Africa Cup of Nations (AFCON) 2015 updates

Africa Cup of Nations (AFCON) 2015 updates

Huku kwa DRC dakika zilizobakia hata kuku hawezi kumeza punje ya mtama
 
Hii ni hatari, maana yake Congo Brazzavile watakutana na DRC!! Majirani hawa wenye historia inayofanana, sidhani kama wanapendana!
 
Mtangazaji wa supersport alikuwa anachemsha kumbe ! kumbe DRC amepita ! mpuuzi kweli kweli
 
Ila huu mpira wetu Afrika sijui ni kwamba timu zinafanana sana, au. Hamna ambition ya kufunga magoli, timu inakuwa na point kidogo ila inaenda hatua ifuatayo, alafu hizi timu nyingi zimekuwa wachoyo wa magoli, hamna burudani sana bila magoli!
Ila kitu kimoja kizuri, hamna timu kubwa Afrika, lazima upige mzigo la sivyo unafunga virago!
 
Wachezaji wengi hawajitumi 100% au zaidi, wengi mawazo yao yapo kwa timu zao za Ulaya, wengi wanaogopa kuumia, kupokwa namba, hawa jamaa wa CAF inabidi wabadilishe kalenda ya michuano hii , angalau ifanyike baada ya kwisha kwa ligi za Ulaya. Wamejitahidi kubadilisha mwaka kwamba isiwe inaingiliana na miaka ya kombe la dunia, sasa wabadilishe na kalenda yake vile vile. Kipindi hicho wachezaji wengi wanakuwa sokoni, wamemaliza ligi za mabwana zao wa Ulaya, wanaweza kujituma kama ilivyokuwa miaka ile ya zamani.
 
Leo patakuwa hapatoshi kati ya Algeria vs Senegal, ila ningependa wasenegal waibuke na ushindi. Jana nimeumia sana matokeo waliyoyapata cape verde yaliyowapelekea kufungasha virago.
 
South leo wameanza vzr mapungufu ya defense yamepungua kidigo
 
Kwa hiyo wadau mpaka sasa hili kundi Algeria anapita na nani? Kwa matokeo yalivyo mpaka sasa?
 
Kwa hiyo wadau mpaka sasa hili kundi Algeria anapita na nani? Kwa matokeo yalivyo mpaka sasa?

Algeria na Senegal wanapita, Algeria atakuwa na pointi sita, Senegal nne sawa na RSA lakini yeye atakuwa na zero goal difference wakti RSA atakuwa negative one, Ghana atawabeba wote kwa pointi zake tatu.
 
As it stands
Algeria 6 pts
Senegal 4 pts
Ghana 4 pts
RSA 2 pts
 
South afrika mashindano haya tatizo moja, defense mbovu na pumzi!! Washapigwa la pili kwa set pieces!!
 
Back
Top Bottom