martial jb
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 864
- 1,463
Habari wakuu,
Leo nimepitia moja ya mkakati wa serikali kuhusiana na mabadiliko ya kielimu nchini, na nikaona suala la kunufaisha mikopo wanafunzi wa ngazi ya Stashahada (Diploma), ni moja ya mabadiliko yanayokwenda kutokea hapo mbeleni.
Kutokana na maelezo ya serikali inasemekana ngazi ya stashahada inauhitaji zaidi na pia ina haki sawa ya kunufaika na mikopo kama ilivyo kwa ngazi ya Shahada (Degree).
Kitu kinachozunguka kichwani mwangu ni swali la je, Advanced level itakuwa na mvuto tena kwa wanafunzi ikiwa mikopo hii itaanza kugawiwa. Maana kwa mpaka sasa tayari ngazi hiyo imeshakosa mvuto kwa watu wengi juu ya kusemekana ni ngumu na haimuandai mwanafunzi na taaluma yeyote.
Sasa mikopo ya Diploma ikianza si ndiyo itakufa kabisa, kuna mtu atakayeacha pesa na kwenda kujitesa huko Advance?