advocate mwale ahofia maisha yake akiwa mahabusu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

advocate mwale ahofia maisha yake akiwa mahabusu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Jackbauer, Mar 21, 2012.

 1. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  advocate huyu ambaye anashikiliwa katika mahabusu ya gereza la kisongo aliyasema hayo leo katika muendelezo wa kesi inayomkabili.
  Amedai mawakili wa serikali humfuata mara kwa mara na kutaka kumpeleka pasipojulikana.
  Ametoa taarifa hii ili kumbukumbu za mahakama ziwepo iwapo jambo baya litamtokea.
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Hivi bado hajatoka tuu huyu ndugu
  Duh balaa
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kesi inaendelea mkuu.
   
 4. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu jack hebu fanya uni update zaidi kuhusu huyo advocate maana sielewi chochote.
   
 5. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,546
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  hiyo kes siyo mchezo
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280

  Haina dhamana mkuu hii kesi yako au ni zile za money laundering
   
 7. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,546
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  hii kesi imesababisha paka yule meneja wa benki ya CRDB (meru branch) asimamishwe kazi.
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ameomba mali zake zinazoshikiliwa na polisi na TRA kuachiwa.
   
 9. K

  Kuchayaa Senior Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu jamaa nasikia alikutwa na B-kadhaa kwenye account yake, ilikuwa na big issue mpaka wale undercover brothers(CIA) walikuja hapa kumchunguza, inasemekana alikuwa na ile fedha chafu ya wale jamaa waliolipua ubarozi wa US hapa nchini na lile jengo la world trading centre.Sheeeeee quite, usije ukasema mimi ndio nimekuambia!
   
 10. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  imehusishwa na ufadhili wa alshabab
   
 11. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,930
  Likes Received: 1,462
  Trophy Points: 280
  yeah,wanasema ni mmoja wa wana mtandao alshabab! Lakini pia hata moja ya nyumba zake wanaingia wasomali kila kukicha!
   
 12. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ndio yule aliyekuwa na 20m kama pocket money?
  Kwani hajui hao state prosecutors wanataka nini?
  Changamka dogo, utafia humo ndani.
   
 13. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Wamesha kusikia wamo jf.
   
 14. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,546
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  mbona hamna cha kuficha ?
   
 15. c

  carefree JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  jukwaa lina heshima yake hili jaribu kuingia na upate ukweli wa kesi hii , fedha hizo hazikukutwa kwenye account yake hata shilingi moja zimekutwa kwenye akaunti za watu aliwahi kufanya nao biashara ya madini ya tanzanite kupitia kampuni ya familia yao ndiyo sababu mpaka sasa unaona hakuna kinachoendelea mahakamani
   
