Afisa wa Takukuru ajiua kwa kujipiga risasi

Francis Kitundu kajiua.

Kajiua mara baada kutoka kwenye kikao.

Kajiulia ofisini.

Kajiua muda/ saa na mahali pa kazi.

FRANCIS, mbona haijaelezwa ni wakinanani waliosikia huo mlio. Nani alikuwa wa kwanza kuingia kwa ofisi yako? Kwanini ujiue? Ni risasi ngapi zimetumika?

Maswali hayaishi....

Kajipiga risasi ya kidevu... hivi anayetaka kujiua anajipiga risasi kidevuni?
Kuna ka uwezekano kuwa akawa amekufa si kwasababu ya risasi ila kwasababu ya kutokwa damu kwa wingi, je jeraha lake lilikuwa na ukubwa gani?

Ni maswali maswali maswali.
 
Ni masikitiko kwa familia na Taifa maana lilihitaji ushiriki wake katika uzalishaji.

Nitoe angalizo; kumekuwa na ugawaji holela wa Bastola kwa raia na maofisa wa ofisi nyeti za serikali. Kwa TAKUKURU bastola imekuwa ni kifaa kama kalamu maana kila afisa Mkuu wa Wilaya anapewa. Wengi wao hawana vifua vya kuhimili hasira na wengi vidole vyao vinawashwa kuvuta "trigger" hata katika mabishano ya kawaida. Bastola mtaani zimekuwa kama Fimbo na Mwalimu wa St. Kanumba! Tuangalie upya ugawaji wa Bastola. Zitatumaliza wenyewe!
 
Afisa mwanadamizi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera amejiua kwa kujipiga risasi kidevuni

afisa huyo bw Francis Kitundu amejiua kwa kujipiga risasi leo saa nne asubuhi baada ya kutoka kwenye kikao cha ndani cha kujadili shughuli za taasisi hiyo.

Mkuu wa Takukuru wa wilaya ya Ngara bw. Stewart Kiondo amesema muda mfupi baada ya afisa huyo kutoka kwenye chumba cha mkutano walisikia mlio wa risasi na walipokwenda walimkuta amelala chini baada ya kujipiga risasi kwa kutumia bastola.

Amesema mwenzake huyo ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Iringa amefariki wakati alipofikishwa kwenye hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara ili kujaribu kuokoa roho yake

Amekosea sana, angempiga risasi jamaa wa Magogoni kabla ya kujiua.
 
iundwe tume ya kuchunguza kifo. Hicho kikao kilikuwa na nini kilichopelekea ajiue? Au karushwa fungu lake!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom