Ado Shaibu amshtaki Rais Magufuli Mahakama Kuu kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Kilangi ni Kilaza sana,Ameteuliwa kikabila (MSUKUMA MWENZETU) kama ikivyo wakuu wa idara zote ni wsukuma wenzetu na hakuna anayehoji ila wachagga ambao hawakuwa raisi,wala waziri mkuu,wala makamo wa raisi haijatokea mchaga wanalaumiwa kushika madaraka na kupendeleana.

Tangu kupata uhuru,NYERERE,MWENYI,MKAPA,KIKWETE,WARIOBA,MSUYA,KARUME,SUMAYE,MALECHELA,LOWASSA,MAJALIWA ,POMBE wote hakuna mchagga lakini watu wanalia wachaga wanapendelewa na huyu wa sasa ameamua kuwakomoa kuanzia kwenye siasa,ajira,teuzi zake .
Hajateua :-
Waziri yeyote toka Kilimanjaro.

Hajateua Balozi toka Kilimanjaro

Hajateua Kamishna yeyote mambo ya usalama toka kilimanjaro.

Hajateua Mkurugenzi yeyote wa Bodi toka Kilimanjaro na hawa madokta kila siku anateua anawapiga chini wote toka kilimanjaro.


Kumbuka Wachaga ni wapambanaji,Mwaka huu wamevunja rekodi ya mwka 2000. Wanarud Moshi kwa wingi kwenda kutoa sadaka za shukrani na pia kuelezea wakichokuwa wanafanya mjini.

Wanakabidhiwa majukumu mapya ya kusomesha wadogo zao na ndugu wasio jiweza.

Wanandaliwa kisaikolojia kwa chuki dhidi yao na sasa wanajua la kufanya,KWA KIFUPI HAWANA TOFAUTI NA TAIFA LA ISRAELI NA HUYO MTESI WAO NI FARAO ambaye baadae ataishia kama farao
Hujielewi wewe!!!!!

Unacholalamikia nawewe unacho na umethibitisha katka uandishi wako yaani unalalmika wachagga wamesahaulika hv labda mie sjui kwan wwchagga ni wa Kilimanjaro tu????? Koz unawatetea wa Kilimanjaro tu utafkr ndo wqchaaga pekee... Ati unasema ww msukuma popoma kweli!!!

Ukidai wa Kilimanjaro wateuliewe halafu hutaji wa maeneo mengne basi ww mkabila mkubwa saana koz unahangaika kutetea utokako mbuuuuzi ww
 
Limekuwa jambo la kawaida mtu akipewa uongozi anakamata katiba kuwa atailinda, muda si muda analikoroga.
Mi nawahi seat ya mbele.
 
Kilangi ni Kilaza sana,Ameteuliwa kikabila (MSUKUMA MWENZETU) kama ikivyo wakuu wa idara zote ni wsukuma wenzetu na hakuna anayehoji ila wachagga ambao hawakuwa raisi,wala waziri mkuu,wala makamo wa raisi haijatokea mchaga wanalaumiwa kushika madaraka na kupendeleana.

Tangu kupata uhuru,NYERERE,MWENYI,MKAPA,KIKWETE,WARIOBA,MSUYA,KARUME,SUMAYE,MALECHELA,LOWASSA,MAJALIWA ,POMBE wote hakuna mchagga lakini watu wanalia wachaga wanapendelewa na huyu wa sasa ameamua kuwakomoa kuanzia kwenye siasa,ajira,teuzi zake .
Hajateua :-
Waziri yeyote toka Kilimanjaro.

Hajateua Balozi toka Kilimanjaro

Hajateua Kamishna yeyote mambo ya usalama toka kilimanjaro.

Hajateua Mkurugenzi yeyote wa Bodi toka Kilimanjaro na hawa madokta kila siku anateua anawapiga chini wote toka kilimanjaro.


Kumbuka Wachaga ni wapambanaji,Mwaka huu wamevunja rekodi ya mwka 2000. Wanarud Moshi kwa wingi kwenda kutoa sadaka za shukrani na pia kuelezea wakichokuwa wanafanya mjini.

Wanakabidhiwa majukumu mapya ya kusomesha wadogo zao na ndugu wasio jiweza.

Wanandaliwa kisaikolojia kwa chuki dhidi yao na sasa wanajua la kufanya,KWA KIFUPI HAWANA TOFAUTI NA TAIFA LA ISRAELI NA HUYO MTESI WAO NI FARAO ambaye baadae ataishia kama farao
Mchagaaa.
Jadili hoja za kuvunjwa katiba/sheria sio mambo ya ukabila.
 
