Kama hali itakuwa hivi:
tutegemee machafuko zaidi kuanzia kesho mpaka siku ya final, nadhani fans wa EQG hawaani kama wametolewa kwenye mashindano.
Mbona huko nje nako naona picha ya dude gani sijui linapita angani mpaka waamuzi na wachezaji nao wameingiwa na hofu tena.
Ingawa ni kweli Ghana wanastahili kwenda fainali, lakini mwamuzi anastahili lawama zote kwa hayo yanayotokea. Maamuzi yake ya kipindi cha kwanza na kwa timu changa kama EQ.G, ni dhahiri ilionekana kana kwamba anataka kufuta dhana ya mbeleko, lakini maamuzi mengi yalikuwa ya kukera kwa wenyeji.Kama kuuma angekuwa anauma na kupuliza kimtindo mtindo, si ndiyo mambo yetu ya uzalendo kwa Afrika.
Matokeo ya mbili kipindi cha kwanza, hayakuonesha taswira ya mpira ilivyokuwa, Wazee wa Mbeleko walikaza buti kisawasawa.
Kuna kila dalili ya mambo kunuka hapo.
Hebu tuone yatakayojiri ila naona wachezaji wa ghana wako katika hali ya utulivu sana ila mashabiki wa EQG wanaendelea kurusha chupa, wanang'oa viti na kurusha uwanjani kama mashabiki wa simba vile!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.