Afisa wa Takukuru ajiua kwa kujipiga risasi

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
718
703
Afisa mwanadamizi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera amejiua kwa kujipiga risasi kidevuni

afisa huyo bw Francis Kitundu amejiua kwa kujipiga risasi leo saa nne asubuhi baada ya kutoka kwenye kikao cha ndani cha kujadili shughuli za taasisi hiyo.

Mkuu wa Takukuru wa wilaya ya Ngara bw. Stewart Kiondo amesema muda mfupi baada ya afisa huyo kutoka kwenye chumba cha mkutano walisikia mlio wa risasi na walipokwenda walimkuta amelala chini baada ya kujipiga risasi kwa kutumia bastola.

Amesema mwenzake huyo ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Iringa amefariki wakati alipofikishwa kwenye hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara ili kujaribu kuokoa roho yake
 
Afisa mwnadamizi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU katika wilaya ya Ngara mkoani kagera amejiua kwa kujipiga risasi kidevuni

afisa huyo bw Francis kitundu amejiua kwa kujipiga risasi leo saa nne asubuhi baada ya kutoka kwneye kikao cha ndani cha kujadili shughuli za taasisi hiyo

Mkuu wa Takukuru wa wilaya ya Ngar bw Stewart Kiondo amesema muda mfupi baada ya afis ahuyo kutoka kwenye chumba cha mkutano walisikia mlio wa risasi na walipokwenda wlaimkuta amelala chini baada ya kujipiga risasi kwa kutumia bastola

amesema mwendazake huyo ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Iringa amefariki wakati alipofikishwa kwenye hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara ili kujaribu kuokoa roho yake
Kitundu ni watu wa Iramba Singida ni wanyirama,...sio kila mtu anayejiua ni mtu wa iringa kwa kina mkwawa...kweli hao jamaa huwa wanajiua/kujinyonga etc, lakinih ata makabila mengine pia huwa yanajiua pia...huyo si mhehe ni mnyiramba kwa wale walioishi singida watakuambia.
 
huwa siamini sana mazingira ya kujiua kama haya..foensic investigation za mbele zikija kuchunguza utaambiwa kauawa na kuwekewa bastola mkononi..alitaka kumlipua na nani kwa rushwa?
 
Kwa vile ametoka huko huko wanakopenda kujiua haishangazi sana. labda amesalitiwa na mkewe. RIP Kamanda
 
Hata Mtemi ISIKE wa Tabora alijiuwa kwa kujilipua kama Mkwawa ila haina maana na yeye alikuwa mtu wa Iringa.

Kuitwa Kitundu na kuwa Mnyiramba, hakumaanishi umekuwa mwenyeji wa SINGIDA tayari.

Kuna baba mdogo wangu yupo Kamchatka miaka zaidi ya 30 na ana watoto wanaitwa Sikonge vilevile na wanaongea Kinyamwezi kwa mbaali ila wao ni WENYEJI wa KAMCHATKA na si wenyeji wa SIKONGE pale Tutuo kwa Rehani.

BTW: Nape atakuja na usemi "CHADEMA wamehusika" na yule kituko atasema "Alipata SMS kutoka kwa Dr. Slaa."
Kitundu ni watu wa Iramba Singida ni wanyirama,...sio kila mtu anayejiua ni mtu wa iringa kwa kina mkwawa...kweli hao jamaa huwa wanajiua/kujinyonga etc, lakinih ata makabila mengine pia huwa yanajiua pia...huyo si mhehe ni mnyiramba kwa wale walioishi singida watakuambia.
 
Hawa ndugu zangu wanyaru kama wajapan,bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihidimiwe amen.
 
RIP kamanda.
Nadhani tutajuzwa kwa nini kachukua maamuzi hayo ya kustaajabisha
 
Kifo hiki kichunguzwe kisipatiwe majibu mepesi eti kajiua tu.Kwanini ajiue baada ya kutoka kwenye kikao,je walikuwa wanajadili kitu gani ambacho kilimuuma hadi kumfanya ajiue.
 
Kifo kinauma lakini kujiua au 'suasaidi' kama waswahili wanavyotohoa, kunasikitisha. Hakuacha.ujumbe wowote? Maana hao watu wanafanya kaz kwa msongo mkubwa wa mawazo huku dhamiri zao zikiwasuta
 
Duh! Kilichomsibu sana ni nini?

Mi nahisi kuna jambo tu!
Poleni wote mliopatwa na msiba!
 
Kitundu ni watu wa Iramba Singida ni wanyirama,...sio kila mtu anayejiua ni mtu wa iringa kwa kina mkwawa...kweli hao jamaa huwa wanajiua/kujinyonga etc, lakinih ata makabila mengine pia huwa yanajiua pia...huyo si mhehe ni mnyiramba kwa wale walioishi singida watakuambia.

hayo mambo ya majina fulani ni ya watu wa sehemu fulani yameshapitwa na wakati mkuu, kama ni ivyo karibia wa tz wote sasa watkuwa ni watu wa ulaya na uarabuni aisee
 
Alikuwa na siri kubwa kuhusu boss wao dr.hosea kuhusu ufisadi wa jamaa na uozo wa takukuru,alikuwa kwenye mandalizi ya kumlipua Na kuanika kila kitu..police itz ur job.
 
Back
Top Bottom