Adui hatari nambari wani wa taifa letu Tanzania ni CCM, je unaafiki?

Hoja hii imeungwa mkono.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Upuuzi wa chadema ni kubrainwash vijana kwamba wao ni wapigania haki wakati wengi wao ni wapigania tumbo.
Kaka pembe, hebu ongezea nyama kidogo, ni kwa namna gani Chadema hawapiganii haki na badala yake wanapigania tumbo?

Unaweza kuwataja hao Chadema wanaopigania tumbo na namna wanayotekeleza harakati hizo za kupigania tumbo? Ninavyosikia hawaruhusiwi hata kukutana na wakijaribu, polisi huwakamata, kuwatupa selo na kuwafungulia mashtaka!

Mwagika tu ndugu yangu, hii ni JF tunapomkoma nyani ngeledi bila kumtazama uso. Hiyo nafasi ya kupigania tumbo wanaipataje huko korokoroni?
 
Mwinyi aliingia na yake, Mkapa akaingia na yake, Kikwete akaingia na yake, Magufuli kaingia na yake na sasa Mama naye kaingia na yake lakini washiriki bado ni wale wale na nyumba inayonuka bado ni ile ile. Baada ya kupoteza mvuto kwa wananchi, ikaamua kung'ang'ania madaraka kwa ulaghai na matumizi ya nguvu...hata hivyo la kuvunda halina ubani!

View attachment 1920398

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
wabongo nimewanyooshea mikono
 
Nakiri kuwa sijawahi kuishabikia CCM hata kwa bahati mbaya. CCM ni chafu na inanuka. Siwezi kuishi kwenye nyumba inayonuka, nikijifunika blanketi moja na wanaonuka, nikikesha na wenzangu wanaonuka halafu nidanganye umma kwamba sinuki. Kuwa mwanachama wa CCM maana yake ni kwamba huo uvundo haukusumbui, unauona kama marashi ya Pemba.

Kuwa mwanachama wa CCM ni hatua ya kwanza katika kulisaliti taifa kwa kukubaliana na tulipokuwa, tulipo na tunakoelekea. Hata mwenyekiti muasisi wa CCM, Baba wa Taifa, alishindwa kuvumilia huo uvundo na kutishia kujitoa kama juhudi za makusudi hazikufanyika kukisafisha chama kilichoonekana wazi kabisa kukosa dira lakini masikini, hata yeye akapotezwa?

Niliipinga CCM kabla ya mfumo wa vyama vingi, nikaendelea kuipinga baada ya mfumo mpya na nitaendelea kuipinga hadi itoke madarakani. Hii ni kwa sababu ninaamini kwa dhati kabisa kwamba chama ambacho kwa muda zaidi ya nusu karne haikuweza kutuopoa katika lindi la ujinga, maradhi na umasikini, imechoka, imezeeka na haina uhalali wowote wa kubaki madarakani.

CCM inaamini katika kuhodhi kila kuhodhi uhai, kuhodhi nchi, kuhodhi uraia, kuhodhi Katiba, kuhodhi utawala, kuhodhi haki (mahakama), kuhodhi madaraka, kuhodhi fikra, kuhodhi hoja (bunge), kuhodhi akili na kuhodhi hata ujinga! Naam, ukianza kuhodhi kila kitu, umekuwa sawa na kokoro na si ajabu kuhodhi hadi ujinga! Angalia ilipofikia CCM imehodhi hadi ulevi wa madaraka!

Mwinyi aliingia na yake, Mkapa akaingia na yake, Kikwete akaingia na yake, Magufuli akaingia na yake na sasa Mama naye kaingia na yake lakini washiriki bado ni wale wale na nyumba inayonuka bado ni ile ile. Baada ya kupoteza mvuto kwa wananchi, ikaamua kung'ang'ania madaraka kwa ulaghai na matumizi ya nguvu, hata hivyo la kuvunda halina ubani na mwisho wake hauko mbali.
Mkuu 'Mag3', wahenga husema kulitambua tatizo ni mwanzo wa ufumbuzi wa tatizo hilo.

Ni mara nyingi sana nimepiga kelele nyingi humu JF, watu watambue adui hasa wa nchi yetu kwa wakati huu ni nani, lakini watu ni wazito sana kuondoa mawazo yao kwa watu, kama mwenyekiti wa chama hicho kuwa ndiye adui yao mkubwa, wanasahau kwamba ni chama anachoongoza ndiye adui mkubwa wa taifa letu. Tofauti hapa atakuwa Magufuli, kwa sababu wakati wake Magufuli ndiye alikuwa CCM na CCM ikawa ndiye Magufuli.