 16. c

  carefree JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]Mahakama yaamuru Wakili Mwale apewe mali zake
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Arusha imewaagiza Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DPP), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha kuyarudisha magari saba na simu za mkononi kwa Wakili maarufu mkoani Arusha, Mediam Mwale, anayetuhumiwa kupatikana na fedha chafu.
  Akisoma hukumu hiyo katika kesi hiyo ya jinai namba 330/11 wiki iliyopita, Hakimu Mkazi Mfawidhi Charles Magesa, alisema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote, mahakama imeridhika kuwa mamlaka hizo zilikamata magari hayo kinyume cha sheria ya matunda ya uhalifu (Proceeds Crimes Act) pamoja na vifungu namba 41 na 44 vya sheria ya mwenendo wa kesi za jinai.
  "Ukamataji huo ni kinyume cha sheria kutokana na kitendo cha upande wa mashitaka cha kukamata magari hayo, hivyo mahakama inaamuru kuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa TRA nchini na Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha ambao walihusika katika zoezi la ukamataji kuhakikisha wanayarudisha yote kwa mshitakiwa nyumbani kwake walikoyachukua," alisema hakimu huyo.
  Magari ambayo mahakama hiyo iliamuru kurudishwa nyumbani kwa mshitakiwa ni T 690 BEW aina ya Range Rover, T 643 BTS Land Rover Discovery, T 907 BTS BMW, T 118 BRS Cadillac Escalade, T 499 APX Land Cruiser, T 520 BBJ BMW, ambayo yalichukuliwa Novemba mosi pamoja na gari T 660 BCG Toyota Chaser lililokamatwa Desemba 8, mwaka jana.
  Mwale ambaye yupo rumande katika gereza kuu la Mkoa wa Arusha la Kisongo nje kidogo ya Jiji la Arusha kutokana na kesi inayomkabili kutokuwa na dhamana, alitoa malalamiko mahakamani hapo Desemba 20 mwaka jana na kumtaja ofisa mmoja wa Polisi, Selemani Nyakulinga, kwamba alifika nyumbani akiwa na wenzake na kuchukua magari hayo bila amri ya mahakama.
  Aliieleza mahakama kuwa baada ya magari hayo kuchukuliwa yalipelekwa ofisi ya TRA Mkoa wa Arusha bila kuwapo sababu za kilichopelekea magari hayo kukamatwa, hivyo kuiomba mahakama hiyo kutoa amri ya kuachiwa kwani yalikamatwa kinyume cha kifungu namba 28 cha sheria ya kudhibiti fedha chafu na kifungu namba 24 cha Sheria ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
  Kufuatia malalamiko hayo, Wakili wa Serikali Neema Ringo, aliiomba mahakama kuahirisha shauri hilo ili aweze kufanya utafiti kuhusiana na malalamiko ya mshitakiwa na zaidi awe katika nafasi nzuri ya kujibu.
  Mahakama ilikubali ombi hilo na kesi hiyo ilipangwa kuendelea tena Januari 5 mwaka huu. hata hivyo siku hiyo ilipowadia mawakili wote wa serikali wanaoendesha kesi hiyo hawakutokea mahakamani isipokuwa wakili mmoja tu.
  Wakili huyo wa serikali aliitaarifu mahakama hiyo kuwa mawakili hao wameshindwa kufika baada ya kukabiliwa na majukumu mengine, hata hivyo mahakama hiyo haikuridhika na sababu hiyo, hivyo kupanga kutoa uamuzi Januari 19, mwaka huu.
  Hata hivyo, Januari 19 Hakimu Magesa anayesikiliza kesi hiyo hakuwepo na kesi iliahirishwa hadi Januari 31 mwaka huu ambapo pia hakimu huyo hakuwepo na kesi kuahirishwa hadi Februari 22 mwaka huu ambapo upande wa mashitaka ukiongozwa na Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Bibi Mlay ulitoa utetezi wake kwa barua, ambapo uliieleza mahakama kwamba magari hayo hayakuchukuliwa na Polisi bali na maofisa wa TRA kuhusiana na masuala ya kodi.
  Alisema kuwa kuwapo kwa maofisa wa polisi wakati wa zoezi hilo kusimfanye mshitakiwa kudhani kuwa ndio waliochukua magari hayo bali walisimamia uchukuaji. Alijitetea kuwa gari namba T 520 BBJ lilikabidhiwa kwa wakili wa mshitakiwa Agosti 18, 2011 na kuhusu simu za mshitakiwa alisema kuwa hazikurejeshwa kwake kwa sababu zilipelekwa kwenye kitengo cha polisi cha uchunguzi.
  Hata hivyo Hakimu Magesa katika hukumu yake hiyo aliileza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa aliitaarifa mahakama kwamba alituma ndugu zake TRA kuulizia kuhusu magari yake ambapo ndugu zake walitaarifiwa na maofisa wa TRA kwamba magari hayo yalikamatwa kwa maagizo ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) E.S.A. Mmari, kwa barua yake ya Desemba 15, mwaka jana na ndugu wa mshitakiwa walipatiwa nakala ya barua hiyo.
  Aliongeza kuwa ni muhimu kuelewa awali kabla kwamba mshitakiwa bado ni mtuhumiwa tu na mtu asiye na hatia hadi hapo itakapothibitishwa vinginevyo na upande wa mashitaka, hivyo anapaswa kutendewa kama mshitakiwa na si kama mtu aliyetiwa hatiani.
  "Hoja kubwa ni kwamba magari yake pamoja na ya marafiki zake yamekamatwa na kuchukuliwa bila kuzingatia sheria, na makosa ambayo mshitakiwa ameshitakiwa nayo yapo chini ya sheria ya udhibiti wa fedha chafu ya 2006 na kifungu namba 28 cha sheria hiyo kinaeleza kwamba utaratibu wa kukamata, ukusanyaji taarifa, utaifishaji au ukamataji na udhibiti wa mali utakuwa kama ulivyo chini ya sheria ya matunda ya uhalifu (Proceeds Crimes Act & The Criminal Procedure Act 1991).
  "Sheria hiyo ya matunda ya uhalifu ya mwaka 1991 inatoa utaratibu wa namna ya mali ya mtu aliyotiwa hatiani au aliyeshitakiwa na makosa yanayohusiana na sheria hiyo itakavyokamatwa…kifungu muhimu katika sheria hiyo ni kifungu namba 31 (1)" aliieleza mahakama.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 17. K

  Kowakdengo Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kesi hii ilitungwa kwa chuki binafsi baina ya mawakili wakishirikiana na Mombo wa usalama wa Taifa sasa inaanza kuwaelemea wanatafuta namna ya kumdhuru
   
 18. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nyaga hausiki kweli!
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Nasikia haka kakesi ni kabaya!
   
 20. vaspanya

  vaspanya Member

  #20
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mm nimemuona mke wake last week akiwa anaendesha hiyo escallade..Pia kuna hela zimetolewa karibu 200m kwa ajili ya kuhonga na hyo kesi sasa hivi ni danganya toto. Na waliopeleka hiyo hela dar nawafahamu kwa sura na majina. mmoja wao ni dalali maarufu sana arusha ambaye naye ni shabiki mzuri wa magari ya kifahari, ana gari lake moja aina ya HYUNDAI arusha analo peke yake. Initials za majina yake ni C.L
   
Loading...