Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Projectile motion, dynamics, wave sijui na nini nini huko mi kwangu sikupata navyo shida sana lakini nilikuja kujuta na mziki wa HEAT.
Kama kuna topic imenitesa kwanye physics toka nipo o'level basi Heat sikuwahi kuiweza na ilinipa joto kweli kweli.
 
Wakati tunakwenda kwenye Umisseta wanafunzi wa Advanced wa PCM walikua wanatushangaa sana kuona tunasolve haya madudu;
Projectile,Angular Motion,Electromagnetism,Friction Force (ile Deep) n.k
Ukijaribu kupima ugumu huo ww ukiwa form five au Six pima ukiwa form three na form four!

Titcomb (Fundamental of Engineering Science) ndio kitabu pekee nitakiheshimu sana.
 
Mi mwenyewe form six ikawa bye bye na chuo nikasoma vitu vingine kabisa. Japo I regret kwanini sikwenda kusoma hata Civil engineering ila ndo basi tena.
Ha ha ha for my side am not regretting ki ukwel fact that am happy with what i went to per sue in univ tho nikiwaona pilots nataman, Revenge yangu ikawa lazma niwe abiria wao mara kwa mara
 
Namkumbuka yule TO alitoka Tosa Boys miaka ile halafu akafukuzwa chuo. Dah jamaa alikua mtukutu sana second master alikua anamtafuta sana hampati hata bwenini hapatikani wala darasani. Alivokuja kuwa TO ndio akapata heshima....
 
"Measurements and error" ilikuwa topic ya kwnza kwenye A level Physics, hii ilifanya mwalimu wetu wa Physics tumpe jina la utani "An Error".
 
Khaaa sitasahau physics ya advance ndo ilinifanya nikaachana na mambo ya science !!!!!
Nakumbuka olevel phy A kichwa ndo mimi uniambie nini nikusikilize hapo hata masomo ya arts nilikuwa sisomi madai marahisi hapo history ilishanishinda kabisa ila kwakuwa nilikuwa kipanga wa science walimu wote walikuwa wananisikiliza nakumbuka enzi hizo form three pepa langu la phy ndo ilikuwa markn scheme hahahahaha
Mziki ukaja advance sasa test ya kwanza phy nikapata 22% nilichanganyikiwa nikamwambia mzee ndo akanitia moyo adv ni ngumu soo nikaze nikakomaa nikarudi katika mstari hadi mock nikawa wa 2 kimkoa .....

Sitosahau siku ya necta mtihan wa practical !!!!! Kwa bahati mbaya nikapangiwa prat B sababu A walipangiwa pcb , daaah practical ilikuwa ngumuuuuuu yaaani vitu havibalance kabisa rula zinabinuka tuu aisee hii siku hadi nikaumwa ndani ya lab ....tokea siku hiyo nikasema mimi science basi huu ujinga sitak kuusikia tena huo ndo ukawa mwisho wangu na mambo sayans nikasema if there’s other life apart frm science letm go for it ,thu nilifaulu vizur ila chuo nikaingia zangu business sikutaka tena stress za kujitakia bora kupambana na makabati tuu !!!!
 
Back
Top Bottom