Kwa hiyo ukitaka kuleta mabadiliko, ni lazima utambue ni nani hasa unayehitajika kupambana naye ili upate mafanikio unayotafuta.

Kwa hiyo, sasa tukitambua kwamba CCM ndiye adui, ni lazima tujue ndani ya CCM hiyo, ni watu gani hasa wanaoshikilia na kuendesha chama hicho kiendelee kutuletea madhara. Kuna kundi maalum, ndani ya chama hicho, kundi la watu wasiosikika wala kuonekana jinsi wanavyokiendesha chama hicho kuendelea kuleta maumivu kwa wananchi. Watu hawa hawasiskiki lakini matendo yao ndiyo yanayoleta matokeo tunayoyaona.

Ni watu hawa ndio wanaong'ang'ania pasiwepo na katiba mpya na mambo mengine yasiyoliletea tija taifa letu. Mwenyekiti anacgukua maamuzi yao na kuyatangaza. Ndiyo maana wengi hudhani mwenyekiti ndiyye mwamuzi ya haya mambo yote.

Kwa hiyo basi, katika kutafuta mbinu za kupambana na adui huyu, ni lazima kuwatambua hawa watu wachache walioko huko ndani ya CCM. Watu hawa inatakiwa wajulkikane kwa wananchi kuwa ndio kikwazo kikubwa katika mabadiliko yanayohitajika. Watu kama Mizengo Pinda, ndio wanaoishikilia CCM iendelee kuleta madhara makubwa kwa nchi yetu.
 
Siyo Magufuli tena?

Mimi nilifikiri mbaya wetu hii nchi ni Magufuli, na hata zile shangwe za wana chadema baada ya kifo chake nilifikiri sasa mtajiona mko Newyork!

Mmakwama wapi mabavicha?
Wakati wake CCM haikuwepo. Kwa hiyo isingewezekana kuilaumu CCM badala ya kumlaumu Magufuli ambaye aliitwaa CCM.
 
Nakiri kuwa sijawahi kuishabikia CCM hata kwa bahati mbaya. CCM ni chafu na inanuka. Siwezi kuishi kwenye nyumba inayonuka, nikijifunika blanketi moja na wanaonuka, nikikesha na wenzangu wanaonuka halafu nidanganye umma kwamba sinuki. Kuwa mwanachama wa CCM maana yake ni kwamba huo uvundo haukusumbui, unauona kama marashi ya Pemba.

Kuwa mwanachama wa CCM ni hatua ya kwanza katika kulisaliti taifa kwa kukubaliana na tulipokuwa, tulipo na tunakoelekea. Hata mwenyekiti muasisi wa CCM, Baba wa Taifa, alishindwa kuvumilia huo uvundo na kutishia kujitoa kama juhudi za makusudi hazikufanyika kukisafisha chama kilichoonekana wazi kabisa kukosa dira lakini masikini, hata yeye akapotezwa?

Niliipinga CCM kabla ya mfumo wa vyama vingi, nikaendelea kuipinga baada ya mfumo mpya na nitaendelea kuipinga hadi itoke madarakani. Hii ni kwa sababu ninaamini kwa dhati kabisa kwamba chama ambacho kwa muda zaidi ya nusu karne haikuweza kutuopoa katika lindi la ujinga, maradhi na umasikini, imechoka, imezeeka na haina uhalali wowote wa kubaki madarakani.

CCM inaamini katika kuhodhi kila kitu…kuhodhi uhai, kuhodhi nchi, kuhodhi uraia, kuhodhi Katiba, kuhodhi utawala, kuhodhi haki (mahakama), kuhodhi madaraka, kuhodhi fikra, kuhodhi hoja (bunge), kuhodhi akili na kuhodhi hata ujinga! Naam, ukianza kuhodhi kila kitu, umekuwa sawa na kokoro na si ajabu kuhodhi hadi ujinga! Angalia ilipofikia CCM imehodhi hadi ulevi wa madaraka!

Mwinyi aliingia na yake, Mkapa akaingia na yake, Kikwete akaingia na yake, Magufuli akaingia na yake na sasa Mama naye kaingia na yake lakini washiriki bado ni wale wale na nyumba inayonuka bado ni ile ile. Baada ya kupoteza mvuto kwa wananchi, ikaamua kung'ang'ania madaraka kwa ulaghai na matumizi ya nguvu, hata hivyo la kuvunda halina ubani na mwisho wake hauko mbali.
Naafiki 100%
 
Hata Ndugai nae kaja na yake......Mwenyeji wa Galilaya,Kapernaumu,Nazareth na Bethlehemu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom