Afia gesti akifanya mapenzi

Afia gesti akifanya mapenzi

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,493
Reaction score
12,453
DEREVA WA HALMASHAURI IRAMBA
AFIA GESTI AKIFANYA MAPENZI


Na Nathaniel Limu, Singida

DEREVA wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida Juma Juma (52) amefariki dunia wakati akifanya mapenzi na mwanamke mhudumu wa baa kwenye nyumba ya kulala wageni. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea mei
tatu mwaka huu saa nane za usiku chumba no.S.2 nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Top Life New Kiomboi mjini. Amesema siku ya tukio,dereva Juma saa sita za usiku alimwaga mpangaji wake kuwa anatoka mara moja na hatachelewa kurudi nyumba kwa kwa hiyo alifunga mlango wa mbele ya nyumba. Amesema kuwa saa mbili baadaye Juma alionekana akiwa baa iliyoko kwenye nyumba hiyo la kulala wageni iliyoko umbali wa mita 50 kutoka nyumbani kwake. "Muda huo Juma alionekana akiwa na mmoja wa wahudumu wa baa hiyo alitwaye Agness Mayo (32) anayesadikika kuwa na uhusinao wa kimapenzi na Juma.",amesema.

Kamwela amesema mhudumu huyo wa baa mpenzi wa Juma,alitoweka mei nne mwaka huu baada ya kuaga kwamba anakwenda kanisani na kutorokea kusikojulika.Hata hivyo,ufunguo wa chumba alicholala Juma zilikutwa chumba cha kulala wahudumu wa baa. Kamanda huyo amesema kuwa toka siku hiyo ya mei tatu chumba alicholala Juma hakifunguliwa hadi mei tano mwaka huu na ndipo mwili wa dereva huyo ulipokutwa ukiwa umeharibika vibaya. "Uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta mhudumu aliyetoroka ili ahojiwe na kisha kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili endapo atabainika kuhusika na tukio hilo",amesema Kamanda Kamwela.


HIZI VIAGRA JAMANI KAMA HUJUI KUZITUMIA NI BORA UKAE NAZO MBALI
 
viagra vimefanyaje tena? c kwamba naviunga mkono,la hasha ila ripoti ya daktari inasema kuwa juma afya amefariki kwa shinikizo la damu,na habari ya viagra ilikuja baada ya maiti kukutwa kavimba sehemu za siri ndio watu wakaamini eti wamemkuta kadindisha huku amefariki tangu jana yake,kitu ambacho hakijawahi tokea popote duniani.
 
Huu upotoshaji wa habari huu!sasa kama ni viagra kwa nini afungiwe kwa ndani?kwa nini muhudumu akimbie?
 
Whilongo whilongo mwee whilongo yooooooo x2
Whilongo bhategana whilongoo yoooooooooo x2
Whilongo bhayaa mweee, whilongoo yoooooo x2

[SUB]whilongo = kaburini![/SUB]
 
viagra vimefanyaje tena? c kwamba naviunga mkono,la hasha ila ripoti ya daktari inasema kuwa juma afya amefariki kwa shinikizo la damu,na habari ya viagra ilikuja baada ya maiti kukutwa kavimba sehemu za siri ndio watu wakaamini eti wamemkuta kadindisha huku amefariki tangu jana yake,kitu ambacho hakijawahi tokea popote duniani.

Mkubwa viagra huongeza pressure sasa mtu anapokwenda kuachia dozi moyo hongeza kasi ya kusukuma damu sasa kwa umri huo 52 likely alikuwa na ka presha ukiongeza ka viagra kazi kwisha,watu wangapi wanakuwa kwa presha mkuu mbona wengi tu.
 
52 -32 = 20 years apart!!! Mwanaye wa kumzaa!!! Nguvu alikuwa nayo wapi ya kupiga K hii ambao kwa umri wa miaka 32 mwanamke ni active kama pilipili mbuzi!!! Aende anakostahili.
 
Mkubwa viagra huongeza pressure sasa mtu anapokwenda kuachia dozi moyo hongeza kasi ya kusukuma damu sasa kwa umri huo 52 likely alikuwa na ka presha ukiongeza ka viagra kazi kwisha,watu wangapi wanakuwa kwa presha mkuu mbona wengi tu.
mkuu mm cjaona logic ya ww kung'an'gania viagra,wakat tunamtoa chumbani alikua kavimba sana ikiwa ni pa1na sehemu za siri,kule kuvimba kwa sehemu za siri ndio watu wakasema kuwa amekufa huku uume umesimama na kusimama kule kunatokana na viagra,mkuu mi naamini we unajua kitaalamu ni nini kinachopelekea uume usimame je ukifa uume utaendelea kusimama ht baada ya siku mbili?
 
Back
Top Bottom