maliuogo
Member
- Jul 30, 2017
- 62
- 30
Kama nilivoeleza hapo juu, mimi ni kijana mtafutaji kwa sasa niko hapa mjini Dar, sasa kule kijijini kwetu wanyonge wanaonewa kweli wapendwa. Mama yangu mzazi anashamba lake kalima pamba kachanganya na mahindi kwenye ile pamba na amefanya hivo kwa lengo lakutaka kujiongezea kipato. Maana ana eneo dogo la kulima ndio akaamua alime mazao mawili kwenye eneo moja, lakini sasa kipindi anaanza kulima mpaka mazao yamekua hakupewa hata ushauri wowote kutoka kwa Afisa kilimo.
Sasa kinachoumiza leo hii pamba na mahindi yameanza kubeba watoto anakuja afisa kilimo wa kata na mtendaji wa kijiji kaambiwa ayatoe mahindi kwenye pamba . Mama akayatoa alipomaliza kuyatoa kaambiwa alipe kuku lasivyo wamkamate waende naye polisi. Mama kwakuwa ndio na uzee umemsogelea alipoambiwa kupelekwa polisi ikabidi awape kuku wawili ndio wakamuacha.
Sasa mimi nimeambiwa leo hii na Mama yangu alipoenda kutafuta simu kwa jirani ili anipigie .Wapendwa kwa hali hii kweli ndio tunatetea wanyonge nimeumia sana naombeni ushauri wenu.
Afisa kilimo huyu anapatikana mkoa wa Mwanza wilaya ya Misungwi, kata ya Mamaye ndio anapofanyia kazi.
Naombeni tu ushauri jamani ukiona labda nimekukwaza nishauri tu usinitukane. Ahsanteni