu.

Christopher Elnathan Okoro Cole wa Sierra Leone aliyekuwa Jaji Mkuu wa nchi hiyo April 1971 aliapishwa kuwa rais na siku mbili baadaye akajiuzulu na kumkabidhi madaraka waziri mkuu Siaka Stevens.

Yusuf Kironde Lule wa Uganda alikuwa rais wa Uganda kwa siku 68 tu (April 13 -June 20, 1979), wananchi walimkataa, 'he became unpopular', aliondolewa na bunge.

Robert Guei – Ivory Coast alikuwa rais kwa miezi 10 tu, December 24th 1999-october 26, 2000), alishindwa kwenye uchaguzi na Laurent Gbagbo.

Michel Djotodia alikuwa rais wa Central African Republic kwa miezi 9 tu, (March 24, 2013 - January 10, 2014) aliingia kwa kuipindua serikali, aliondolewa na umoja wa mataifa baada ya kushindwa kukomesha mauaji ya kidini.

Ernest Adegunle Oladeinde Shonekan alikuwa rais wa Nigeria kwa miezi 3 tu, (August 26, - November 1993) baada ya Gen. Ibrahim Babangida kulazimishwa kujiuzulu na wananchi, na yeye alikuja kuondolewa na jeshi sababu ilikuwa kudorola kwa uchumi.

Gen. Tito Okello aliyekuwa kiongozi ndani ya jeshi la Uganda alimpindua Milton Obote, Okello alikuwa rais wa Uganda kwa miezi 5 tu, (July 29, 1985 January 26, 1986). Aliondolewa na waasi wakiongozwa na Yoweri Museven ambaye hadi leo bado rais.

Thomas Sankara wa Burkina Faso aliingia madarakani mwaka 1983 kwa mapinduzi ya kijeshi, aliwaahidi wananchi kuleta mapinduzi ya kiuchumi, October 15, 1987 aliuawa na wajeshi.

Melchior Ndadaye wa Burundi, alikuwa rais Mhutu wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia, alidumu madarakani kwa miezi 3 tu, (July 10, 1993 - October 21, 1993). Aliuawa na wanajeshi wa Kitusti.

Mohamed Morsi alikuwa rais wa kwanza wa Misri wa kuchaguliwa kidemokrasia, aliingia madarakani June 30, 2012 baada ya nguvu ya umma kumwondoa dikteta Hosni Mubarak, wananchi waliamini kuwa labda Morsi atakuja kuwa kiongozi mzuri kwao. Baada ya Morsi kupewa madaraka alibadili katiba na kujipa madaraka yote, kila kitu aliamua yeye bila kulihusisha bunge, mahakama wala vyombo vya sheria. Aliwakamata na kuwaua wote aliokuwa wakimpinga.

Kutokana na utawala wake wa mabavu wa kutofuata sheria Morsi alishitakiwa na ilipofika May 2015 alihukumiwa kunyongwa na mahakama ya nchi yake.

Tuna cha kujifunza kutokana na utawala huu wa Magufuli?
 
Watanzania ni wanafiki na malimbukeni wanaopenda mteremko kwenye kupata mafanikio....

Mlilia lia kikwete fisadi, huduma mbovu, wenye nacho wanasikilizwa kuliko wasionacho mkawa mnaomba usiku kucha atoke rais wa tofauti mkalli asiwe legellege like kikwete amepatikana mnaanza kulalamika ooh mara ivi mara kilikwenda kimerudi pumbavu kabisa.

Magufuli kanyaga mafuta twende wasikutishe.
 
Pamoja na hayo haizuii watu kutoa maoni yao juu ya utawala wake.
 
Nikweli lakini imekuwa too much to the extent sasa....
Ikisoma bandiko hilo limejaa hadithi za mapinduzi mapinduzi na kutokamilisha mihula ya uongozi.

Hadithi kama hizi zinapandikiza threats na upumbavu, why now?

KWENYE BIBILIA WAMEANDIKA ATAKAE VUMILIA HADI MWISHO NDIO ATAKAE OKOKA lakini hapa tunaona kuna mipumbavu ambayo ilizoea kuiba imeshindwa kuvumilia kusubiri matunda, maziwa na asali yameanza kuleta choko choko.