Mchagaaa.
Jadili hoja za kuvunjwa katiba/sheria sio mambo ya ukabila.
Raisi hajavunja Sheri, ibara ya 109 ya Katiba inatoa exception kuteua mtu yeyote iwapo ataona inafaa, awe mwanasheria wa Serikali, sema mambo ya USUKUMA ndiyo yanamuangusha
 
Raisi hajavunja Sheri, ibara ya 109 ya Katiba inatoa exception kuteua mtu yeyote iwapo ataona inafaa, awe mwanasheria wa Serikali, sema mambo ya USUKUMA ndiyo yanamuangusha
Hakuna ushahidi unaothibitika kisheria kwamba alimteua kwa sababu ya usukuma wake.
 
Mchagaaa.
Jadili hoja za kuvunjwa katiba/sheria sio mambo ya ukabila.
Raisi hajavunja Sheri, ibara ya 109 ya Katiba inatoa exception kuteua mtu yeyote iwapo ataona inafaa, awe mwanasheria wa Serikali, sema mambo ya USUKUMA ndiyo yanamuangusha
 
Hapa naona Mhe. Rais alikosa washauri. NImesoma katika affidavit kuwa ili uwe Mwanasheria Mkuu wa Serikali lazima uwe umekuwa Wakili kwa muda usiopungua miaka 15 lakini naona kama wameandika kuwa ana miaka 7 katika Uwakili wake. Sijui hili watalimalizaje. Watendaji muwe mnamshauri vizuri Mhe. Rais wetu.
Ibara ya 109 Naskia imeboronganya ulazima na kusema sasa yeyote tu ambaye Ataona inafaa eti
 
Hivi huyu ni mgeni kwenye nchi hii! Kama anaielewa vema nchi hii, basi hawezi poteza muda wake kufungua hii kesi. Anyway, muache aendelee kupaka hewa rangi.
 
Raisi hajavunja Sheri, ibara ya 109 ya Katiba inatoa exception kuteua mtu yeyote iwapo ataona inafaa, awe mwanasheria wa Serikali, sema mambo ya USUKUMA ndiyo yanamuangusha
Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mashitaka, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali ni vyeo vya Kikatiba hivyo Jiwe hana luxury ya kuteua tu wahutu wenzie kadri anavyopenda yeye
 
Hivi Wakati Jaji Stephen Werema anateuliwa Kuwa AG alikuwa Ni Wakili Wa Mahakama Kuu? Kama Alikuwa ni Wakili Wa Mahakama Kuu Alikuwa Na Mda Gani Toka aapishwe Kuwa Wakili Wa Mahakama Kuu?
Kwani hawa wapinzani wanashida gani na AG jamani! Mbn wale waliokuwa wanaingia mikataba ya ajabu ajabu hawakuwa na matatizo nao. Au kwa kuwa kakaza walizoea kuiangusha serikali, yaani wapinzani bana wako selfishi sana. Hiki sijui kiado kinatafutaga sana attention ya watu. Hahaha umaarufu kupitia migongo ya watu!
 
ADO SHAIBU v MAgufuli ,Dr.Kilagi
nimesoma na kusoma katiba ya jamhuri ya muungano kifungu cha 59 and 46 nimegundua yafuatayo 1.sifa za mwanasheria mkuu wa serikali ni tatu 1. ni lazima awe mtumishi wa umma 2.awe na sifa za kufanya kazi kama wakili(awe wakili kamili au alifaulu mtihani wa Bar au law school kwa sasa).3.awe na sifa hizo kwa miaka isiyopungua 15.sa hapo dr kilagi inabidi athibitishe hizo sifa tatu.Je ni sahihi kumuunganisha rais kwenye kesi ya kikatiba kwa hakika katiba ipo kimya juu ya hilo hivyo pingamizi tarajiwa la serikali litahitaji kuwa imara sana na pia jaji atakayesilikiliza atahitaji kuwa na huruma kwa serikali kulikubali maana kinga imetolewa kwenye makosa ya jinai na yale ambayo ni ya kibinafsi uteuzi si jambo binafsi ni capacity kama mkuu wa serikali.Hivyo kesi hii ni nzuri si tu itakuwa lazima kushinda bali itaifanya serikali kuwa makini kabla ya kufanya maamuzi.Ushindi itkuwa ni aibu kubwa sana kwa nchi hivyo mahakama itahitaji kuwa na jicho la kizalendo kwa kutetea katiba hata kama mbingu zitaanguka bila kujali nani atapata aibu ili makosa hayo yasijirudie tena.
 
