Africa Cup of Nations (AFCON) 2015 updates

Africa Cup of Nations (AFCON) 2015 updates

Huyu refa naye anaharibu sasa, beki mmoja wa Ivory Coast karudisha mpira kwa goli kipa wake kwa kichwa na golikipa kuudaka matokeo yake refa kawapa Mali free kick ndani ya penalty box.

Mkuu soma maelezo yangu kwa namna ya kutafsiri sheria ya back pass. Refa yupo sahihi kutoa indirect free kick.
 
Hawa jamaa wa West Africa wana vipaji sana, kiukweli sisi huku East Africa tutasubiri sana, angalia yule Mmali anayechezea klabu ya Sudan alivyo na kipaji lakini hayupo. Kina Tchetche na ndugu yake walivyo na kipaji lakini hata kuitwa tu hakuna.

Si nasikia aliitwa!!! labda tu leo hajaanzishwa.
 
Dak24: Ivory Coast 0-1 Mali.
Matokeo yangebaki hivi hivi au Mali waongeze lapili, ili haya makubwa jinga yarudi kwao manake wachezaji wao wanacheza ki-father father sana.
 
Mkolaj hongera mkuu kwa ushindi Moro.
Ahsante, ila leo sijakuona mkuu Ngarna au unavutia kasi pambano la kesho!!! kila la kheir timu lambalamba funga hao mambumbumbu wa Aveva.
 
Raha ya mpira,unadunda. Chelsea,Man City, Southampton na Tottenham nje kombe la FA. Chelsea kapigwa 4 - 2 nyumbani baada ya kuongoza 2 bila dhidi ya Bradford. City kalala nae 2 mtungi dhidi ya Middlesbrough nyumbani. Southampton kapigwa 3-2 na Crystal Palace. Spurs nae kalala 2-1 kwa Leicester.
 
Ahsante, ila leo sijakuona mkuu Ngarna au unavutia kasi pambano la kesho!!! kila la kheir timu lambalamba funga hao mambumbumbu wa Aveva.

Mkuu nilidhani lambalamba mnamchukia zaidi yetu. Hahaaa.
 
Mkuu soma maelezo yangu kwa namna ya kutafsiri sheria ya back pass. Refa yupo sahihi kutoa indirect free kick.
Mkuu inaonekana hiyo sheria ni ngumu si umeona hadi beki mkongwe Kolo Toure naye alikuwa analalamika na kumwonyesha refa kwamba mpira ulipigwa kwa kichwa. Mimi nilikuwa najua ile last touch toka kwa beki kwenda kwa kipa ndo inayoangaliwa kumbe kuna vigezo vingine tena. Asante kwa ufafanuzi.
 
Je hawa Ivorian bado wana nafasi ya kufuzu na kusonga mbele?
 
Mkuu inaonekana hiyo sheria ni ngumu si umeona hadi beki mkongwe Kolo Toure naye alikuwa analalamika na kumwonyesha refa kwamba mpira ulipigwa kwa kichwa. Mimi nilikuwa najua ile last touch toka kwa beki kwenda kwa kipa ndo inayoangaliwa kumbe kuna vigezo vingine tena. Asante kwa ufafanuzi.

Kweli mkuu kutafsiri hiyo sheria ni ngumu. Imagine refa anachezesha Simba na Yanga aamue hivyo against mojawapo ya timu hizo.Patachimbika.
 
Moukandjo anaipatia cameroon goli la kuongoza
 
Naona hii timu ya Cameroon inajituma kuliko ile iliyopelewa world cup
 
Hii game tamu sana kila upande unatafuta magoli kwa nguvu zote, naipenda hii game kati cameroon vs guinea.
 
Goooooool!! 42, Traore anaisawazishia guinea goli. cameroon 1-1 guinea
 
Back
Top Bottom