Afande Sele: Lazima CHADEMA Itashainda Morogoro

Afande Sele: Lazima CHADEMA Itashainda Morogoro

Selemani Msindi (Afande Sele) Jumamosi hii, akihutubia mamia ya wananchi wa Kata ya Kichangani, jimbo la Morogoro Mjini, aliwahakikishia wanachi, kama watashikamana na kusiliza maneno ya busara yanayotolewa na viongozi wa CHADEMA, basi lazima CHADEMA itachukua madiwani wengi na nafasi ya ubunge, Jimbo la Morogoro Mjini. Alieleza sababu za wanamziki wenye upeo mkubwa kuingia katika siasa, kwamba wanasiasa wameziba masikio na hawataki kusikiliza jumbe zao kupitia muziki. Kabla ya kupanda jukwaani alikanusha kabisa, kushiriki katika kuikosoa kamati kuu ya CHADEMA na maamuzi yake, kwani yeye anaipenda CHADEMA, Muundo wake, Katiba na vikao vyake, na hana muda wa kuzungumza mambo yaliyowekwa katika mitandao, yakimhusisha na kauli zisizo za kweli, eti kwamba analaani uamuzi wa kamati kuu. Alisema hizo ni njama zinazopangwa kumchonisha na chama anachokipenda, na kamwe hazitafanikiwa. Kazi imeanza na sasa hakuna kulala mpaka kieleweke. Angalia picha hapa chini.

Kama kweli hakuyasema yale maneno ya kuipinga kamati kuu kuhsu maamuzi yake basi kuanzia leo ninamsamehe maana nilikua nimemchukia sana hata kufikia miziki yake kuifuta kwenye computer yangu.
 
Kama kweli hakuyasema yale maneno ya kuipinga kamati kuu kuhsu maamuzi yake basi kuanzia leo ninamsamehe maana nilikua nimemchukia sana hata kufikia miziki yake kuifuta kwenye computer yangu.
Hilo nalo neno.
 
Back
Top Bottom