Kwa mjibu wa katiba ibara ya 15, 17, na 18 unaruhusiwa kutoa maoni lakini kwa namna gani basi, kwa namna ambayo haivunji utu wa mwingine wala kumdharisha na kukashifu.

Na ukumbuke unavyo mkashifu raisi unakuwa umemkashifu kiongozi wa taasisi ya urais jopo lake halitakubali kuendelea kukashifiwa kwa namna yoyote ile na wao watajibu kwa njia yeyote ile kutetea taasisi yao.
 
Hakuna cha too much..... rais anaongoza watanzania mil 50 wenye fikra tofauti kwahiyo ategemee kupata changamoto zaidi ya hizo.

Kukosoa au kutoa tahadhari au kupinga kitu siyo kashifa wala kudhalilisha na ipo kisheria utaona ni kashifa kama hautapendezwa na unachokosolewa,
 
Waliosema CDM ni nyumbxxx hawakukosea, yaani uchaguzi wa Ubunge makao makuu ya Ufipa mmeshindwa, Monduli kwa Rais wa mioyo yenu mmeshindwa halafu hapo hapo unaota kumshinda Magu Tz nzima.
KATAA KUWA NYUMBXXX.
Topic umeielewa lkn?
 
Sijakataa maoni na ushauri ni vizuri kuendelea kutolewa kwa mjibu wa katiba yetu lakini kwa methodology zilizo nzuri zisizo za kukashifu na kudhihaki na vitisho juu.

In short methodology mnazotumia kushauri na kutoa maoni ni tactically wrong hakuna kiongozi duniani mwenye akili akasikiliza maoni au ushauri kutoka kwa njia na watu wenye kukashifu serikali au taasisi.
Hakuna cha too much..... rais anaongoza watanzania mil 50 wenye fikra tofauti kwahiyo ategemee kupata changamoto zaidi ya hizo.

Kukosoa au kutoa tahadhari au kupinga kitu siyo kashifa wala kudhalilisha na ipo kisheria utaona ni kashifa kama hautapendezwa na unachokosolewa,
 
Sijakataa maoni na ushauri ni vizuri kuendelea kutolewa kwa mjibu wa katiba yetu lakini kwa methodology zilizo nzuri zisizo za kukashifu na kudhihaki na vitisho juu.

In short methodology mnazotumia kushauri na kutoa maoni ni tactically wrong hakuna kiongozi duniani mwenye akili akasikiliza maoni au ushauri kutoka kwa njia na watu wenye kukashifu serikali au taasisi.
Mkuu unataka methodology gani sisi backbencher tutumie, mimi siyo mbunge kuwa nitaenda bungeni kushauri, siyo waziri nitaingia kwenye baraza la mawaziri kumshauri wala siyo mwanasiasa nitapata platform niseme, methodology yangu ya kushauri ni through mitandao ya kijamii bila matusi wala vitisho.

Hivi kusema kuna one term presidents ni kumtisha rais, basi rais wa kutishwa hivyo hafai kuwa rais, afterall Ikitokea haitakuwa ajabu na hatakuwa wa kwanza kuwa one term president Tanzania, Abdul Jumbe alikuwa one term president.
 
Katika kutoa maoni yetu kwa ajili ya nchi yetu tusitumie maneno yenye kukashifu,kudhihaki, na kutukana mamlaka.

Kama ulivo sema wewe hutukani,hudhihaki wala kutoa maneno yenye kutishia us alama na ustawi wa nchi. Lakini tambua kuna watu wengine wengi tu hutumia mitandao kuzusha, kudhihaki, kutukana mamlaka nk.

Maoni yanayotolewa kwa staha husikilizwa na kufanyiwa kazi hata kama sio kwa haraka lakini hushughulikiwa.

Kuhusu vitisho...
Unadhani nchi ambazo viongozi wake walipinduliwa au waliondolewa kabla ya mihula yao kuisha nchi hiyo zimetulia. ..?hebu nenda fanya Google search za nchi hizo uangalie hali zao zipoje kwa maana ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiusalama.

