Advanced Diploma: Ni Digrii ama nini?

Pengine wizara ingelitolea maelezo hili nalo. Maana wana-Advanced Diploma wamepata wasiwasi sana
 
Wadau tafadhali msaada nimekutana na wahitimu wanaodai wana Vyeti vinaitwa Advanced Diploma nataarifiwa "eti" kuna sehemu wanalinganisha na shahada ya kwanza ya Chuo kikuu. Tafadhali mwenye ujuzI anijuze. Samahani lakini.
Mimi nilichokuwa najua ni kuwa Mwanafunzi anayesoma Adv Dipl anakuwa amekosa sifa sitahiki kimax za kuingia chuo kikuu, kwahiyo anasoma hiyo na akimaliza anaingia chuo 2nd year.
 
Mr(s) roho mbaya mwaga details hao advanced diploma kwa nn unawapenda!
Dah...naona Mr itanifaa zaidi... nipo kwenye field ya engineering design kwa muda kidogo... waliosoma advanced dip wako vizuri zaidi....mawazo mapana.... good reasoning....wanaelewa upesi sana kuliko hao wengine....hii nadhani kwa sababu wengi wao wameanza kuwa na misingi ya engineering mapema...wengi wao wamesoma technical secondary school...wakaenda technical college....ni wazuri kwa kweli...wamebeba tools za kutosha vichwani mwao kuliko hao wengine....wako tayari kufanya kazi haraka zaidi kuliko wengine....fikiria kwa uchunguzi wangu nilibaini wale wa advanced dip huenda field training mara 5 wakati wale wengine huenda mara 3 -4 wakati wa masomo yao.....unaweza kuwauliza waliosoma advanced kitu muhimu sana...wa nne kati ya watano wakakuelewa....lakini kitu hicho hicho ambao hawakusoma advanced dip wote wasikijue kabisa...
 
Mr. Rohombaya umepitia malengo/objectives za university education in Tanzania. Nijuavyo mimi Bachelor degree holders hawaandaliwi kuwa mafundi "mchundo" bali ni kuwaongoza hao jamaa ZOOM/VETA.
 
Mimi nilichokuwa najua ni kuwa Mwanafunzi anayesoma Adv Dipl anakuwa amekosa sifa sitahiki kimax za kuingia chuo kikuu, kwahiyo anasoma hiyo na akimaliza anaingia chuo 2nd year.
Dah... Basi ajabu sana...nilifuatilia mitaala yao....kinachosomwa na watu wa advanced kwa mwaka mmoja husomwa na wengine hasa BSc Eng kwa miaka karibu miwili
 
Dah....mimi binafsi waliosoma advanced dip ya engineering Tz nawapendelea zaidi.....wanakitu cha ziada zaidi dhidi ya waliosoma BSc Eng au B Eng....
Nishasikia aliesoma engineering DIT ni bora kuliko wa UDSM,ss sijui ni kweli
 
Mimi nilichokuwa najua ni kuwa Mwanafunzi anayesoma Adv Dipl anakuwa amekosa sifa sitahiki kimax za kuingia chuo kikuu, kwahiyo anasoma hiyo na akimaliza anaingia chuo 2nd year.
Siyo kweli. Zamani Mzumbe, UCLAS(sasa Ardhi University), DIT,IFM,DSA(sasa TIA) nk kadhalika zilitoa wahitimu wa katika ngazi hiyo ya Elimu. Wengi wa Architects,Quantity Surveyors ambao ni product ya UCLAS ambao kwa sasa ni Senior Officers walipata elimu hiyo. Pia wengi wa Engineers wa zaman kutoka DIT, MIST-sasa MUST, pia wengi wa ile IDM mzumbe ambao ni watawala walipata level hiyo ya elimu. Ina content za masomo ambayo ni sawa na degree, lakini hasa wakati huo ilitumia Term na siyo Semester hizi tuzijuazo. Hivyo itoshe tu kusema, mtu mwenye Advanced Diploma ni equivalent na degree, na mimi nasema reverse is true. Huna utakachomshinda katika kujua mambo ya fani au taaluma husika. Ila naona Form Six kuita ni equivalent, naona inanipa shida kidogo, kwa sababu Form six amesomea nini cha kumpa ujuzi? Anasoma sawa na Form4 tu ili afaulu aende akasomee ujuzi, wakati Diploma ni equivalent na Form Six hasa kwa ukweli kwamba hesabu zake hasa kwa upande wa Diploma ya Uhandisi hesabu zake ni sawa au zaid ya zile za kidato cha sita.
 
AdvanceD Degree ianzishwe ili iwe equivalent na masters. Watanzania tuache short-cut.
 
Back
Top Bottom