Nawaza Sana Jinsi Applicant Kwa Maana Ya Ado Shaibu atavyoweza Kumsave John Joseph Magufuli Wito Pamoja Na Madai Ya Kuitwa Mahakamani.
....
Maana Magufuli Kashitakiwa Yeye Kama Yeye Kwa Jina Lake Kwa Hiyo Inabidi Akamkabidhi Yeye Na Amsainishe Ili Uwe Ushahidi Mahakamani Kwamba Mdai Wa Kwanza amepokea Wito
 
Iwapo mashtaka zaidi yakafunguliwa dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulingana na makosa ya kikatiba ambayo anakuwa amevunja itapelekea kujitathmini na kujaribu kutovunja sheria za nchi na katiba kwa ujumla. Pia huenda hatua hii ikafanya hata wasaidizi wa mhe. Rais kujitafakari na kujitahidi kufuata sheria za nchi na katiba kwa ujumla.
Wenyewe husema ukiona kiza kinazidi ujue kuna karibia kukucha.
 
Nimepata habari kuwa Ndugu Ado Shaibu wa ACT-Wazalendo ametoa maelekezo kwa mwanasheria wake Bibi Fatma Karume kumfungulia mashtaka mahakamani mwanasheria mkuu wa Serikali Dr. Kilangi na Rais Magufuli kutokana na Rais kumteua Dr. Kilangi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati ambapo Dr. Kilangi hana sifa za kuwa mwanasheria mkuu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 59 (2) ya katiba ya Tanzania, mtu anakuwa na sifa za kuwa mwanasheria mkuu wa serikali iwapo ana sifa zifuatazo;

(1) Ni mtumishi wa Umma mwenye sifa za kufanya kazi za wakili na amekuwa na sifa hii mfululizo kwa muda wa miaka 15.

(2) Ni wakili au mtu mwenye sifa za kuwa wakili na amekuwa na sifa hii mfululizo kwa muda wa miaka 15.

Swali ni je Dr. Kilangi ana sifa hizi? Kadri nijuavyo mimi ni kuwa Dr. Kilangi hana sifa hizi.

Kwanza, ukisoma wasifu (CV) ya Dr. Kilingi haioneshi mahala popote kuwa aliwahi kufanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma ambayo inamfanya kuwa na sifa za kuwa wakili kama vile mwanasheria wa serikali, mwendesha mashtaka wa serikali au mwanasheria wa serikali za mitaa au kazi nyingine za sheria katika utumishi wa umma kama zilivyo tajwa na masharti ya kifungu cha 3 (2) cha sheria ya mawakili, Sura ya 341 au masharti ya Sheria ya ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (Kutimiza Majukumu), 2005 au Sheria ya huduma ya mashtaka ya taifa, 2008. Kutofanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma moja kwa moja inamnyima Dr. Kilangi sifa ya kuwa na sifa hii kwa muda wa miaka 15 mfululizo. Mpaka hapo Dr. Kilangi ameshapoteza sifa ya kwanza ya kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pili, kumbukumbu kutoka chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) zinaonesha kwamba Dr. Kilangi ni wakili mwenye Roll No. 2022 ambaye alipata uwakili tarehe 8 October 2011, hivyo bado Dr. Kilangi hajafikisha muda wa miaka 15 mfululizo tangia alipoapishwa kuwa wakili wa mahakama kuu na wakati anateuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali alikuwa bado hajafikisha miaka 15 mfululizo tangia amekuwa wakili.

Kutokana na maelezo haya ni wazi kabisa kuwa Dr. Kilangi hachomoki kwenye mtego huu labda tu kama ataweza kuchomokea kwenye sifa ya kwanza ya kufanya kazi ya sheria katika utumishi wa umma maana kwenye sifa hii sina ushahidi wa kutosha.

Kama huu ndo ukweli basi ni masikitiko yangu kwa taifa kumpoteza mwanasheria mkuu mbobezi katika sheria ya mafuta, gesi asilia na madini, mtu huyu tuna muitaji sana kulisaidia taifa katika sekta za mafuta, gesi asilia na madini, hivyo basi, ni imani yangu kuwa mhe. Rais atamteua kuwa mwanasheria kwenye nafasi nyingine katika sekta ya mafuta na gesi asilia au madini iwapo mahakama itaamua kuwa uteuzi wake kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ni batili.

Ushauri wangu kwa Mhe. Rais ni kuwa iwapo nafasi ya mwanasheria mkuu itabaki wazi basi kwa heshima na taadhima ninakushauri kuwa kwa mtizamo wangu watu wanao weza kuimudu nafasi ya mwanasheria mkuu wa serikali ni moja wapo katika ya watu (mawakili) watatu wafuatao;

(1) Francis Stolla (Rais mara 3 mfululizo wa TLS)

(2) Audax Kaendaguzi ( Mwandishi maarufu wa vitabu vya sheria na amicus curie wa mahakama ya rufaa)

(3) Dr. Onesmo Kyauke ( Mhadhiri wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam).

