AFANDE MWEMA!!! Aibu hii ya mauaji polisi itakwisha lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AFANDE MWEMA!!! Aibu hii ya mauaji polisi itakwisha lini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 13, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,429
  Likes Received: 5,688
  Trophy Points: 280
  Aibu hii ya mauaji polisi itakwisha lini?
  HIVI karibuni kumekuwapo habari za mauaji ya raia yanayofanywa na askari polisi wa vituo mbalimbali nchini.

  Hili linathibitishwa na tukio la jana lililoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu mauaji ya dereva teksi wa Kituo cha Kariakoo, Mussa Juma.

  Kwa mujibu wa habari hizo, Juma alifikwa na mauti hayo akiwa katika Kituo cha Polisi ChangÂ’ombe alikoshikiliwa kwa tuhuma za kuhusika katika ujambazi. Mtuhumiwa huyo alikufa wakati akihojiwa na askari.

  Aidha, kutokana na kifo hicho, jeshi hilo Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, chini ya Kamanda Alhaji Suleiman Kova, limeanza uchunguzi wa kina unaohusisha jopo la madaktari ili kubaini sababu za kifo hicho.

  Kwa kauli ya Kamanda Kova, marehemu huyo alikamatwa baada ya kuhusishwa na tukio la ujambazi lililotokea maeneo ya Mbozi Road, ChangÂ’ombe wiki tatu zilizopita, akiwa kwenye teksi yenye namba za usajili T 227 AFF.

  Inaelezwa kuwa wakati anahojiwa, marehemu alilalamika kuwa na maumivu ndipo askari waliokuwa wakimhoji waliamua kumchukua na kumpeleka Hospitali ya Temeke kwa matibabu.

  Hii si mara ya kwanza kwa wananchi hususan wakazi wa Dar es Salaam kusikia taarifa za mauaji ya aina hii yanayohusisha askari polisi na raia.

  Kwetu mauaji ya aina hii yanatulazimisha kuamini kwamba ndani ya jeshi hilo wapo watumishi wasiofahamu maadili ya kazi zao, kwa sababu kitendo cha mtuhumiwa kufariki dunia mikononi mwa polisi, hutokana na kipigo.

  Hivi ni sheria gani ya nchi inayompa mamlaka askari polisi kumpiga mtuhumiwa wakati anahojiwa? Tunafahamu kwamba wakati wa kutoa maelezo, lazima mtuhumiwa awe na mtu anayemwamini kwa ajili ya kusikia anachokieleza kwa polisi.

  Si hivyo; bali ni lazima mtuhumiwa atoe maelezo anayoyafahamu kwa uhuru na uwazi bila kushinikizwa kwa njia yoyote ile.

  Tatizo la kulazimishwa kwa kutumia kipigo linasababisha asilimia kubwa ya watuhumiwa wanaofikishwa mahakamani, kuyakana maelezo hayo.

  Tunasikitishwa na Jeshi letu la Polisi, kwao ili kupata maelezo ya mtuhumiwa ni lazima wampige na kumtesa kadiri wawezavyo bila kujali kwamba kufanya hivyo ni kudhulumu haki ya mtuhumiwa.

  Wengi wanaolazimishwa kutoa maelezo kwa kipigo wanakubali makosa wasiyoyatenda ili kuepukana na kipigo cha polisi. Tu - mashuhuda wa hiki tunachoandika. Ukitaka kuamini, fika mahakamani wakati mtuhumiwa akisomewa maelezo aliyoyatoa kituo cha polisi.

  Tunaamini dhima ya jeshi hilo ni kulinda raia na mali zao. Kinachotokea sasa ni raia kuwaogopa polisi, hali inayoweza kukwamisha shughuli za polisi jamii na kusababisha upotevu wa amani.

  Sisi Tanzania Daima tunachukua fursa hii kulaani matendo haya na kuwaomba wakuu wa jeshi hili kuwaonya askari wao wanaokatisha uhai wa nafsi za watu wanaotuhumiwa kwa kipigo waache, vinginevyo watawalazimisha wananchi kuwachukia polisi ambao wengi tunaishi nao uraiani.
   
Loading...