Nikwambie kitu magufuli akitolewa kwa njia hizo wakaingia hao mnao waona bora sasa kabla ya muda wao nao watatolewa na makundi mengine ambayo yatapata uhalali wa kutumia njia hiyo hiyo iliyotumika kwa magufuli hivo choko choko za ajabu na visa havitaisha humu nchini.

So lets think twice sio kuwaza pesa tu mifukoni ukiwanazo kama huna amani utashindwa kutimia hizo pesa.

Sawa... hivi umejiuliza ni kwanini leo watu wameanza kuwa na mawazo ya 'one term president' kwanini haikutokea kwa Mkapa wala kipindi cha Kikwete?

Ndio majuto ni mjukuu lkn watu wakiamua huwa hawaangalii matokeo ndiyo maisha yalivyo.

Tunapotoa mifano hiyo ya marais waliopinduliwa au kuondolewa na bunge siyo vitisho ni mafunzo kwa watawala na wananchi kwamba watendeane haki yasije kuwakuta kama hayo.
 
Hivi ni funzo gani unatoa hapo?
Hakuna funzo linalotolewa kwa vitisho....

Maranyingi vichocheo chanya huleta matokeo bora zaidi na kwa wakati kuliko vichocheo hasi.

Kwanini sasa? Kwa sababu sasa tayari kuna wanyang'anyi wa nchi na rasilimali za keep wameanza kushughulikiwa vilivyo ili kuleta usawa kwa watu wote. Hawa wanyang'anyi wametengenezwa katikati awamu hiyo zilizopita na ukazitaja.

Wanyang'anyi hawa sasa hivi wanateseka wanavyo shughulikiwa vilivyo kwani walizoea kufanya vile watakavyo kana kwamba the whole country belonging to them and no one deserve to live while kwa kuwanyekea wao kwa sababu walimiliki sehemu kubwa ya resources zetu.

This is why now.
 
Hata kama walitenda makosa huko nyuma anatakiwa atende haki na afuate sheria wakati anawashughulikia siyo kwa kuwateka.

Jamii inachoangalia nini anafanya leo haiangalii nini walifanya huko nyuma, jamii itamhukumu rais kutokana na yale anayowatendea wakosaji.
 
Watanzania ni wanafiki na malimbukeni wanaopenda mteremko kwenye kupata mafanikio....

Mlilia lia kikwete fisadi, huduma mbovu, wenye nacho wanasikilizwa kuliko wasionacho mkawa mnaomba usiku kucha atoke rais wa tofauti mkalli asiwe legellege like kikwete amepatikana mnaanza kulalamika ooh mara ivi mara kilikwenda kimerudi pumbavu kabisa.

Magufuli kanyaga mafuta twende wasikutishe.
Hapa Kazi Tu....HAWATOMUWEZA KAMWE
 
Hata kama walitenda makosa huko nyuma anatakiwa atende haki na afuate sheria wakati anawashughulikia siyo kwa kuwateka.
Umeona sasa kauli zako(zenu) ni nani atakaewasikiliza hata kama ni mwendawazimu......

Una uhakika yeye ndio anateka au anaagiza kuteka.

Je ni wapi hafati sheria?
 
Kuna wangapi wameumizwa awamu hii kwa makosa ya kuhisiwa au kusingiziwa,
Kesi ya Lugumi imeishaje, kesi ya milioni 7 kwa dakika iliishaje, Manji na madawa ya kulevya imeishaje,

Hizo ni baadhi tu ya kesi zilizoumiza watu bila sababu za msingi achilia mbali kuminywa kwa uhuru wa demokrasia ya vyama vingi, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kufanya tafiti, mauaji na utekaji kuongezeka, ni mengi tu yametokea wakati wa utawala wake.

Hayo na mengi lazima watu waanze kufikiri one term president.
 
Haya yote yallikuwa yanatokea wakati wa nyuma au awamu zingine ila sasa yanaonekana makubwa kwa sababu ya utandawazi na kukuwa kwa technology...

Magufuli sio malaika yule ni binadamu mengine anakosea na kwa nafasi yake pengine wapo washauri wake wanampa mawaidha mabaya as a leader wa taasisi inabidi atekelleze tu kwa sababu system inamtaka hivo hata awe nani itakuwa hivo hivo tu.
 
Back
Top Bottom