Sitataja au kueleza sifa za watu hawa maana Mhe Rais kwa kutumia vyombo vyake vya kimkakati ataweza kupata sifa za watu hawa.

Pia, Jaji Kiongozi, Dr. Feleshi anafaa kuwa mwanasheria mkuu lakini kwa wadhifa wake sio busara kumteua kuwa mwanasheria mkuu.

Ni hayo tu Mhe. Rais.

SHAHADA YA SHERIA (LL.B) PEKEE HAIMFANYI MTU KUWA NA SIFA ZA KUWA WAKILI.

Kuna wanasheria na wanasiasa hata raia wa kawaida wanaamini au kuaminishwa kuwa kupata shahada ya kwanza ya sheria (LL.B) pekee inamfanya mtu kuwa na "sifa za kuwa wakili" kwa minajiri ya kuteuliwa ya kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali. Watu wanaounga mkono hoja hii wanasema kuwa Dr. Kilangi alipata shahada ya kwanza ya sheria mwaka 2000 hivyo alikuwa na sifa za kuwa wakili kuanzia mwaka 2000, hii ikiwa na maana kwamba wakati anateuliwa kushika wadhifa wa mwanasheria mkuu tiyari alikuwa na zaidi ya miaka 15 akiwa na sifa za kuwa wakili. Wapinzani wa hoja hii wanasema kuwa Dr. Kilangi alipata sifa za kuwa wakili baada ya kufaulu bar examinations chini ya Baraza la Elimu ya sheria na kuwa wakili mwaka 2011 hivyo bado hajafikisha miaka 15 ya uwakili au ya kuwa na sifa za kuwa wakili. Maoni yangu kuhusu swala la shahada ya kwanza ya sheria kumpa mtu sifa za kuwa wakili ni kama ifuatavyo;

Ibara ya 59 (2) ya katiba imeweka masharti kuwa ili mtu ateulie kuwa mawanasheria mkuu wa serikali lazima awe "wakili" au awe na "sifa za kuwa wakili". Swala la kuwa "wakili" halina utata liko wazi mno na haliitaji mjadala kabisa na swala lenye utata ni mtu mwenye "sifa za kuwa wakili". Mtu mwenye shahada ya kwanza ya sheria hana kabisa "sifa za kuwa wakili" kwa sababu sheria mbili zinataja kwa uwazi mtu mwenye sifa za kuwa wakili. Sheria zimeweka aina tano (5) za watu wenye sifa za kuwa wakili kama ifuatavyo;

Kwanza, "mtu mwenye Post-Graduate Diploma in Legal Practice" ambayo imetolewa na Law School of Tanzania ana sifa za kuwa wakili, hii ni kwa mujibu wa section 12 (3) of the Law School of Tanzania Act, 2007 (sheria Na. 18 ya 2007). Na mtu kamwe hawezi kupata Post-Graduate Diploma in Legal Practice" ambayo imetolewa na Law School of Tanzania mpaka awe na shahada ya sheria au sifa zingine za kitaalum ambazo zinatambuliwa na Baraza la Elimu ya Sheria (Council for Legal Education), hii ni kwa mujibu wa section 11 (1) (a) and (b) of the Law School of Tanzania Act, 2007

Pili, mtu ambaye ana shahada ya sheria ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki au chuo kikuu chochote ambacho kinatambuliwa na Baraza la Elimu ya Sheria na awe amefauli "Bar examinations" inayosimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria , na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (i) and (b) (i) of the Advocate Act, Cap. 1.

Tatu, Mtu ambaye amekuwa wakili Zanziba, Kenya na Uganda kwa kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya kufanya maombi ya kuwa wakili, na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (i) and (b) (i) of the Advocate Act, Cap. 1.

Nne, mtu ambaye ni wakili wa mahaka zisizokuwa na mipaka ya mamlaka katika maswala ya jinai na madai katika nchi za jumuia ya madola au nchi nyingine zilizoteuliwa na waziri wa sheria kwa ajiri hiyo, na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (ii) of the Advocate Act, Cap. 1.

Tano, mtu ambaye ni solisita (solicitor) wa mahakama ya juu ya Uingereza (England), Northern Ireland, Jamhuri ya Ireland na Scotland (United Kingdom).

Hivyo basi, hitimisho langu ni kuwa mtu mwenye shahada ya sheria (LL.B) kamwe hawezi kuwa na sifa za kuwa wakili mpaka apate Post-Graduate Diploma in Legal Practice Kutoka Law School of Tanzania au afaulu mitihani inayosimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria (Council for Legal Education) au awe amekuwa wakili au solisita katika nchi za jumuia ya madola au awe amekuwa wakili katika Kenya, Zanzibar na Uganda kwa kipindi cha miaka mitano.
 
Back
Top Bottom