Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema chama hicho kipo tayari kuwapokea wanasiasa kutoka vyama vingine na kitawapokea kwa heshima ya hali ya juu pindi watapokuwa tayari.
Akizungumza katika mahojiano maalum aliyofanya na Jambo TV Ado, amesema kuwatengeneza baadhi ya hao wanasiasa hasa wanawake sio kazi rahisi hivyo kwa chama chao kuwapata inakuwa ni thamani imeongezeka kwao.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Katika mahojiano hayo amemtaja wanasiasa mashuhuri kama Halima Mdee, Esther Bulaya, Esther Matiko na Catherine Ruge ambao wamejitengenezea majina katika kipindi walichohudumu katika siasa za upinzani.
"watu wa aina hii wakitaka kuja ACT Wazalendo sio kwamba tu tuwapokea, tutawapokea kwa kishindo kinachoendana na heshima yao kwa hiyo tunawakaribisha sana" amesema Ado.
Hata hivyo amesema ni vyema wanasiasa hao wakawachukua kuliko wakaichezea nafasi halafu wakachukuliwa na Chama cha Mapinduzi CCM.